• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Msoga Half Marathon Mkombozi wa afya za akinamama na watoto wanaozaliwa kabla ya wakati.

Imewekwa: June 29th, 2024


Mashindano ya mbio za Msoga Half Marathon yaliyoandaliwa na Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete(Mb) na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais ,Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora, yaliandaliwa kwa ajili ya kusaidia upatikanaji wa vifaa tiba mbalimbali katika Hospitali ya wilaya Msoga inayohudumia wakazi wote wa halmashauri ya Chalinze na wananchi wengine wa nje ya halmashauri ya Chalinze.


Mbio hizo zimefanyika leo katika kijiji cha Msoga na kuwa na washiriki mbalimbali kutoka maeneo mbalimbali hapa nchini,kama Dar es salaam,Mwanza,Arusha,Kilimanjaro,Pwani na Njombe. Pamoja na washiriki hao viongozi mbalimbali wa kisiasa na dini wameshiriki katika shughuli hiyo ili kuunga mkono juhudi za upatikanaji wa vifaa tiba kwa ajili ya akina mama na watoto wanaozaliwa kabla ya wakati.


Viongozi waliofika katika shughuli hiyo ya mbio za Msoga Half Marathon ni Mheshimiwa Profesa Adolf Mkenda(Mb) ambaye pia ni Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia,Askofu Josephat Gwajima(Mb) na Kiongozi wa kanisa la Ufufuo na Uzima, Askofu Mwampossa na Mheshimiwa Rais Mstaafu wa Awamu ya nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ambaye alikuwa mwenyeji wao katika shughuli hiyo.


Shughuli hiyo ilipambwa na burudani mbalimbali zilizochagizwa na wasanii mbalimbali hapa nchini ili kutatua kero inayowakabili akina mama na watoto wanaozaliwa kabla ya wakati.


Mgeni Rasmi katika hafla hiyo Dkt Jakaya Kikwete alitoa shukrani za dhati kwa washiriki wote wa mashindano hayo  na kuwapongeza wanariadha kwa kuweza kukimbia kilomita za kutosha katika mashindano hayo,ambayo yalikuwa na umbali wa kilomita 21,kilomita 10 na kilomita 05.


Aidha Kikwete aliwashukuru wafadhili wote walioshiriki katika kuwezesha mashindano hayo na kwa kuonyesha upendo wa hali ya juu kwa akinamama na watoto wanaozaliwa kabla ya wakati. Sanjari na shukrani hizo Mgeni rasmi alitoa zawadi kwa washindi wa mashindano hayo na kutoa vyeti vya shukrani kwa wahisani wote waliowezesha shughuli hiyo.


Kwa upande wake Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete alitoa shukrani kwa wachangiaji wote waliojitoa kwa hali na mali katika kufanikisha jambo hili muhimu la kuokoa uhai wa akinamama na watoto wanaozaliwa kabla ya wakati. Sanjari na shukrani hizo kipekee aliwashukuru wabunge wenzake na viongozi wa dini kwa kuona umuhimu wa jambo hili na kuacha shughuli zao na kuja kuungana naye ili kuokoa maisha ya wanachalinze na watanzania kwa ujumla.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • TANGAZO LA KAZI June 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Waziri Kikwete Apokea Hundi ya Tsh Milioni 52 kutoka kiwanda cha Keda

    June 21, 2025
  • Chalinze yapongezwa kwa Hati Safi Mfululizo miaka mitano

    June 18, 2025
  • Mwenyekiti wa UWT akagua miradi ya maendeleo Chalinze

    June 13, 2025
  • Madiwani wa Pangani waipongeza Chalinze kwa Miradi ya mapato ya ndani

    June 11, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.