• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Chalinze Ramadhani Possi afanya kikao na wafanyabiashara wa Chalinze.

Imewekwa: January 29th, 2026

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze, Bwana Ramadhani Possi, amefanya kikao kazi na wafanyabiashara wa Mamlaka ya Mji Mdogo wa Chalinze kwa lengo la kutoa elimu kuhusu masuala ya biashara, kodi na uzingatiaji wa sheria na taratibu za biashara.

Kikao hicho kimefanyika Jana katika Ukumbi Mdogo wa Mkurugenzi uliopo Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze, kikilenga kuwajengea uelewa wafanyabiashara juu ya wajibu wao kama walipa kodi na umuhimu wa kufanya biashara kwa kuzingatia sheria.

Katika kikao hicho, wafanyabiashara walipatiwa elimu kuhusu mchakato wa kuanzisha biashara, ukataji wa leseni za biashara pamoja na vigezo vinavyotakiwa kuzingatiwa. Akitoa elimu hiyo, Afisa Biashara wa Halmashauri, Bi. Zamzam Kabogota, aliwasisitiza wafanyabiashara kuhakikisha wanakata leseni za biashara kwa wakati na kuhuisha leseni hizo mara tu muda wake unapokwisha.

Kwa upande wake, Afisa Biashara Shukuru Masenga alitoa elimu kuhusu ushuru wa huduma, akieleza faida za ulipaji wa ushuru huo kwa wafanyabiashara na kwa maendeleo ya halmashauri kwa ujumla. Masenga alifafanua kuwa kuanzia mwezi Julai 2025, kiwango cha ushuru wa huduma kimepunguzwa kutoka asilimia 0.3 hadi asilimia 0.25, hatua iliyochukuliwa na Serikali kwa lengo la kuwapunguzia mzigo wafanyabiashara.

Naye Mkuu wa Idara ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji, Bi. Prisca Mtendamema, aliwaeleza wafanyabiashara umuhimu wa kulipa kodi na ushuru mbalimbali kwa Halmashauri, akibainisha kuwa mapato hayo huiwezesha Halmashauri kutoa huduma muhimu kwa wananchi ikiwemo ujenzi wa zahanati, shule, madarasa na ufungaji wa taa za barabarani.

Aidha, Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Sheria cha Halmashauri, Wakili Rose Kamugisha, aliwakumbusha wafanyabiashara kuzingatia sheria za nchi kwa kulipa kodi na ushuru stahiki kwa mujibu wa Sheria ya Fedha za Serikali za Mitaa, Sura ya 290, kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2023.

Kwa ujumla, kikao hicho kimeongeza uelewa kwa wafanyabiashara kuhusu masuala ya kodi na biashara, na kuimarisha ushirikiano kati ya Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze na wafanyabiashara.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • TANGAZO LA KAZI June 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • TRA yatambulisha Mfumo wa Kielektroniki wa Usimamizi wa Kodi (IDRAS)

    January 29, 2026
  • TRA yatambulisha Mfumo wa Kielektroniki wa Usimamizi wa Kodi (IDRAS)

    January 29, 2026
  • Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Chalinze Ramadhani Possi afanya kikao na wafanyabiashara wa Chalinze.

    January 29, 2026
  • Maadhimisho ya kuzaliwa Kwa Rais Mhe. Dkt, Samia Suluhu Hassan Halmashauri ya Chalinze yaungana nae katika upandaji wa miti.

    January 28, 2026
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.