• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

MWENGE WA UHURU WAMURIKA NA KUANGANZA HALMASHAURI YA CHALINZE

Imewekwa: June 9th, 2017

Mwenge wa Uhuru 2017 Halmashauri ya Chalinze umepita katika vijiji 7 vyenye jumla ya miradi 9 ambapo, Mradi 1 umewekewa jiwe la msingi, miradi 05 Imezinduliwa na miradi 03 imekaguliwa, miradi ipo katika sekta za Afya, Elimu, Maji, Kilimo, Maendeleo ya Jamii, Mashirika yasiyo ya Kiserikali, Watu binafsi. Thamani ya miradi hiyo ni Jumla ya Tshs. 110,466,950,250.00 kwa mchanganuo ufuatao

  • Watu binafsi Tshs 110,004,455,000.00
  • Wananchi wamechangia Tshs 65,000,000.00,
  • Halmashauri Tshs 91,500,000.00 na
  • Wahisani Tshs 305, 950,,250.00

Aidha, katika maeneo ambayo Mwenge umepita ulikuwa umebeba ujumbe usemao “SHIRIKI KUKUZA UCHUMI WA VIWANDA KWA MAENDELEO YA NCHI YETU” Kauli mbiu hii imeambatana na Mapambano dhidi ya Rushwa, Mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI, Mapambano dhidi ya Matumizi ya Dawa za Kulevya na Mapambano dhidi ya Malaria.

Akizungumza katika Eneo la makabidhiano ya Mwenge(Kiwangwa) Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mh. Alhaj Magid Mwanga alisema Hali ya uwekezaji katika Halmashauri ya Chalinze umeanza kwa kasi kutokana na uwepo wa mazingira mazuri na vivutio vingi vya uwekezaji ikiwa ni pamoja na miundombinu ya barabara, maji, umeme, mawasiliano ya simu, ardhi yenye rutuba, mito, bahari na fukwe.

Hali halisi ya sasa ni uwepo wa ujenzi unaoendelea wa Viwanda vikubwa Vitatu ambavyo ni

  • Kiwanda cha Vigae (tiles) Twyford Industry ambacho kipo katika kitongoji cha Pingo kata ya Pera.
  • Ujenzi wa Kiwanda cha Matunda cha Sayona Industry unaendelea na kipo katika kijiji cha mboga kata ya Msoga.
  • Ujenzi wa Kiwanda cha Sementi (Lake Cement) unaoendelea kipo katika kijiji cha Talawanda kata ya Talawanda.

Pia Halmashauri ya Chalinze ina Viwanda ambavyo viko katika hatua za awali za upimaji na upatikanaji wa vibali. Viwanda hivyo ni:-

  • Kiwanda cha sementi (Mamba cement) kilichoko Talawanda.
  • Kiwanda cha Betri kilichopo katika kijiji cha Msoga.
  • Kiwanda cha Magazeti kinachojulikana kwa jina la Jamhuri Media kilichopo katika kijiji cha Msolwa.

Halmashauri ya Chalinze kwa kushirikiana na Viongozi wa dini na Asasi za Kiraia pamoja na Wadau wengine wanaopinga matumizi ya dawa za kulevya wameweza kuwatambua wanaotumia dawa za kulevya ambao ndio nguvu kazi ya Taifa na hivyo kurahisisha mapambano dhidi ya dawa za kulevya.

Aidha katika kukabiliana na janga hili Halmashauri ya Chalinze imefanya yafuatayo:-

  • Imetoa jumla ya Tshs. 100,000,000/= mikopo yenye masharti nafuu kwa Vikundi vya Vijana 42 ili waweze kushiriki ipasavyo kwenye shughuli za uzalishaji mali na kujiongezea kipato.
  • Imefanya utambuzi wa vijana 20 wanaotumia dawa za kulevya katika kata za Bwilingu na Kiwangwa na zoezi ni endelevu.
  • Imetenga 150,000,000/= kwa ajili ya kuwakopesha vijana kwa bajeti ya mwaka 2017/2018.
  • Halmashauri kwa kushirikiana na Asasi ya Filbert Bayi Foundation chini ya KP Programme,  imefanikiwa kutoa elimu ya kutambua madhara ya kutumia dawa ya kulevya katika kata za  Bwilingu, Pera, Mbwewe, Msata na Kiwangwa.  

Ni ukweli usiopingika kuwa Rushwa ni kikwazo kikubwa cha maendeleo katika jamii yoyote yenye ari na mtazamo wa kuleta mabadiliko ya Kiuchumi.

TAKUKURU katika Halmashauri ya Chalinze imeendelea na juhudi za mapambano dhidi ya Rushwa ili kuunga mkono juhudi za Serikali za kuwaletea Wananchi Maendeleo endelevu katika nyanja mbalimbali.

Aidha katika kipindi cha Julai hadi Aprili 2017 TAKUKURU kwa kuhakikisha kuwa inapunguza kero za vitendo vya Rushwa kwa ustawi na maendeleo endelevu kwa Wananchi yafuatayo yalifanyika:-

  • Kuendesha semina 25 (Wavulana 289, Wasichana 164),
  • Mikutano ya hadhara 23 (Wanaume 1431, Wanawake 679), 
  • Kuanzisha na kuimarisha Vilabu 23 vya wapinga Rushwa katika Shule za Msingi na Sekondari (Wavulana 1184, Wasichana 1381) na Maonyesho 2 yamefanyika. 
  • TAKUKURU pia imegawa machapisho zaidi ya 105 yenye jumbe mbalimbali zenye kukemea Vitendo vya Rushwa katika Jamii na pia makala 1 imetolewa inayohusu mmomonyoko wa maadili ni chanzo cha kukithili kwa Rushwa Nchini Tanzania

Kwa matukio katika picha bofya hapa



Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango chafanya kikao kujadili mapato na matumizi kwa mwezi Aprili 2025.

    May 31, 2025
  • Maafisa Habari watakiwa kuitangaza miradi ya serikali

    May 30, 2025
  • Halmashauri ya Chalinze yatembelewa na wawekezaji wa nyumba

    May 29, 2025
  • Kampeni ya "Ni rahisi sana"yatoa Elimu kuhushu usalama Mtandaoni Chalinze

    May 28, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.