• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Pongezi zatolewa kwa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze na watendaji wake

Imewekwa: August 30th, 2019

Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Bi. Zainabu Mfaume Kawawa ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze kwa  ukusanyaji wa mapato kwa mwaka wa fedha 2018/2019 ikilinganishwa na ule wa mwaka wa fedha wa 2017/2018 na kusaidia kufikia lengo la ukusanyaji  wa mapato kwa zaidi ya asilimia mia moja, kwani katika mwaka wa fedha wa 2017/2018 Halmashauri ilikusanya kiasi cha Tsh Bilioni 4.3 sawa na asilimia 91 na Tsh. Bilioni 7.6 kwa mwaka wa fedha wa 2018/2019 sawa na asilimia 132.


Mh. Mkuu wa Wilaya aliyasema hayo kwenye kikao cha baraza la madiwani  ROBO YA NNE  ya mwaka wa fedha 2018/2019 kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze siku ya Alhamisi Tarehe 29/08/2019.

‘’Naipongeza sana Halmashauri yetu ya Chalinze kwa kufanikiwa ukusanyaji wa mapato na kuifanya Halmashauri ya Chalinze kuwa kinara  kitaifa kati ya Halmashauri zote Nchini na kufikia lengo, hii ni kutokana na jitihada na ushirikiano ulioonyeshwa na Mkurugenzi wa Halmashauri, Madiwani, Wajumbe, Watendaji na Wananchi kwa ujumla.’’

Vilevile  Mh. Mkuu wa Wilaya ameiagiza kamati ya Elimu kupitia kwa afisa elimu kusimamia usajili wa shule zote zinazotoa huduma ya elimu haliyakuwa hazikusajiliwa

 Bi.Zainabu Kawawa hakuliacha suala la utoro na mimba mashuleni hii ni kutokana na kuwapo kwa wimbi kubwa la mimba na utoro mashuleni hasa katika shule za sekondari za kata kwa kutolea mfano shule ya sekondari ya Msata alipoenda kuitembelea shule hiyo na kupata orodha ya wanafunzi wenye ujauzito takribani  wanafunzi 8 kuanzia mwezi  Januari mpaka Agosti 2019 na kuagiza madiwani kuhakikisha mimba mashuleni zinatoweka kabisa.

‘’Ndugu Madiwani kutokana na hili mnatakiwa kuhahakisha mnazitembelea shule zenu za kata kwa kutenga siku kadhaa na kwenda kuongea na wanafunzi katika shule hizo kwani ninyi ndio walezi na hili suala si la mkuu wa wilaya peke yake kwani hili suala ni la wote na Taifa kwa ujumla ili kufanikisha maendeleo nchini.’’


Kwa upande wa ulinzi na usalama mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ameiagiza kamati ya ulinzi na usalama kufuatilia kesi zote zilizotokea na kuhakikisha usalama kwa raia wake.

‘’Naiagiza kamati ya ulinzi na usalama kufuatilia kesi zote za mauaji na  matukio ya uovu ili kuhakikisha usalama na kuondoa hofu kwa wananchi ili waweze kufanya shughuli zao za maendeleo kwa amani.’’Alisema Bi Zainabu

 Pia suala la migogoro ya wafugaji wavamizi ambao wamekuwa na tabia ya kuvamia maeneo na hili ni kutokana na wenyeviti wa vitongoji kuwakaribisha wageni kwa kuwapa ardhi na kuwaomba kuacha mara moja tabia hiyo na pia alitoa agizo kwa wafugaji wavamizi hao waondoke maramoja kwani wasipifanya hivyo watachukuliwa hatua stahiki.


Na mheshimiwa mkuu wa wilaya alimalizia kwa kuishukuru kamati nzima ya maendeleo, mkurugenzi  na wajumbe wote kwa ushirikiano waliounesha katika kufanikisha mbio za Mwenge wa uhuru na kutoa neno kwa viongozi kutojihusisha na kupanga viongozi kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika mwezi Novemba mwaka huu kwani jukumu kubwa na la  muhimu kwa watendaji na viongozi wote ni kuhakikisha uhamasishaji wa wananchi kushiriki kikamilifu katika uchaguzi kwa kutoa taarifa mara kwa mara kuhusu uchaguzi huo.    


Kabla ya kufunga Baraza hilo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze Bw.Saidi Zikatimu ameiagiza kamati ya elimu kwa kusema,

‘’Naiagiza kamati ya elimu katika kikao kijacho ituletee idadi kamili za shule zote za binafsi na za serikali ambazo bado hazijasajiliwa ili kujua na kuzifanyia utaratibu wa usajili ili kutengeneza elimu iliyo bora wilayani kwetu na taifa kwa ujumla.’’ Alisema

Vikao hivyo vya baraza hukaliwa kila baada ya robo ya mwaka wa fedha katika Halmashauri kwa lengo la kujadili maendeleo yaliofanywa na serikali na kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili Halmashauri kwa maendeleo zaidi.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango chafanya kikao kujadili mapato na matumizi kwa mwezi Aprili 2025.

    May 31, 2025
  • Maafisa Habari watakiwa kuitangaza miradi ya serikali

    May 30, 2025
  • Halmashauri ya Chalinze yatembelewa na wawekezaji wa nyumba

    May 29, 2025
  • Kampeni ya "Ni rahisi sana"yatoa Elimu kuhushu usalama Mtandaoni Chalinze

    May 28, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.