• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

RC Kunenge afanya ziara ya ukaguzi kituo cha kupoza umeme Chalinze

Imewekwa: July 25th, 2022



Mkuu wa Mkoa wa Pwani leo amefanya ziara ya kuutembelea na kukagua ujenzi wa Mradi wa kupoza umeme uliopo Magome Halmashauri ya Chalinze ili kujionea ni kwa namna gani shughuli za ujenzi wa mradi huo unavyoendeshwa.

Akizungumza mara baada ya ukaguzi wa mradi huo Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Abuubakar Kunenge ametoa shukrani za dhati kubwa kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania kwa kuendelea kuhakikisha kuwa yale yote aliyotuahidi Mkoa wa Pwani anayatekeleza kwa vitendo na kwa haraka.

“Leo hii tuko hapa kushuhudia mradi mkubwa wa kituo cha kupoza umeme na kwa dhati nimshukuru Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan kwa kuyatekeleza yale yote aliyosema kwa vitendo kwani Mheshimiwa Rais aliahidi na kuliambia Taifa kuwa Mkoa wa Pwani ambao ni Mkoa wa kimkakati utapata nishati ya maji na umeme kwa matumizi ya wananchi pamoja na matumizi ya kiuchumi ikiwa ni pamoja na viwanda na mradi mkubwa wa Treni za Mwendo kasi (SGR)”. Amesema Mhe. Kunenge.

Hata hivyo Mhe. Kunenge amewaasa vijana waliopata nafasi na ambao watapata nafasi za kufanya kazi katika mradi huo kuepukana na udanganyifu na wizi na badala yake wafanye kazi kwa bidii kwa fursa zinazopatikana katika maeneo yao hasa hili la mradi wa Umeme.

Aidha Meneja wa Mradi huo kutoka TANESCO Mhandisi Newton Livingstone amesema kuwa mradi huo una thamani ya Dolla Mil.42.5 za Kimarekani na mpaka kufikia jana mradi huu umefikia 17% na kwa awamu ya kwanza mradi huu  unaatarajiwa kuzalisha umeme wa  MW1000 na kwa awamu ya pili utazalisha umeme wa MW 2115 kwa ujumla.

Mradi huo wa umeme unamilikiwa na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na upo chini ya Mkandarasi Mkuu wa Kampuni ya TBEA kutoka China pamoja na Mkandarasi mshauri Kampuni ya SHAKER kutoka nchini Misri.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango chafanya kikao kujadili mapato na matumizi kwa mwezi Aprili 2025.

    May 31, 2025
  • Maafisa Habari watakiwa kuitangaza miradi ya serikali

    May 30, 2025
  • Halmashauri ya Chalinze yatembelewa na wawekezaji wa nyumba

    May 29, 2025
  • Kampeni ya "Ni rahisi sana"yatoa Elimu kuhushu usalama Mtandaoni Chalinze

    May 28, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.