• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Miradi yenye Thamani ya Milioni 132 yakaguliwa Kibindu

Imewekwa: August 14th, 2018

Kamati ya Elimu,Afya na Maji ya Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze imefanya ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo katika sekta za Afya na Elimu katika kijiji cha Kibindu kata ya Kibindu hivi karibuni,ziara hiyo ni ziara ya kukamilisha robo ya nne ya mwaka wa fedha 2017/2018.

Kamati hiyo ikiongozwa na Mwenyekiti Mheshimiwa Malota Hussein ilipitia na kukagua ujenzi wa vyumba vya madarasa vinne vinavyojengwa kwa ufadhili wa shirika la hifadhi ya Taifa TANAPA na ujenzi wa madarasa mawili na ofisi vinavyojengwa na halmashauri kwa kushirikiana na Benki ya NMB,miradi hii yote iliyopitiwa na kamati ilikuwa na thamani ya fedha za kitanzania milioni 132.

Kamati pia ilikagua na kuona eneo la zahanati ya Kibindu ambalo litaanza kujengwa kwa kuongezewa miundombinu ya afya ambayo ni maabara,Jengo la upasuaji na Jengo la Mama na Mtoto.Miundombinu itaanza kujengwa hivi karibuni kutokana na fedha iliyotolewa na serikali kuu jumla ya fedha za kitanzania milioni 400.

Mwenyekiti wa Kamati Mheshimiwa Malota alitoa ushauri kwa wataalamu na wasimamizi wa ujenzi wa madarasa yanayoendelea kujengwa kuzingatia ubora na ubora huo uendane na thamani ya fedha inayotumika yaani “Value for Money.”

Naye Mwenyekiti wa kamati ya shule ya Msingi Kibindu Bi Halma Mazige alipokuwa akizungumza mbele ya wajumbe wa kamati ya Elimu,Afya na Maji alieleza changamoto zinazoikabili shule yake ikiwa ni pamoja na upungufu wa walimu 25,vyumba vya madarasa 25.”Kutokana na wingi wa wanafunzi katika shule hii naiomba halmashauri iweze kusaidia katika ukamilishaji wa miundombinu ya kujifunzia na kufundishia ili elimu bora iweze kutolewa.”Mazige alisema.

Kwa upande wake Diwani wa kata ya Kibindu Mheshimiwa Ramadhani Mkufya aliishukuru kamati ya huduma za jamii kwa kufika katika kata yake na kujionea changamoto zinazoikabili sekta za Elimu na Afya na kutoa ombi kwa kamati ili kukamilisha madarasa yanayojengwa na kuanza kujenga miundombinu ya afya ili kuondokana na kero mbalimbali zinazowakabili wananchi wa Kibindu.

Hata hivyo Mwenyekiti wa Kamati ya Afya ,Elimu na Maji Mheshimiwa Malota Hussein aliwaagiza wataalam kufanya tathmini ya ujenzi na kubaini gharama zinazohitajika ili kukamilisha ujenzi huo ili kuiwasilisha katika vikao vya maamuzi kwa hatua zaidi.


Madiwani na Wataalam wakikagua Ujenzi wa madarasa shule ya Msingi Kibindu,Kata ya Kibindu

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • PPRA yatoa Mafunzo ya NeST kwa Watendaji wa Kata na Wakuu wa Shule Chalinze

    May 08, 2025
  • Watendaji wa Kata na Vijiji wapewa Mafunzo ya namna ya kukusanya Kodi ya Majengo Chalinze

    May 07, 2025
  • PPRA yatoa mafunzo ya Ununuzi kwa watumishi wa Afya Chalinze

    May 07, 2025
  • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango yafanya ziara kukagua miradi ya maendeleo

    May 06, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.