• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Ridhiwani Kikwete ataka maboresho yanayofanywa sekta ya Elimu yaendane na matokeo chanya

Imewekwa: February 25th, 2024

NAIBU Waziri Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Ridhiwani Kikwete  amesema maboresho yanayofanyika katika sekta ya elimu ni kuhakikisha elimu bora inapatikana ufaulu unaongezeka na si kuzalisha vijana ambao hawataleta mabadiliko ya maendeleo kwenye maeneo yao.


Pia amesema ujenzi wa Hospitali ya Msoga na maboresho yanayofanyika mara kwa mara ni kwa ajili ya huduma bora kwa wananchi na si kukata miguu ya waendesha bodaboda.


Ridhiwani ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Chalinze aliyasema hayo mwishoni mwa wiki alipokuwa katika shule ya sekondari Mboga, kwenye hafla ya makabidhiano ya vifaa vya mradi wa maabara za kompyuta  kwa shule nne za Sekondari Halmashauri ya Chalinze.


Katika makabidhiano ya kompyuta hizo zilizotolewa na Shirika lisilo la kiserikali la Reneal International Education Outreach, Naibu Waziri huyo alisisitiza wanafunzi kujikita kwenye masomo na kuachana na tamaa ambazo zinarudisha nyuma maendeleo.


"Wapo waliotangulia kuolewa kabla ya muda angalieni maisha yao yalivyo duni, achaneni na makundi ambayo hayana tija kwenu sikubali kuona mnafeli na kwenda kuendesha bodaboda wakati mazingira ya elimu yameboreshwa kwa asilimia kubwa" alisisitiza.


Alisema awali shule za kata zilikuwa nyuma kwenye upande wa tehama lakini sasa maboresho yanaendelea kuhakikisha wanajifunza somo hilo na kwenda na teknolojia ya sasa


Alikemea tabia ya baadhi ya Wazazi kushawishi watoto wao kufeli kwenye mitihani yao ya kitaifa Ili wasiendelee na masomo wakidai kukwepa gharama jambo ambalo si sahihi kwani tayari Serikali imeondoa ada shuleni.


Ridhiwani ameishukuru Shirika hilo kwa kuwezesha kompyuta hizo ambazo zitawasaidia wanafunzi kuondokana na kutafuta vitu vingi maktaba ambavyo watavipata kwa urahisi kwenye kompyuta.


Awali Afisa Elimu Sekondari Salama Ndyetabura aliwaelekeza walimu na wanafunzi kuona namna Bora ya kuvitunza vifaa hivyo Ili viweze kuwa na manufaa kwa vizazi vya sasa na baadae.


Alisema Halmashauri hiyo ambayo inashule za Sekondari 26 nne pekee ndio zimenufaika na msaada huo wenye thamani ya sh. 71.1 Milion ambazo ni Mboga, Msata, Mdaula na Mandera lengo likiwa ni kusaidia ujifunzaji na ufundishaji wa masomo hususani ya sayansi .


Alimshukuru Mbunge huyo kwa kufanikisha upatikanaji wa vifaa hivyo  ambavyo vinakwenda kurahisisha ufanyaji wa masomo ya sayansi kwa vitendo kupitia kompyuta, walimu kuandaa masomo na matokeo kwa wakati na kuibua na kumkuza vioawa vya wawanafunzi katika matumizi na maendeleo ya teknolojia.


Afisa Tehama Wizara ya Habari  Mawasiliano  na Teknolojia ya Habari ambaye pia ni mratibu wa Shirika lililotoa msaada huo alisema Mbunge wa Jimbo hilo aliomba kompyuta kwa shule zote za Sekondari za Jimbo hilo na kwa kuanzia wametoa kompyuta 20.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • PPRA yatoa Mafunzo ya NeST kwa Watendaji wa Kata na Wakuu wa Shule Chalinze

    May 08, 2025
  • Watendaji wa Kata na Vijiji wapewa Mafunzo ya namna ya kukusanya Kodi ya Majengo Chalinze

    May 07, 2025
  • PPRA yatoa mafunzo ya Ununuzi kwa watumishi wa Afya Chalinze

    May 07, 2025
  • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango yafanya ziara kukagua miradi ya maendeleo

    May 06, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.