• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Mkurugenzi Mtendaji Chalinze Atembelea maonyesho ya 49 ya Saba saba

Imewekwa: July 14th, 2025


Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze, Bwana Ramadhani Possi, leo hii ametembelea maonyesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam. Maonyesho hayo ambayo yanashirikisha taasisi mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi, yamekuwa jukwaa muhimu la kuonesha fursa za kiuchumi, uwekezaji na ubunifu wa ndani.


Katika ziara yake, Mkurugenzi Possi alitembelea banda la Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze, ambalo kwa mara ya kwanza limepata fursa ya kushiriki maonyesho hayo makubwa kitaifa. Banda hilo linaonesha huduma mbalimbali zinazotolewa na halmashauri hiyo, mafanikio ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo pamoja na fursa za uwekezaji zilizopo katika maeneo ya kilimo, ufugaji, viwanda na utalii wa kiutamaduni.


Akizungumza mara baada ya kutembelea banda hilo, Bwana Possi alisema ushiriki wa Chalinze katika maonyesho ya Sabasaba ni hatua kubwa katika kutangaza fursa na kuvutia wawekezaji. Aliongeza kuwa banda hilo limetengenezwa kwa ubunifu na limejikita katika kutoa taarifa sahihi kwa wananchi, wawekezaji na wadau mbalimbali kuhusu huduma na maendeleo ya halmashauri.


Mkurugenzi huyo pia alipata fursa ya kuzungumza na watumishi wa halmashauri waliopo kwenye banda hilo, ambapo aliwataka kuhakikisha wanatumia vyema fursa hiyo ya maonesho kwa kutoa elimu na taarifa sahihi kuhusu huduma za serikali ngazi ya halmashauri. Alisisitiza kuwa maonesho hayo ni nafasi muhimu ya kujifunza kutoka kwa taasisi nyingine na kuimarisha utoaji wa huduma kwa wananchi wa Chalinze.


Ushiriki wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze katika maonyesho ya Sabasaba kwa mara ya kwanza unaonesha dhamira ya dhati ya uongozi wa halmashauri hiyo katika kufungua milango ya ushirikiano, uboreshaji wa huduma, pamoja na kukuza maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa wananchi wake. Banda la Chalinze linaendelea kupokea wageni na wadau mbalimbali waliovutiwa na mafanikio na mikakati ya halmashauri hiyo.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • TANGAZO LA KAZI June 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Mkurugenzi Mtendaji Chalinze Atembelea maonyesho ya 49 ya Saba saba

    July 14, 2025
  • Walimu wapewa maelekezo ya kazi Chalinze

    July 10, 2025
  • Kampeni ya Ugawaji vyandarua bila malipo yazinduliwa Chalinze

    July 10, 2025
  • Waziri Dkt Kijaji Azindua Kampeni ya Chanjo ya Mifugo Kitaifa Mkoani Pwani

    July 09, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.