• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Possi: Hakikisheni mnatokomeza sifuri kwa kusimamia ufundishaji Chalinze

Imewekwa: February 4th, 2026


 

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze, Bwana Ramadhani Possi, amekutana na Wakuu wa Shule za Sekondari kwa ajili ya kufanya tathmini ya matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne na Kidato cha Pili kwa mwaka 2025, pamoja na kujadili changamoto zinazoikabili sekta ya elimu ya sekondari katika halmashauri hiyo.

 

Kikao kazi hicho kilihusisha Wakuu wa Shule za Sekondari 39, zikiwemo shule za Serikali na binafsi, na kililenga kubaini hali ya ufaulu, changamoto zilizopo na kuweka mikakati ya kuboresha zaidi matokeo ya wanafunzi.

 

Akitoa taarifa ya matokeo ya mitihani, Afisa Elimu Sekondari wa Halmashauri ya Chalinze, Mwalimu Godwin Mukaruka, alisema kuwa wastani wa ufaulu wa Mtihani wa Kidato cha Nne kwa mwaka 2025 ni asilimia 89, huku Mtihani wa Kidato cha Pili ukiwa na wastani wa ufaulu wa asilimia 83.3.

 

Katika kikao hicho, Mkurugenzi Possi aliwapongeza walimu na Wakuu wa Shule kwa juhudi kubwa wanazoendelea kuziweka katika ufundishaji na usimamizi wa taaluma, hali iliyochangia kupatikana kwa matokeo hayo chanya. Alisisitiza kuwa mafanikio hayo ni matokeo ya ushirikiano mzuri kati ya walimu, uongozi wa shule na halmashauri kwa ujumla.

 

Hata hivyo, Mkurugenzi aliwataka Wakuu wa Shule kuongeza jitihada katika kufuatilia kwa karibu ufundishaji wa walimu, kusimamia nidhamu ya kitaaluma na kuweka mikakati madhubuti ya kuondoa kabisa ufaulu wa sifuri katika halmashauri ya Chalinze.

 

Kwa upande wao, Wakuu wa Shule walipokea maelekezo hayo na kuahidi kuyafanyia kazi kwa vitendo, kwa kushughulikia mapungufu yote yaliyobainishwa katika ufundishaji na ujifunzaji, kwa lengo la kutokomeza sifuri na kufikia ufaulu wa asilimia 100 katika mitihani ijayo.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • TANGAZO LA KAZI June 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Possi: Hakikisheni mnatokomeza sifuri kwa kusimamia ufundishaji Chalinze

    February 04, 2026
  • Kamati ya Mikopo ya Halmashauri yaketi kujadili maombi ya mikopo ya makundi maalum

    January 30, 2026
  • TRA yatambulisha Mfumo wa Kielektroniki wa Usimamizi wa Kodi (IDRAS)

    January 29, 2026
  • TRA yatambulisha Mfumo wa Kielektroniki wa Usimamizi wa Kodi (IDRAS)

    January 29, 2026
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.