• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

RAIS AWEKA JIWE LA MSINGI KATIKA KIWANDA CHA SAYONA KILICHOPO CHALINZE

Imewekwa: June 22nd, 2017

Rais John Pombe Magufuli afanya ziara Katika halmashauri ya chalinze na Kuweka jiwe la msingi katika kiwanda cha kusindika matunda na utengenezaji wa Juisi Sayona kilichopoa Maeneo ya Mboga Halmashauri ya Chalinze.

Wakizungumza kwa wakati tofauti tofauti Mwakilishi wa Kampuni ya Sayona Mr. Abuu alisema kiwanda hiki kinatarajia kuajiri wafanyakazi 828 sambamba na ajira za muda kulingana na msimu wa uzalishaji. Pia mradi huu unatarajia kuwanufaisha wakulima wapatao 30,000 kutoka katika maeneo ya Wilaya ya Bagamoyo na maeneo mengine yanayolima matunda.


Katika kuhakikisha mradi huu unatekelezwa kwa kufuata sheria na taratibu kiwanda kitafunga mtambo maalumu (ETP Plant) wa kusafisha maji yanayotoka katika uzalishaji na maeneo mengine ili yaweze kutumika kwa matumizi mengine.

Aidha, katika kuhakikisha usalama Kampuni tayari imenunua gari maalum la kuzuia na kupambana na moto ambalo licha ya kuhudumia kiwanda litatoa pia huduma kwa wananchi wa Chalinze pale janga la moto linapotokea

Mradi huu unakabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa maji kwani mradi unategemea maji ya mto Wami. Hata hivyo maji yamekua hayapatikani kwa kipindi kirefu hali inayosababisha wakati huu wa ujenzi kufuata maji katika mto Wami kwa kutumia magari. Hali hii imeifanya kampuni kuomba kuingia ubia na Mamlaka ya Maji Wami ili kuboresha huduma ya maji itakayowezesha wananchi wote kutumia mradi huu kupata maji.

Aidha, Kampuni tayari imenunua vifaa vyenye thamani ya Tshs. 100,000,000/= na kinachosubiriwa ni Mamlaka ya Maji kupitia na kuingia mkataba ili vifaa vifungwe na huduma ya maji ipatikane kwa wananchi wote.

Aidha Mh. Ridhiwani Kikwete (Mbunge Jimbo la Chalinze) akitoa taarifa kwa mgeni rasmi alisema Wakati wa uchaguzi Halmashauri ya chalinze ilikua haina kiwanda hata kimoja bali kwa sasa ina viwanda Saba (7) vilivyo anza kujengwa, Pia yapo mafanikio mengi yamekwisha fikiwa ikiwa ni pamoja na Kutoa 10% ya pato la ndani kwa ajili ya vijana na wanawake ambapo jumla ya Tsh.200,000,000/= imekwisha tumika, ujenzi wa wa hospitari ya wilaya ambapo jumla ya Tsh. 80,000,000/= kwa ajili ya kukamilisha ‘’Theater’’

Katika ziara hiyo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh: John Pombe Magufuli amewapongeza wanannchi wa Chalinze kwa mapokezi mazuri walimpatia na kuwashukuru kwa Kukiamini chama chake kuongoza taifa hili kwa awamu nyingine.

Aidha amewaomba wana nchi wenye uwezo waje kuwekeza halmashauri ya chalinze kutokana na kuwa na mazingira rafiki ya uwekezaji. Pia amewataka wananchi kufanya kazi kwa bidii ili kuhakikisha kuwa Malighafi inayo takiwa na kiwanda inapatikana kwa wakati ili kukipa uwezo kiwanda kuzalisha sawasawa na lengo kilicho jiwekea. Kuhusiana na changamoto ya maji kwanza alimshukuru mwekezaji kwa hatua alichukua ya kugharamia vifaa hitajika kwa ajili ya kulejesha hali nzuri ya upatikanaji wa maji na kumtaka Mkurugenzi wa CHALIWASO kuhakikisha wanaharakisha mazungumzo baina yao na mwekezaji ili upatikanaji wa maji uwe wa uhakikika.

Katika ziara hiyo Mh Rais alitoa maagizo mbalimbali ikiwemo

  • Wale wote waliopewa viwanda na kushidwa kuviendeleza wanyang’anywe na wapewe wale wenye uwezo
  • Wataala kushughurikia migogoro yote ya ardhi na kuwaonya Viongozi wote watakao tetea wanaorisha mashamba ya wakulima  aidha amewaagiza pia wenye mashamba kuhakikisha mashamba yao yanakua katika hali ya usafi ili yasiwe kivutio cha mifugo kuingia na kula mimea yao iliojifisha kwenye majani.
  •  Amewaagiza wakala wa barabara kuikabidhi Halmashauri ya Chalinze majengo yote waliokuwa wakitumia wakati wa ujenzi wa barabara ya Bagamoyo – Msata na halmashauri itaamua matumizi sahihi ya majengo hayo.

Mwisho aliwapongeza watumishi wote kwa kazi nzuri wanayo ifanya na kuwataka waendelee kuchapa kazi na kuwatumikia wananchi hasa walio wanyonge.

Habari na Emmanuel S. Muhizi (AFISA TEHAMA CHALINZE DC)



Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango chafanya kikao kujadili mapato na matumizi kwa mwezi Aprili 2025.

    May 31, 2025
  • Maafisa Habari watakiwa kuitangaza miradi ya serikali

    May 30, 2025
  • Halmashauri ya Chalinze yatembelewa na wawekezaji wa nyumba

    May 29, 2025
  • Kampeni ya "Ni rahisi sana"yatoa Elimu kuhushu usalama Mtandaoni Chalinze

    May 28, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.