• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Serikali yatangaza neema kwa wakulima wa zao la pamba Chalinze

Imewekwa: October 30th, 2024


Na John Mlyambate 

*Chalinze, Tanzania* – Serikali kupitia Bodi ya Pamba imetangaza msaada mkubwa kwa wakulima wa pamba katika Halmashauri ya Chalinze, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuimarisha zao hilo katika kanda ya mashariki. Tangazo hilo lilitolewa na Balozi wa Zao la Pamba, Mheshimiwa Aggrey Mwanri, alipokuwa akizungumza na wananchi kupitia kituo cha redio cha Chalinze FM leo.


Mheshimiwa Mwanri amesema kuwa katika msimu mpya wa kilimo unaoanza Novemba 2024, Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan itatoa mbegu, dawa, na mabomba ya kupulizia bure kwa wakulima wa pamba. Mpango huu unalenga kuongeza uzalishaji na kuwasaidia wakulima wa pamba katika maeneo ya Chalinze na kanda ya mashariki kwa ujumla.


Akizungumza zaidi, Mwanri amewataka vijana kuchangamkia fursa hiyo kwa kuzalisha pamba kwa wingi kutokana na upatikanaji wa pembejeo bure na uhakika wa soko. Ameeleza kuwa Bodi ya Pamba tayari imepata wanunuzi wa kuaminika ambao wataleta soko lenye uhakika kwa wakulima wa pamba.


Kwa upande wake, Mwakilishi wa kampuni ya ununuzi wa pamba ya Bens, Bwana Essau Mwalukasa, ambaye kampuni yake inajenga kiwanda cha kuchambua pamba katika Wilaya ya Mvomero, Morogoro, ameahidi kwamba kampuni yake iko tayari kununua pamba yote itakayozalishwa na wakulima wa Chalinze. Amehimiza wakulima waongeze uzalishaji ili kuhakikisha wana soko thabiti.


Aidha, Mkuu wa Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi katika Halmashauri ya Chalinze, Bwana Jovin Bararata, kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri, ameishukuru Serikali kwa juhudi zake za kuweka mazingira rafiki kwa wakulima, ikiwemo upatikanaji wa pembejeo bure na soko la uhakika kwa wakulima wa pamba.


Hatua hii inatarajiwa kuinua uchumi wa wakulima wa pamba na kuchangia maendeleo ya kilimo katika wilaya ya Chalinze na maeneo jirani.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • PPRA yatoa Mafunzo ya NeST kwa Watendaji wa Kata na Wakuu wa Shule Chalinze

    May 08, 2025
  • Watendaji wa Kata na Vijiji wapewa Mafunzo ya namna ya kukusanya Kodi ya Majengo Chalinze

    May 07, 2025
  • PPRA yatoa mafunzo ya Ununuzi kwa watumishi wa Afya Chalinze

    May 07, 2025
  • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango yafanya ziara kukagua miradi ya maendeleo

    May 06, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.