• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Mkutano wa wadau wa Elimu wafanyika Chalinze

Imewekwa: September 20th, 2022


“Tunataka zawadi zinazotia moyo walimu na wamiliki wa shule katika Halmashauri ya Chalinze,tutoe zawadi zinazomotisha wadau wa elimu kama walimu ili kuwafanya watekeleze Majukumu yao kwa moyo mmoja. Hali kadhalika tuwapongeze wamiliki wa Shule ambao wameamua kuwekeza katika Elimu,wangeweza kuwekeza katika miradi mingine lakini wakaamua kujenga shule.” Mkuu wa wilaya alisema.


Maneno hayo yamesemwa na Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo ,   Mheshimiwa Zainabu Abdallah wakati akitoa hotuba ya uzinduzi wa kikao cha wadau wa Elimu leo katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari Lugoba.

Katika kikao hicho Mkuu wa wilaya amewataka viongozi wa Elimu kuwa mstari wa mbele katika suala zima la kujiendeleza kielimu ili waweze kutekeleza Majukumu yao kwa weledi na kutoa elimu bora kwa wanafunzi.


Katika kikao hicho cha wadau wa Elimu Mwenyekiti wa kikao hicho Mheshimiwa Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Zainabu Abdallah aliwataka Wakuu wa Idara za Elimu Msingi na Sekondari kutoa taarifa zao za utekelezaji wa Majukumu katika sekta za Elimu kwa kueleza ufanisi na changamoto zinazosababisha Halmashauri ya Chalinze kutofanya vizuri katika taaluma lakini pia ufumbuzi wa changamoto hizo ili kuinua kiwango cha ufaulu katika shule za Msingi na Sekondari.


Wakuu wa Idara hao walieleza changamoto mbalimbali katika ufundishaji na ujifunzaji ikiwa ni pamoja na wanafunzi wa Shule za kutwa kwa Shule za Sekondari kutopata chakula cha mchana hivyo wanafunzi kukosa usikivu katika kujifunza,upungufu wa walimu wa masomo ya sayansi wapatao 133 kusababisha wanafunzi kuwa na Msingi mbaya wa masomo haya tangu wakiwa vidato vya chini hali inayopelekea kuwa na ufaulu duni katika masomo ya sayansi,njia za ufundishaji zisizo rafiki wanazotumia walimu kama njia ya mhadhara,ukosefu wa vyumba vya maabara 43 unakwamisha ufundishaji wa masomo ya sayansi,upungufu wa nyumba za walimu kwa shule za Msingi na Sekondari,upungufu wa miundombinu ya Elimu kama nyumba za walimu,vyumba vya madarasa,na matundu ya vyoo,walimu kuishi mbali na shule,uelewa ndogo wa dhana ya Elimu bure kwa wazazi,na upungufu wa walimu waliosomea Elimu maalum katika Vitengo na Shule jumuishi.


Baada ya kuwasilishwa kwa changamoto zinazoikabili sekta ya Elimu katika Mkutano wa wadau wa Elimu,Mkuu wa wilaya aliruhusu mjadala wa wazi kwa wadau wa Elimu katika kutafuta ufumbuzi wa changamoto hizo ili kuweza kuinua ufaulu wa wanafunzi.


Wajumbe wa Mkutano huo walichangia hoja mbalimbali kama suluhisho na mwarobaini wa kuinua kiwango cha Elimu sanjari na kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia katika shule za Msingi na Sekondari kama madarasa,maabara,nyumba za walimu,upatikanaji wa walimu wa sayansi,madawati na motisha kwa walimu.


Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Chalinze aliwapongeza wadau wa Elimu kwa kuzichambua changamoto zinazoikabili sekta ya Elimu na kuwataka wadau wa Elimu kufanya kazi bega kwa bega na Halmashauri na wadau mbalimbali wa Elimu katika kutatua kero zinazoweza kuipandisha taaluma na hatimaye kutoka hatua tuliyonayo kwenda hatua nyingine.


Naye Katibu Tawala wa wilaya ya Bagamoyo Bi. Kasilda Mgeni alitoa maoni yake kwa kuwataka wazazi kama wadau wakubwa wa kuinua ufaulu wa mtoto kutimiza wajibu wao na siyo kuwaachia walimu pekee katika suala la kumlea mtoto.

“Wazazi tutimize wajibu wetu katika kuinua kiwango cha Elimu kwa watoto wetu pasipo kuwaachia walimu pekee,mwalimu ana nafasi yake katika kumlea mtoto na mzazi pia ana wajibu wake, tukitekeleza wajibu wetu kiwango cha Elimu kitapanda “. Katibu Tawala alisema.


Mwenyekiti wa Halmashauri alitoa mchango wake katika Mkutano wa wadau wa Elimu kwa kueleza mipango iliyo Pangwa na Baraza la Madiwani katika kuboresha miundombinu ya Elimu ikiwa ni pamoja na kuhamasisha wadau wa Maendeleo katika kuboresha miundombinu ya Elimu.


Mheshimiwa Mkuu wa wilaya alihitimisha Mkutano wa wadau wa Elimu kwa kusoma maazimio ya kikao hicho ambayo yatatekelezwa kwa wakati maalum na maazimio hayo yatawasilishwa katika kikao cha wadau wa Elimu kwa kipindi kinachofuata.


Aidha maazimio hayo ni pamoja na kutakuwa na kikao cha wadau wa Elimu mara mbili kwa mwaka ili kuweza kuyapima maazimio yaliyowekwa na vikao vya wadau wa Elimu,kutakuwa na maadhimisho ya wiki la Elimu yatakayojumuisha Halmashauri za Chalinze na Bagamoyo kwa kila mwaka kwa ajili ya kupima mafanikio na changamoto za Elimu sanjari na kutoa zawadi kwa shule zinazofanya vizuri na tunu kwa walimu wanafanya vizuri katika ufundishaji ,kila Shule ya Msingi na Sekondari suala la chakula ni la lazima kwa wanafunzi,kutakuwa na kamati ya Elimu itakayokuwa inakaa kila mwezi ili kupima ufanisi wa sekta ya Elimu na kamati hiyo itakuwa inapeleka taarifa zake katika Mkutano wa wadau wa Elimu kila kinapofanyika,madarasa yote ya mitihani kwa shule zenye mabweni watoto lazima wakae kambini kwa shule zisizo kuwa na mabweni shule ziweke ratiba ya kujisomea ya ziada,shule zote za Msingi na Sekondari ziwe na miundombinu wezeshi kama Umeme,Maji na barabara. Mkuu wa wilaya aliendelea kusisitiza kuwa vipaumbele katika sekta ya Elimu ni madarasa,meza na viti,matundu ya vyoo,maabara,Ofisi za walimu,mabweni,nyumba za walimu na mabwalo.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango chafanya kikao kujadili mapato na matumizi kwa mwezi Aprili 2025.

    May 31, 2025
  • Maafisa Habari watakiwa kuitangaza miradi ya serikali

    May 30, 2025
  • Halmashauri ya Chalinze yatembelewa na wawekezaji wa nyumba

    May 29, 2025
  • Kampeni ya "Ni rahisi sana"yatoa Elimu kuhushu usalama Mtandaoni Chalinze

    May 28, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.