• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

RC Ndikilo:Halmashauri Tengeni fedha kwa ajili ya Wanawake

Imewekwa: March 8th, 2018

Mkuu wa Mkoa wa Pwani,Mhandisi Evarist Ndikilo ametoa agizo kwa Halmashauri zote za mkoa wa Pwani kutekeleza kwa vitendo Ilani ya Chama cha Mapinduzi kwa kutoa asilimia tano ya mapato ya ndani kwa ajili ya kuwawezesha wanawake kujikwamua kiuchumi,maagizo hayo ameyatoa leo katika maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani yaliyofanyika kimkoa katika Mji wa Chalinze.

Mheshimiwa Ndikilo katika hotuba yake aliendelea kusisitiza kwamba wakati tukielekea kwenye Tanzania ya viwanda hatuna budi kuendelea kutenga fedha kwa ajili ya kuwawezesha wanawake kupambana na umasikini na kuzalisha kwa tija kwani katika familia wanawake ndiyo wazalishaji wakubwa na walezi wa familia.

Sanjari na kuwawezesha wanawake kiuchumi Mkuu wa Mkoa amekemea ndoa za utotoni,ukatili wa kijinsia kwa wanawake na kupambana na tamaduni zisizofaa zinazoweza kupelekea kukwamisha ndoto za mwanamke katika jamii na kushindwa kufikia malengo yake.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Chalinze,Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete alimhakikishia Mkuu wa Mkoa kwamba kwa Halmashauri ya Chalinze tunatekeleza kwa vitendo Ilani ya Chama cha Mapinduzi na maagizo ya serikali kwa Ujumla kwa kutenga fedha kwa ajili ya wanawake  kwani kwa mwaka wa fedha wa 2016/2017 tulitenga fedha na kuwakopesha wanawake na Vijana kiasi cha milioni 234 na walikopeshwa zaidi ya asilimia 100 na wanawake wanajitahidi kurejesha mikopo hiyo kwa wakati na aliwapongeza wakina mama kwa uaminifu huo na kuwataka jamii iendelee kuwatia moyo akina mama,Aidha kwa mwaka wa fedha 2017/2018 Halmsahauri ya Chalinze imekwisha kopesha wanawake zaidi ya Milioni 120.

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze Mheshimiwa Said Zikatimu alipokea maelekezo ya Mkuu wa Mkoa na kumhakikishia kuwa Halmashauri yake iko mstari wa mbele katika utengaji wa fedha kwa ajili ya Vijana na kuahidi kutoa fedha zingine kwa ajili ya mikopo ya wanawake na Vijana kwa robo ya pili ya mwaka wa fedha wa 2017/2018 ambazo zitakuwa Milioni 140

Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii,Saidi Mwakapugi alitoa ufafanuzi kwa kueleza idadi ya vikundi vilivyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze ni 384 ,vikundi 215 ni vya wanawake na 169 ni vya vijana.Vikundi 59 vya wanawake na vikundi 50 vya vijana vilikopeshwa Jumla ya fedha za kitanzania Milioni 234 kwa kwa mwaka wa fedha 2016/2017 na Jumla ya fedha za kitanzania Milioni 120 zimekopeshwa kwa wanawake na Vijana kwa mwaka huu wa 2017/2018.”Kwa mwaka 2016/2017 Halmashauri ilitoa fedha zote zilizokuwa zimetengwa kwa mujibu wa bajeti na kuzikopesha kwa walengwa au wanawake na vijana”Mwakapugi alisema.

Mkuu wa Idara ya Maendeleo aliendelea kufafanua  kwamba kwa mwaka wa fedha 2017/2018 Halmashauri ya Chalinze imetenga Jumla ya fedha za kitanzania milioni 270 kwa ajili ya wanawake na vijana.


Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • PPRA yatoa Mafunzo ya NeST kwa Watendaji wa Kata na Wakuu wa Shule Chalinze

    May 08, 2025
  • Watendaji wa Kata na Vijiji wapewa Mafunzo ya namna ya kukusanya Kodi ya Majengo Chalinze

    May 07, 2025
  • PPRA yatoa mafunzo ya Ununuzi kwa watumishi wa Afya Chalinze

    May 07, 2025
  • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango yafanya ziara kukagua miradi ya maendeleo

    May 06, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.