• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Tumebaini Wafugaji Wavamizi 78-DC Kawawa

Imewekwa: August 30th, 2018

Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo,Mheshimiwa Zainabu Kawawa amekutana na wananchi wa kijiji cha Pongwe Mnazi ili kutoa mrejesho wa hatua alizozichukua dhidi ya wafugaji wavamizi wanaoingia katika kijiji hicho na kuharibu amani ya wakazi wa kijiji hicho,"Kama wilaya tumeanza kuchukua hatua kwa wafugaji wavamizi wanaohatarisha amani ya wananchi, tumekwisha wabaini wafugaji wavamizi 78 vijiji vya Pongwe Kiona na Pongwe Mnazi hivyo tunaendelea na hatua mbalimbali kuhakikisha wanatoweka katika maeneo hayo."Mkuu wa wilaya alisema.

Mheshimiwa Kawawa amewataka wananchi kutoa ushirikiano wa hali ya juu katika mapambano dhidi ya wafugaji wanaoingia katika vijiji vya Halmashauri ya Chalinze bila utaratibu wa kisheria kwa kutoa taarifa ofisi ya Mkuu wa wilaya kwa hatua zaidi.

Aidha amewaonya watendaji wa vijiji,kata na wenyeviti wa vijiji wanaotoa vibali na kuwakaribisha wafugaji wavamizi kuingia katika vijiji bila kufuata taratibu za kisheria na kuahidi kuwachukulia hatua za kisheria

Kawawa aliendelea kusisitiza na kuziagiza Halmashauri za vijiji kukaa na kuainisha maeneo yanayofaa kwa ufugaji na kuona kiasi cha mifugo kinachotakiwa kwa kila kaya,hii ni operesheni maalum itakayoendelea kwa wilaya nzima ili kuondokana na migogoro na hatimaye kulinda tunu tuliyoachiwa na waasisi wetu ambayo ni amani. Mkuu wa wilaya alifafanua.

Kwa upande wake Afisa Ardhi na maliasili Bi Zaina Kijazi alisema eneo hili la Pongwemnazi halifai na halitoshi kwa shughul za ufugaji hivyo hakutakiwi kufanya shughuli za ufugaji mpaka hapo mpango wa matumizi bora ya Ardhi utakapopangwa na Halmashauri.

Naye Diwani wa kata ya Kimange  Hussein Hading'oka alimshukuru Mkuu wa wilaya kwa hatua za haraka alizozichukua katika kutokomeza Migogoro ya wakulima na wafugaji kwa muda mfupi tangu aanze Kazi katika wilaya ya Bagamoyo na kuahidi kutoa ushirikiano wa kina katika kutokomeza vitendo viovu vinavyofanywa na wafugaji dhidi ya wakulima.

Naye Mohammed Mkola ,Mzee maarufu alizungumza kwa niaba ya wananchi wa kijiji cha Pongwe Mnazi kwa kuiomba ofisi ya mkurugenzi mtendaji kuleta mtendaji wa kijiji  kwani mpaka sasa kijiji hakina mtendaji na hivyo shughuli za kijiji kutotekelezeka kwa ufasaha.

Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Bi Zainabu Kawawa alitoa maagizo kwa Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri kupeleka mtendaji Mara moja na Mkurugenzi aliahidi kutekeleza agizo hilo


Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • PPRA yatoa Mafunzo ya NeST kwa Watendaji wa Kata na Wakuu wa Shule Chalinze

    May 08, 2025
  • Watendaji wa Kata na Vijiji wapewa Mafunzo ya namna ya kukusanya Kodi ya Majengo Chalinze

    May 07, 2025
  • PPRA yatoa mafunzo ya Ununuzi kwa watumishi wa Afya Chalinze

    May 07, 2025
  • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango yafanya ziara kukagua miradi ya maendeleo

    May 06, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.