• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Rais Mstaafu awamu ya nne akutana na Baraza la Madiwani Chalinze

Imewekwa: November 7th, 2022

RAIS MSTAAFU AWAMU YA NNE AKUTANA MADIWANI CHALINZE

Rais Mstaafu wa awamu ya nne,Mheshimiwa Dkt Jakaya Mrisho Kikwete amefanya mkutano na madiwani na watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Chalinze leo katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete katika halmashauri ya hiyo.


Mheshimiwa Kikwete amewataka madiwani kufanya kazi kwa bidii kuhakikisha halmashauri inasonga mbele kwa kuisimamia kwa weledi wa hali ya juu katika kuiletea maendeleo halmashauri na wananchi wa chalinze kwa ujumla kunufaika.

“Hatima ya Maendeleo ya halmashauri ya Chalinze iko mikononi mwenu,mambo yakiharibika hamuwezi kukwepa kama ilivyo kwa serikari kuu mambo yakiharibika wabunge hawawezi kukwepa.” Kikwete alisema.

Aliendelea kuwaasa madiwani kuisaidia halmashauri kusonga mbele kwa kutoa mawazo ya kujenga kuhakikisha eneo la Chalinze linakuwa na huduma za jamii kama maji,barabara,elimu bora na umeme. Sanjari na nasaha hizo Mheshimiwa Kikwete aliwataka madiwani kuwa na shughuli za kuwaingizia kipato pasipo kutegemea halmashauri. 


Vivyo hivyo alizungumza kuhusu utendaji wa wakuu wa Idara na watumishi kwa ujumla na kuwataka kufanya kazi kwa weledi na tija na kuifanya halmashauri ipige hatua kutoka ilipokuwa kwenda sehemu nyingine.

“Wakuu wa Idara mnatakiwa kujipima na kuona umuhimu wa ninyi kuwa katika nafasi mlizonazo kwa kutoa mchango chanya, kupanga mipango inayotekelezeka na kutoa matokeo pia mnatakiwa kujihoji tangu nifike hapa mpaka sasa nimefanya kitu gani chenye matokeo.”Kikwete alisisitiza.


Aidha Dkt Kikwete aliwataka madiwani na wataalam kufanya kazi kwa ushirikiano katika kuwaletea maendeleo wananchi na kuondoa tofauti zao kwa kujadiliana na kufikia muafaka pasipo kuathiri mipango ya maendeleo. Aliendelea kueleza katika kikao hicho kwa kueleza umuhimu wa Chalinze na mwonekano wake kijiografia na kuwahoji watendaji pamoja na madiwani wamejiandaa vipi ili kunufaika na ujenzi wa bandari ya nchi kavu ya Kwala inayoendelea kujengwa.

“Bandari ya nchi kavu inayoendelea kujengwa kule Kwala ni fursa kwa wanachalinze kama ninyi viongozi mmejipanga ili wananchi wenu waweze kunufaika katika uzalishaji na pia upatikanaji wa ajira na hivyo ndivyo vitu mnatakiwa kujadili kama madiwani.” Kikwete alisema.


Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Mheshimiwa Zainab Abdallah Issa alisema Chalinze ni chachu ya uchumi katika nchi kutoka na jiografia yake kwani Chalinze ina vivutio vingi vya kiuchumi ambavyo vikiwekewa mazingira wezeshi wananchi watanufaika kiuchumi na kuondokana na ufukara wa kipato.


Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chalinze Meshimiwa Hassani Mwinyikondo kwa niaba ya madiwani na wananchi wa Chalinze alipokea ushauri na maelekezo kutoka kwa Rais Mstaafu wa Awamu ya nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete.

“Binafsi nakiri kupokea ushauri na maelekezo kutoka kwa Mzee wetu na kuahidi kuyafanyia kazi kwa maslahi ya wanachalinze na watanzania kwa ujumla,kwa kweli leo tumepata semina kutoka kwa Rais Mstaafu na uzoefu mbalimbali katika kuwaongoza na kuwatumikia wananchi asante sana kwa yote.” Mwinyikondo alisema.


Akitoa neno la shukrani,Mheshimiwa Ridhiwani Jakaya Kikwete(Mb) na Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendele ya Makazi kwa nasaha zilizotolewa na Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Dkt Jakaya Kikwete. Mheshimiwa Ridhiwani alimshukuru na kumpongeza Mzee Kikwete kwa yote aliyoyasema na kuahidi kuyafanyia kazi na kujipanga kimkakati kwani Chalinze ni eneo ambalo ni chachu ya uchumi, hivyo tukiweka miundombinu stahiki watu wetu wataondokana na umasikini.

“Mgeni Rasmi katika kikao hiki umetufundisha mengi na yenye tija katika halmashauri yetu, tunaahidi kuwa kitu kimoja katika utekelezaji wa shughuli zetu katika kuwaletea maendeleo wanachalinze na watanzania kwa ujumla, tunaahidi kuzifanyia kazi nasaha zote ulizotupatia, asante sana.” Ridhiwani alisema.

 

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • PPRA yatoa Mafunzo ya NeST kwa Watendaji wa Kata na Wakuu wa Shule Chalinze

    May 08, 2025
  • Watendaji wa Kata na Vijiji wapewa Mafunzo ya namna ya kukusanya Kodi ya Majengo Chalinze

    May 07, 2025
  • PPRA yatoa mafunzo ya Ununuzi kwa watumishi wa Afya Chalinze

    May 07, 2025
  • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango yafanya ziara kukagua miradi ya maendeleo

    May 06, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.