• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Mkakati wa Kudhibiti Magonjwa ya Mifugo Wazinduliwa Kitaifa

Imewekwa: August 3rd, 2018

Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Mheshimiwa Luhaga Mpina amezindua Mkakati wa Kudhibiti Magonjwa ya Mifugo na Matumizi ya Dawa,Chanjo na Viuatilifu vya Mifugo kitaifa katika kijiji cha Chamakweza katika Halmashauri ya Chalinze Mkoani Pwani hivi karibuni.

Katika uzinduzi huo Mheshimiwa Mpina amechukua hatua za makusudi kutokana na umuhimu wa sekta ya mifugo nchini ili kuondoa umasikini,kuchangia katika kuhakikisha usalama wa Chakula,kutengeneza ajira pamoja na kuwa na hazina kubwa ya rasilimali mifugo katika taifa.”Sekta ya Mifugo inakabiliwa na Changamoto nyingi ikiwa ni pamoja na vifo vingi vya Mifugo vinavyosababishwa na magonjwa mengi hususan yale yanayoenezwa na kupe na yale ya mlipuko.Changamoto hizo zinasababisha Sekta ya Mifuo kutokuwa na tija hivyo kutochangia katika pato ghafi la taifa kama inavyotarajiwa.”Mpina alisema.

Katika kukabiliana na changamoto hizo mkakati ulioandaliwa unalenga kufanya mapitio ya Sheria na kanuni mbalimbali,kuweka utaratibu utakaohakikisha upatikanaji wa dawa,chanjo na viuatilifu muhimu nchini ikiwa ni pamoja na kuimarisha Taasisi ya Chanjo(TVI Kibaha),kutoa elimu na kuhamasisha wafugaji na wadau juu ya udhibiti wa magonjwa,kuimarisha mfumo wa utambuzi na uchunguzi wa magonjwa ya wanyama,kuimarisha vitengo vya ukaguzi na ufuatiliaji na kuendeleza miundombinu ya majosho kwa kujenga na kukarabati yaliyopo, Waziri Mpina alisisitiza katika hotuba yake ya uzinduzi wa mkakati wa kudhibiti magonjwa ya mifugo nchini.

Aidha katika hotuba yake aliziagiza mamlaka za serikali za mitaa nchini kusimamia zoezi la uogeshaji mifugo na kukarabati miundombino ya majosho nchini ili kutekeleza kwa vitendo mkakati wa kuboresha sekta ya mifugo nchini,ameziagiza halmashauri nchini kote kukarabati majosho ifikapo tarehe 30/12/2018 halmashauri zote nchini ziwe zimekarabati majosho” kwa halmashauri zitakazoshindwa kutekeleza kwa mamlaka niliyonayo nitazifungia kukusanya mapato yatokanayo na mifugo” Waziri Mpina alisema. Pia aliwataka maafisa ugani au watendaji wa sekta ya mifugo kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa sheria ili kuwahudumia wafugaji kwa lengo la kuijengea tija sekta ya mifugo.

Kwa upande wake Katibu wa Chama cha Wafugaji Tanzania Bwana Magembe Makoye aliishukuru serikali ya awamu ya tano kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kuzindua Mkakati bora unaolenga kuiboresha na kuiimarisha sekta ya mifugo nchini na kuiwezesha kuzalisha ili kuunga mkono jitihada za serikali za uendelezaji viwanda kwani sekta ya mifugo ni chimbuko la malighafi za viwandani.

Hata hivyo Makoye alimwomba waziri katika mkakati wake wa kuboresha sekta ya mifugo ayalinde maeneo yaliyotengwa kwa shughuli za ufugaji nchini ili kuondokana na migogoro inayoweza kutokea kwa kubadili matumizi ya ardhi kinyume cha sheria na kuomba idhini kwa niaba ya wafugaji ili waruhusiwe kuchungia maeneo ya Ranchi za taifa kipindi cha ukame na ukosefu wa nyasi ili kuinusuru mifugo wakati wa njaa.

   Naye Mkurugenzi wa Mifugo nchini Dkt.Martin Ruheta alitoa ufafanuzi wa Mkakati wa Kudhibiti Magonjwa ya Mifugo na matumizi ya Dawa,Chanjo na Viuatilifu lengo likiwa ni kupambana na magonjwa ya mifugo kama Mdondo(ND),Ndigana kali(ECF) na Homa ya Mapafu ili ufugaji nchini uwe ufugaji wa tija na endekevu.Aliendelea kusisitiza kuhusu mkakati huu kuwa wizara ya mifugo imejiandaa kuwekeza katika kiwanda cha chanjo cha Kibaha(TVI) ili chanjo zote Muhimu nchini zizalishwe ndani ya nchi ili kumwondelea mfugaji kero ya upatikanaji chanjo na dawa za mifugo.

Aidha Mkurugenzi Ruheta alisistiza Mkakati huu utatekelezeka kwani wizara imejipanga kujenga majosho na kukarabati yaliyopo na kila halmashauri nchini inatakiwa kukarabati majosho na kusimamia zoezi la uogeshaji mifugo na utoaji chanjo mbalimbali za mifugo,Kuimarisha  mfumo wa utambuzi na uchunguzi wa magonjwa ili kubaini na kuchukua hatua kwa wakati,Ukaguzi na udhibiti-dawa,chanjo na viuatilifu ili kuwa na dawa na viuatilifu vyenye  ubora na viwango vinavyotakiwa.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Chamakweza Bwana Mika Laini kwa niaba ya wananchi na wafugaji wa kijiji chake aliishukuru serikali ya awamu ya tano kwa Mkakati wa kuboresha sekta ya Mifugo na kuwajali wafugaji kwa kuwahakikishia upatikanaji wa dawa za mifugo kwa bei nafuu na zenye ubora unaotakiwa.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi katika picha ya Pamoja na Wafugaji wa Kijiji cha Chamakweza katika Halmashauri ya Chalinze Mkoani Pwani

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango chafanya kikao kujadili mapato na matumizi kwa mwezi Aprili 2025.

    May 31, 2025
  • Maafisa Habari watakiwa kuitangaza miradi ya serikali

    May 30, 2025
  • Halmashauri ya Chalinze yatembelewa na wawekezaji wa nyumba

    May 29, 2025
  • Kampeni ya "Ni rahisi sana"yatoa Elimu kuhushu usalama Mtandaoni Chalinze

    May 28, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.