• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Shule Mpya ya Sekondari yajengwa Chalinze

Imewekwa: February 10th, 2020

     Na John Mlyambate 

Halmashauri ya wilaya ya Chalinze katika kukabiliana na uhaba wa vyumba vya madarasa kwa wanafunzi waliofaulu kuanza kidato cha kwanza mwaka 2020 wapatao 270 imeanzisha ujenzi wa shule mpya ya sekondari kwa kuanza kujenga vyumba vitano vya madarasa na vyoo ambavyo vitawawezesha wanafunzi hao kuendelea na masomo.


Shule hiyo inajengwa katika kitongoji cha Chahua kilichoko katika mamlaka ya mji mdogo wa Chalinze,ujenzi huo unajengwa kwa kutumia mapato ya ndani ya halmashauri yenye thamani ya fedha za kitanzania milioni 112. Kiasi hicho cha fedha kitatumika kujenga vyumba vitano vya madarasa,ofisi mbili za walimu na vyoo vya walimu


Kwa mujibu wa Mhandisi wa halmashauri ya Chalinze John Chizima akitoa maelezo ya kwa kamati ya Elimu afya na Maji ilipotembelea katika mradi huo ili kuona maendeleo ya mradi aliihakikishia kamati hiyo kuwa ifikapo Machi 10 mwaka huu 2020 majengo yatakuwa tayari na wanafunzi watakuwa wanasoma.”Kwa hali ilivyo na tuliyonayo tunategemea tukamilishe kazi hii mapema iwezekanavyo na wanafunzi waanze kuyatumia Kwani vifaa vyote vipo.” Chizima alisema.


Naye Afisa Elimu Sekondari,Mwalimu Timothy Bernard aliieleza kamati ya Huduma za Jamii kuwa,kwa sasa wanafunzi wapatao 270 wako katika shule ya sekondari ya Chalinze ambako wanasoma kwa muda wakisubiri kukamilika kwa majengo mapya ya shule ya sekondari ya Chahua ambako walichaguliwa na kuwataka kamati ya ujenzi na mafundi kufanya kazi kwa bidii na weledi ili kukamilisha kwa wakati na kupunguza msongamano katika shule mama ya Chalinze.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati ya Huduma za Jamii Mheshimiwa Malota Hussein pamoja na wajumbe wa Kamati hiyo walifurahishwa na namna unavyotekelezwa mradi na kuwapongeza wasimamizi wa mradi huo na kuwataka kuongeza kasi ya ujenzi huo ili wanafunzi waanze kusoma mara moja,Malota katika ukaguzi wa miradi ya Elimu alisema Halmashauri yetu katika kuhakikisha wanafunzi wote wanaochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza tumedhamiria kuongeza vyumba vya madarasa kila mwaka kutokana na mapato ya ndani ili kummunga mkono Rais Magufuli kauli mbiu yake ya Elimu Bure kwa kila mtoto wa kitanzania Kwa kuweka miundombinu rafiki ya Elimu.


Malota aliongezea kwa kusema pamoja na kuanzisha shule hii lakini pia mwaka jana tumeanzisha shule nyingine ya sekondari katika mamlaka ya mji mdogo  Chalinze katika kitongoji cha Pingo,ambayo ni shule ya sekondari ya Pera. Shule hii nayo tumeipatia fedha za kitanzania milioni 104. Milioni 64 kwa ajili ya ujenzi wa maabara na milioni 40 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa.



Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • PPRA yatoa Mafunzo ya NeST kwa Watendaji wa Kata na Wakuu wa Shule Chalinze

    May 08, 2025
  • Watendaji wa Kata na Vijiji wapewa Mafunzo ya namna ya kukusanya Kodi ya Majengo Chalinze

    May 07, 2025
  • PPRA yatoa mafunzo ya Ununuzi kwa watumishi wa Afya Chalinze

    May 07, 2025
  • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango yafanya ziara kukagua miradi ya maendeleo

    May 06, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.