• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Mkutano Mkuu wa Kijiji cha Tukamisasa waazimia Mwenyekiti Kupisha Uchunguzi

Imewekwa: June 10th, 2025


Na John Mlyambate

Kijiji cha Tukamisasa, wilayani Bagamoyo, kimetawaliwa na mvutano mkubwa baada ya Mkutano Mkuu wa Kijiji hicho, uliofanyika hivi karibuni, kuazimia Mwenyekiti wa Kijiji, Bwana Ramadhani Zahaki, asimame kazi ili kupisha uchunguzi dhidi ya tuhuma mbalimbali zinazomkabili.


Mkutano huo uliitishwa na Mwenyekiti Zahaki mwenyewe kwa lengo la kujadili na kupokea kero mbalimbali za wananchi, na kufanyika katika ofisi ya kijiji hicho mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Mheshimiwa Shaibu Ndemanga.


Katika kikao hicho, wananchi walipata nafasi ya kueleza matatizo yao hadharani, ambapo Bwana Malaki Mamungiti, ambaye ni Mwenyekiti wa wafugaji wa kijiji hicho, aliibuka na tuhuma nzito dhidi ya Mwenyekiti Zahaki, akidai amekuwa akijimilikisha ardhi ya kijiji kinyume cha sheria.


Malaki alidai kuwa Mwenyekiti huyo anamiliki zaidi ya ekari 500 ambazo anazidai kuwa ni za familia yake, akitumia nafasi yake vibaya kwa maslahi binafsi, jambo linalokiuka taratibu za kisheria na kiutawala.


Mbali na suala la ardhi, Malaki alieleza kuwa Mwenyekiti huyo amekuwa akiwaingiza wawekezaji kwenye vitega uchumi vya kijiji bila idhini ya vikao halali, huku akijipatia mapato yasiyo halali bila uwazi au ufuatiliaji wa fedha hizo.


Wananchi wengine pia walitoa tuhuma mbalimbali, akiwemo Mzee Mathias Mkundi, ambaye alisema kuwa Mwenyekiti Zahaki hana ushirikiano na Mtendaji wa Kijiji pamoja na Halmashauri ya Kijiji, hali inayozorotesha utendaji wa serikali ya kijiji.


Mzee Mkundi alieleza kuwa hakujawahi kufanyika kikao chochote cha kisheria tangu Mwenyekiti huyo aingie madarakani, hali inayomnyima mamlaka na sauti ya wananchi katika maamuzi ya kijiji.


Kwa upande wake, Mzee Ismail Lugoma, alieleza kuwa Mwenyekiti hajawahi kusoma mapato na matumizi ya kijiji hadharani, licha ya kijiji hicho kuwa na vyanzo vingi vya mapato vinavyoendelea kukusanya fedha.


Mzee Lugoma alipendekeza kuwa ni busara kwa Mwenyekiti Zahaki kupisha uchunguzi ili ukweli ubainike na hatua stahiki zichukuliwe, kwa kuwa hali ya sasa inarudisha nyuma maendeleo ya kijiji hicho.


Wananchi waliunga mkono hoja hiyo kwa kauli moja, wakimtaka Mkuu wa Wilaya kuingilia kati na kuhakikisha tume huru inaundwa kuchunguza tuhuma hizo, kwa lengo la kulinda maslahi ya umma na kurejesha imani ya wananchi kwa uongozi.


Kutokana na hali hiyo, Mkutano Mkuu wa Kijiji cha Tukamisasa uliamua rasmi kwamba Mwenyekiti Zahaki asimame kazi kwa muda, hadi uchunguzi kamili ufanyike, na walimkabidhi rasmi ombi hilo Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo.


Mkuu wa Wilaya, Mheshimiwa Shaibu Ndemanga, alikubaliana na ombi hilo na kutoa maelekezo kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze, ambaye aliiwakilishwa katika kikao hicho na Afisa Utumishi, kuunda tume ya uchunguzi mara moja.


Tume hiyo itapitia na kuchunguza tuhuma zote zilizotolewa na wananchi, zikiwemo za matumizi mabaya ya madaraka, ubaguzi, ukabila, ubadhirifu wa mali ya kijiji na uvunjaji wa taratibu za kiutawala.


Mkuu wa Wilaya alisisitiza kuwa tume hiyo itafanya kazi kwa weledi na itatoa ripoti ya uchunguzi mbele ya Mkutano Mkuu wa Kijiji cha Tukamisasa kwa ajili ya hatua zaidi, kuhakikisha haki na uwajibikaji vinazingatiwa.


Wananchi wa Tukamisasa walionyesha matumaini kuwa hatua hiyo ya kusimamishwa kwa Mwenyekiti Zahaki itasaidia kurejesha utawala bora na uwazi katika uongozi wa kijiji chao.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • TANGAZO LA KAZI June 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Madiwani wa Pangani waipongeza Chalinze kwa Miradi ya mapato ya ndani

    June 11, 2025
  • DC Ndemanga Aongoza Kikao cha Tathmini ya Utekelezaji wa Mkataba wa Lishe

    June 10, 2025
  • Mkutano Mkuu wa Kijiji cha Tukamisasa waazimia Mwenyekiti Kupisha Uchunguzi

    June 10, 2025
  • Waziri Kikwete atua Geneva kushiriki Mkutano wa 113 wa Shirika la kazi Duniani

    June 04, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.