• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

RC Kunenge: Hati Safi Kawaida yetu Chalinze

Imewekwa: June 21st, 2023

                 Na John Mlyambate

Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mheshimiwa Abubakar Kunenge ameupongeza uongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Chalinze kwa kupata Hati Safi(Unqualified report). Mkuu wa Mkoa amezitoa pongezi hizo leo katika kikao cha Baraza la Madiwani kilichoketi leo katika Ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete.


Mheshimiwa Kunenge ametoa pongezi hizo baada ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Chalinze, Bwana Ramadhani Possi kuwasilisha taarifa ya Hoja na Majibu ya Mkaguzi wa Nje kwa mwaka wa Fedha 2021/2022. Taarifa hiyo iliwasilishwa kwa mujibu wa Agizo la 31 la Randama ya Fedha katika Mamlaka za serikali za Mitaa ya mwaka 2009.


Akitoa pongezi hizo Mheshimiwa Kunenge ameipongeza Halmashauri ya Chalinze kwa kuzingatia matumizi sahihi ya fedha za serikali kwa kupata Hati safi mfululizo kwa miaka yote tangu ianzishwe halmashauri hiyo mwaka 2016. Ametoa pongezi kwa waheshimiwa Madiwani kwa usimamizi bora wa fedha na mali za halmashauri na kuwapongeza Menejimenti ya Halmashauri kwa kufanya kazi kwa uaminifu na ueledi katika kuwaletea maendeleo wananchi.


“Halmashauri ya Chalinze kupata Hati Safi ni kawaida yetu tusijipime kwa kufunga hoja bali tujipime kwa kutozalisha hoja na mipango yetu iendane na vipaumbele halisi(Reflection of the Planning Priorities).” Mheshimiwa Kunenge alisema.


Mkuu wa Mkoa katika Hotuba yake alisisitiza utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa wakati kwani miradi ni jibu la kero za wananchi na jibu la maendeleo ya wananchi ambao wametoa ridhaa kwa serikali ya Dkt Samia Suluhu Hassan kuwaletea maendeleo wananchi wa Chalinze na watanzania kwa ujumla.


Adha Mheshimiwa Kunenge alitaka Halmashauri ya Chalinze kubuni na kuanzisha vyanzo vipya vya mapato ili kuwa na uhakika wa kukusanya mapato na kufikia malengo ya bajeti,kwani kunapokuwa na vyanzo vingi vya mapato hata kama kutatokea msukosuko katika ukusanyaji mapato halmashauri huweza kufikia malengo yake pasipo shaka.


Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani Bwana Rashid Mchata alitoa pongezi za dhati kwa Halmashauri ya Chalinze kwa kazi nzuri inazoendelea kuzitekeleza,ujenzi bora wa ofisi ya Halmashauri na akapongeza ubora wa samani zilizopo katika jengo la halmashauri kwa kutengenezwa kutokana na mbao ngumu(Hard wood).


Mchata aliendelea kulipongeza Baraza la madiwani na wataalam kwa upande wa ukusanyaji mapato na kusisitiza kukusanya mapato hayo kwa kufuatilia kila chnzo kwa umakini na akataja baadhi ya vyanzo ambavyo havijafikia asilimia takiwa kama mpunga na pamba katika sekta ya kilimo. Hata hivyo Katibu Tawala wa Mkoa alitoa pkngezi kwani mpaka leo halmashauri ya Chalinze ilikuwa imefikia asilimia 99 ya ukusanyaji wa mapato yake kwa mwaka wa fedha 2022/2023 na kuwataka kuongeza bidii ili kukamilisha ndani ya siku chache zilizobakia.


Naye Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo,Mheshimiwa Halima Okash alilipongeza Baraza la Madiwani,Wakuu wa Idara na Vitengo wakiongozwa na Bwana Ramadhani Possi kwa kufanya kazi kama timu katika kuwaletea maendeleo wananchi wa Chalinze na kuwataka kuundeleza utamaduni huo kwa ufanisi zaidi.


Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Chalinze,Mheshimiwa Hassani Mwinyikondo alihitimisha kikao cha Baraza la Madiwani kwa kupokea pongezi zilizotolewa na viongozi mbalimbali wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani na kuahidi kuufanyia kazi ushauri uliotolewa na viongozi hao. Mheshimiwa Mwinyikondo aliahidi kuufanyia kazi ushauri uliotolewa na Mheshimiwa Kunenge wa kutozalisha hoja tena bali kutekeleza miradi ya maendeleo kwa wakati ili kuweza kupunguza kero za wananchi kwani ndiyo majawabu halisi kwa wanchi.


Aidha Mwinyikondo alitoa ombi kwa Mkuu wa Mkoa kutoa fursa kwa kuitafutia Chalinze wawekezaji wa masuala mbalimbali ya kiuchumi kwani Chalinze ina ardhi ya kutosha kwa uwekezaji mbalimbali.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • TANGAZO LA KAZI June 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Waziri Kikwete Apokea Hundi ya Tsh Milioni 52 kutoka kiwanda cha Keda

    June 21, 2025
  • Chalinze yapongezwa kwa Hati Safi Mfululizo miaka mitano

    June 18, 2025
  • Mwenyekiti wa UWT akagua miradi ya maendeleo Chalinze

    June 13, 2025
  • Madiwani wa Pangani waipongeza Chalinze kwa Miradi ya mapato ya ndani

    June 11, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.