• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Naibu Waziri wa Madini auelimisha Umma Chalinze

Imewekwa: May 8th, 2018

Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mheshimiwa Dotto Mashaka Biteko ametembelea katika halmashauri ya wilaya ya Chalinze  na kukutana na wawekezaji wa machimbo ya kokoto na wananchi wa vijiji vya Lugoba,Msata,Kihangaiko,Kinzagu na Saleni  katika ukumbi wa shule ya sekondari ya Lugoba hivi karibuni na kufanya mkutano wa hadhara uliolenga kutatua changamoto za wananchi wa maeneo hayo.Katika ziara hiyo Mheshimiwa Biteko aliambatana na Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete,ambaye alieleza kero za wananchi wa Jimbo lake kuhusiana na wawekezaji wa madini ya kokoto yanayopatikana katika jimbo hilo.Mhe.Ridhiwani alilaani kitendo cha baadhi ya wawekezaji kutotekeleza makubaliano waliyoingia kati yao na vijiji katika suala la uchangiaji wa miradi ya maendeleo.

Aidha Mhe Kikwete alieleza kuhusu suala zima la mgongano wa kisheria kati ya sheria ya madini na sheria ya ardhi ya kijiji sheria hizi zina leta mgongano kwa wananchi pindi wanapompatia mwekezaji ardhi baadaye anakuja mwekezaji mwingine akidai naye kapewa ardhi kutoka juu kwa maana ya kamishina wa ardhi au madini,hivyo aliomba ufafanuzi wa suala hilo ili kuondoa kero kwa wananchi.

Naye Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo,Mheshimiwa Majid Mwanga aliwataka wawekezaji katika halmashauri ya Chalinze kuheshimu sheria za nchi na kuzingatia sheria za ardhi na Madini sanjari na kuwa na mahusiano kati ya wananchi,serikali na wadau wengine wanaofanya nao kazi ili amani ya nchi ikachukue nafasi yake.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Madini,Mheshimiwa Dotto Biteko alianza hotuba yake kwa kusema “Serikali ya awamu ya tano imeamua kuyafanya madini kuwa mali ya watanzania na siyo wawekezaji kwa mujibu wa sheria ya madini iliyofanyiwa  marekebisho hivi karibuni”.Biteko alisema.Naibu waziri alifafanua kwa kusema Mheshimiwa Rais wa awamu ya tano wakati akianzisha wizara hii alituagiza akisema nendeni mkawasaidie watanzania ili wakawe wanufaika wa kwanza wa madini na siyo wageni,ndiyo maana serikali iliamua kufanya mabadiliko ya sheria kwa makusudi ili watanzania wanufaike na mali waliyonayo,wawekezaji walitumia udhaifu wa sheria iliyokuwepo ili kuwakandamiza watanzania pamoja na wingi wa madini tuliyonayo lakini bado watoto wa kitanzania wanakaa chini wawapo shuleni hii haikubaliki hata kidogo.

Aliendelea kwa kusema tumebadilisha sheria ili iwanufaishe wazawa na kuwawezesha wachimbaji wadogo kuwa wachimbaji wa kati na wachimbaji wa kati kuwa wachimbaji wakubwa,sheria itaongeza pato la taifa kwani kabla ya sheria hii pato la taifa kutokana na madini lilikuwa halizidi asilimia 5 pamoja na wingi wa madini tuliyonayo.

Biteko aliendelea kwa kuuelimisha umma kuhusu sheria ya madini na sheria za ardhi kwa maana ya sheria ya ardhi namba 4 na sheria ya ardhi ya vijiji namba 5,alisema wizara ya madini inatowa leseni kwa wawekezaji kwa maana ya kuchimba madini yaliyoko chini ya ardhi kwa mujibu wa sheria ya madini baada ya mwekezaji kuwa amepata leseni anatakiwa afanye taratibu za kupata ardhi kutoka kwa mtu binafsi ama serikali ya kijiji kwa ardhi inayomilikiwa na kijiji,ama kwa kamishina wa ardhi kwa ardhi iliyo ya jumla na wizara haihusiki na kumtafutia mwekezaji ardhi ya juu kwani siyo jukumu la wizara kisheria.Upatikanaji wa ardhi ya kuchimba ni kwa mujibu wa sheria za ardhi sura ya 113 na 114.

Kwa mwekezaji anapotaka kutwaa ardhi ya mtu binafsi kwa ajili ya uchimbaji ni lazima kufanya mambo matatu muhimu kisheria,kwanza ni “Resettlement”pili ni “Reallocation”na tatu ni “Compasation”masuala haya matatu yakitekelezwa kwa umakini hakuna mgogoro utakaojitokeza na uchimbaji utafanyika kwa amani,Biteko alfafanua.

Naibu Waziri alimalizia hotuba yake kwa kutoa onyo kwa wawekezaji wanaouziana leseni za kuchimba kinyemela au juu kwa juu pasipo kupata kibali cha wizara ni kosa kisheria na mwekezaji akibainika kufanya hivyo atachukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kufutiwa leseni,kuuza leseni ni suala ambalo linatakiwa muuzaji apate kibali cha kuuza na mkataba lazima uangaliwe na wizara ya madini na ikikubalika muuzaji sharti alipe kodi ya serikali kwa mauzo yatakayofanyika kwa mujibu wa sheria ya madini na sheria zingine za mikataba.

                               Wananchi wa halmashauri ya wilaya ya Chalinze wakiwa katika Mkutano wa Naibu Waziri wa Madini Mhe Dotto Biteko,katika ukumbi wa shule ya sekondari ya Lugoba    

                                           Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo,Mhe.Majid Mwanga akitoa neno la ukaribisho kwa Naibu Waziri wa Madini,Mhe.Dotto Biteko

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango chafanya kikao kujadili mapato na matumizi kwa mwezi Aprili 2025.

    May 31, 2025
  • Maafisa Habari watakiwa kuitangaza miradi ya serikali

    May 30, 2025
  • Halmashauri ya Chalinze yatembelewa na wawekezaji wa nyumba

    May 29, 2025
  • Kampeni ya "Ni rahisi sana"yatoa Elimu kuhushu usalama Mtandaoni Chalinze

    May 28, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.