• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Shule ya Mtakatifu Alphonsa Mfano wa Kuigwa Chalinze

Imewekwa: July 23rd, 2022


Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Chalinze Mheshimiwa Hassani Mwinyikondo azitaka shule za Msingi za Serikali kuiga mazuri ya Shule ya Msingi ya Mtakatifu Alphonsa iliyopo katika kitongoji cha Msolwa kata ya Bwilingu.


Mwinyikondo ameyasema hayo leo katika mahafali ya kuhitimu wanafunzi wa darasa la saba katika Shule hiyo alipokuwa akihutubia kama mgeni rasmi. “Naupongeza uongozi wa Shule hii ya kanisa kwa matokeo mazuri mnayopata kila mwaka na kuibeba Halmashauri kutokana na ufaulu mzuri wa wanafunzi wanaosoma hapa,natamani na shule za Serikali zifanye vizuri kama inavyofanya shule hii.” Mwinyikondo alisema.


Shule ya Mtakatifu Alphonsa ni Shule ya kanisa Katoliki chini ya Masista wa Mtakatifu Alphonsa iliyoanzishwa mwaka 2012 na kupata usajili wa Wizara ya Elimu na kutoa wahitimu wa darasa la saba kwa awamu ya kwanza mwaka 2020.


Katika Mahafali hiyo   viongozi mbalimbali walihudhuria walioongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chalinze ambao ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chalinze,Bwana Ramadhani Possi,Kamanda wa Polisi wilaya ya Chalinze Bwana Hussein Mdoe,Afisa Mipango wa Halmashauri,Bwana Shambani Millao na Diwani wa kata ya Bwilingu Mheshimiwa Nassa Karama  na wazazi wa wanafunzi wahitimu.


Mahafali hiyo ilifana kwa kuwa na burudani mbalimbali zilizo andaliwa na wanafunzi wahitimu na wanaoendelea kama nyimbo ngonjera,maigizo sarakasi na michezo ya skauti. Burudani hizi zilionesha ni jinsi gani Shule hiyo inafundisha taaluma na kuibua vipawa mbalimbali walivyo navyo watoto na kuipa ubora sitahiki.


Mgeni rasmi katika mahafali hiyo aliweza kufanya shughuli mbalimbali kama kutoa kutoa zawadi kwa wanafunzi bora kwa masomo yote,zawadi kwa mwanafunzi bora kwa masomo yote na  zawadi kwa walimu bora walifaulisha wanafunzi kwa ufaulu wa juu kwa masomo wanayofundisha kama motisha kwa kazi nzuri waliyoifanya walimu hao.


Mheshimiwa Mwinyikondo alihitimisha kwa kutoa vyeti vya kuhitimu kwa wahitimu na kuwatakia mafanikio mema katika mitihani yao ya taifa itakayofanyika hivi karibuni  na kutoa wito kwa shule za Serikali kuwa na utaratibu wa motisha kwa walimu na wanafunzi ili kuamusha ari ya kujifunza kwa walimu na wanafunzi.


Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Chalinze Bwana Ramadhani Possi aliupongeza uongozi wa Shule pamoja na bodi ya Shule hiyo chini ya Mwenyekiti wa Bodi hiyo Mwl.Merickzedek Komba kwa kazi nzuri inayofanyika katika shule hiyo ya kuinua ufaulu wa wanafunzi kitaaluma na kuahidi kuendelea kutoa ushirikiano pindi Shule inapohitaji misaada mbalimbali husan misaada ya kitaalam na ushauri.


Naye kamanda wa polisi wilaya ya Chalinze Bwana Hussein Mdoe aliupongeza uongozi wa shule kwa jinsi wanavyowaandaa vijana katika masomo na ukakamavu hususan katika nyanja ya skauti na kutoa nasaha kwa vijana kutojihusisha na uhalifu katika kipindi watakacho kuwa nyumbani wakisubiri matokeo,badala yake waendelee kuwa waadilifu kama walivyofundishwa wakiwa shuleni.


Mwenyekiti wa Bodi yaShule ,Mwl. Komba kwa niaba ya Jumuiya nzima ya Shule ya Mtakatifu Alphonsa aliwapongeza wageni wote walioambatana na Mgeni rasmi,wazazi,walimu na wanafunzi kwa kushiriki kikamilifu katika shughuli ya mahafali na kuwaomba waendelee kuwa moyo wa upendo kwa jumuiya ya Mtakatifu Alphonsa siku zote.


Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • PPRA yatoa Mafunzo ya NeST kwa Watendaji wa Kata na Wakuu wa Shule Chalinze

    May 08, 2025
  • Watendaji wa Kata na Vijiji wapewa Mafunzo ya namna ya kukusanya Kodi ya Majengo Chalinze

    May 07, 2025
  • PPRA yatoa mafunzo ya Ununuzi kwa watumishi wa Afya Chalinze

    May 07, 2025
  • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango yafanya ziara kukagua miradi ya maendeleo

    May 06, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.