• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Chalinze afanya mazungumzo na Walimu wa Michezo na Wanafunzi watakao shiriki UMITASHUMTA Mkoa wa Pwani

Imewekwa: May 29th, 2021

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Chalinze Ndugu: Ramadhani Possi amekutana na Walimu wa michezo na wanafunzi wapatao 76 (Wasichana 36 na Wavulana 40) wa Shule za msingi waliochaguliwa kuiwakilisha Halimashauri ya Chalinze katika mashindano ya michezo kwa shule za msingi (UMITASHUMTA) yatakayo fanyika Kibaha Mkoani Pwani kuanzia Tarehe 30.05.2021. Hayo yamefanyika leo katika hafla fupi ya kuwaaga wanamichezo hao iliofanyika katika viwanja vya Halmashauri. Ndugu Possi alikutana na wanafunzi kwa lengo la kuongeza hamasa na kuwapa moyo wanapoelekea katika michuoano ya UMITASHUMTA ili waweze kufanya vizuri katika michuano hiyo na kupelekea Chalinze kuwa kinara katika sekta ya Michezo

Nae Afisa Elimu Msingi  Wilaya Bi. Zainabu Makwinya akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Mkurugenzi Mtendaji kuzungumza na wanamichezo waliochaguliwa kuiwakilisha Halmashauri ya Chalinze katika Michuano ya UMITASHUMTA Mkoa wa Pwani alisema “Kuna jumla ya Wanafunzi 76 na walimu wa Michezo 7 wanaokwenda Kibaha kushiriki mashindano ya mchujo kwa lengo la kupata timu ya Mkoa wa Pwani watakaoshiriki katika michuano hiyo kitaifa inayotegemea kufanyika Mkoa wa Mtwara. Zipo changamoto nilizo zifikisha kwako ikiwemo ufinyu wa bajeti hivyo tunaomba kwa nafasi yako kama mkuu wa taasisi uone namna ya kuwezesha watu hawa(Walimu wa Michezo) ili wapate motisha wa kuendelea kufundisha na kusimamia michezo kwa wanafunzi ili kufanya Halmashauri kuwa kinara katika sekta ya michezo kati ya Halmashauri zote za Mkoa wa Pwani.

Akizungumza na Walimu na Wanafunzi hao Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Chalinze Ndugu, Ramadhani Possi alisema “ Napenda kutoa pongezi zangu za dhati kwa uongozi wa Elimu Msingi Wilaya, Walimu wa michezo na Wanafunzi wote mliochaguliwa kuwakilisha Chalinze katika Michuano ya UMITASHUMTA Mkoa wa Pwani. Wito wangu kwenu ni kuwa fuateni maelekezo na mafunzo mliopewa na walimu wenu, mshiriki michezo hiyo kwa adabu utii na nidhamu ya hali ya juu ili mtuwakilishe vyema, kwani mkifanya vizuri jina la Chalinze kimichezo likuwa na kama mtafanya vibaya aibu itakuwa kwa uonguzi wa Halmashauri hususani Mkurugenzi Mtendaji’’.

Ndugu, Ramadhani Possi aliongeza kusema "ziko faida nyingi kwa ninyi kama wanafunzi kujihusisha katika michenzo ikiwa ni pamoja na kujenga afya, kudumisha umoja na kuongeza watu wapya wa kufahamiana nao(Connection) , Kukua na kukomaa kiakili na hata kujiajili kupitia michezo. Tofauti na miaka ya nyuma sasa mchezaji anaweza kutumia kipaji chake kujipatia kipato na sehemu sahihi ya kukuza kipaji hicho ni pamoja na kushiriki katika michuano mbalimbali ikiwemo UMITASHUMTA".

Ndugu: Ramadhani Possi alikili kupokea changamoto mbalimbali za uendeshaji wa mashindano hayo na kuahidi uongozi wa Elimu Msingi na Afisa Michezo na Utamaduni kuwa changamoto hizi zitatatuliwa kabla au ifikapo siku ya Jumanne wiki inayokuja,

Akihitimisha mazungumzo na wanamichezo hao Ndugu Possi aliwatakia safari njema  na yenye mafanikio waendapo huko Kibaha kwenye mashidano ya michezo (UMITASHUMTA).

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • PPRA yatoa Mafunzo ya NeST kwa Watendaji wa Kata na Wakuu wa Shule Chalinze

    May 08, 2025
  • Watendaji wa Kata na Vijiji wapewa Mafunzo ya namna ya kukusanya Kodi ya Majengo Chalinze

    May 07, 2025
  • PPRA yatoa mafunzo ya Ununuzi kwa watumishi wa Afya Chalinze

    May 07, 2025
  • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango yafanya ziara kukagua miradi ya maendeleo

    May 06, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.