• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Profesa Shemdoe akagua Miradi ya Maendeleo Chalinze

Imewekwa: November 16th, 2022

                                                     Na John Mlyambate 

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,Profesa Riziki Shemdoe leo ameweza kukagua miradi mbalimbali ya Maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze Mkoani Pwani inayotekelezwa na Serikali ya awamu ya sita chini Rais Samia Suluhu Hassan.


Miradi iliyokaguliwa na Katibu Mkuu ni miradi ya Elimu inayotekelezwa kote nchini,miradi hiyo ni Ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa ajili ya wanafunzi watakaoanza masomo ya kidato cha kwanza Januari 2023,Profesa Shemdoe alikagua ujenzi wa madarasa katika shule ya Sekondari Chahua,na shule ya Sekondari Lugoba na kuridhishwa na hatua mbalimbali za utekelezaji wa mradi huo na kuwapongeza wasimamizi wote wa mradi kuanzia Menejimenti ya Halmashauri,Madiwani na walimu kwa usimamizi mzuri uliopelekea madarasa hayo kujengwa kwa kiwango stahiki.

“Nikupongeze Mkurugenzi na timu yako kwa usimamizi makini,Madiwani na Uongozi wa Shule kwa maana ya wakuu Shule wote wanaoendelea na utekelezaji wa miradi hii,nawaomba muongeze bidii mara ifikapo tarehe 15 Desemba madarasa yawe yamekamilika.” Profesa Shemdoe aliagiza.


Katibu Mkuu ,Profesa Shemdoe aliweza pia kukagua Ujenzi wa soko la Bwilingu na kuona ubora wake pia alikagua hatua za awali za ujenzi wa vibanda vya wajasiriamali vinavyoendelea kujengwa kuzunguka soko, jumla ya vibanda hivyo ni 150 na vinajengwa kutokana fedha za mapato ya ndani ya Halmashauri ili kuweza kuwakwamua wananchi kutokana na Umasikini uliokithiri.

“Mara ukikakamilika ujenzi wa vibanda hivi wapewe wananchi sisi Watumishi tusijiingize katika umiliki wa vibanda hivi wapatiwe walengwa waliokusudiwa.” Katibu Mkuu alitoa rai yake.


Mara baada ya Ukaguzi wa soko, Katibu Mkuu alienda katika hospitali ya Wilaya ya Msoga na kukagua Ujenzi wa Kituo cha Matibabu ya Dharura(EMD) kinachoendelea kujengwa katika hospitali hiyo,Profesa Shemdoe alifurahishwa na utekelezaji wa mradi huo na kumshukuru Rais Mstaafu wa awamu Nne,Dkt Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuwezesha upatikanaji wa mradi huo unaotekelezwa kwa faida ya watanzania wanapopatwa na ajali na kuwa na uhakika wa matibabu wakati wowote.


Aidha Profesa Shemdoe alikagua na kujionea Vifaa tiba mbalimbali katika hospitali ya Msoga vilivyonunuliwa kutokana na fedha za Mapato ya ndani ya Halmashauri na fedha kutoka Serikali kuu,vifaa hivyo ni vifaa vya Mionzi (X-ray)na vipimo vya moyo vinavyopima Umeme wa moyo kwa binadamu. Katibu Mkuu alipongeza uongozi wa Halmashauri kwa maana ya Madiwani na Menejimenti ya Halmashauri kwa hatua kubwa za kimaendeleo zinazofanywa na uongozi.

“Nafurahia kuwa sehemu ya mafanikio katika Halmashauri ya Chalinze na sijutii kufanya ziara hii hakika mmenifurahisha kwa matendo makubwa mnayoyafanya ya kuwahakikishia afya bora wanachalinze na watanzania kwa ujumla.” Shemdoe alisema.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • PPRA yatoa Mafunzo ya NeST kwa Watendaji wa Kata na Wakuu wa Shule Chalinze

    May 08, 2025
  • Watendaji wa Kata na Vijiji wapewa Mafunzo ya namna ya kukusanya Kodi ya Majengo Chalinze

    May 07, 2025
  • PPRA yatoa mafunzo ya Ununuzi kwa watumishi wa Afya Chalinze

    May 07, 2025
  • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango yafanya ziara kukagua miradi ya maendeleo

    May 06, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.