• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Upungufu wa Madawati kuwa Historia Chalinze

Imewekwa: December 11th, 2020

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo amekabidhi viti 221,meza 221,na madawati 305 leo katika shule za msingi na sekondari katika Halmashauri ya Chalinze, Mheshimiwa Ndikilo katika hotuba yake katika Mkutano uliofanyika katika kijiji cha Miono,alifurahishwa na uongozi wa Halmashauri ya Chalinze kwa jitihada za makusudi za kutekeleza maelekezo ya Waziri Mkuu katika kukamilisha utengenezaji wa madawati kwa shule za msingi 106 na shule za sekondari 21.


Mhandisi Ndikilo ameupongeza uongozi wa wilaya ya Bagamoyo na Halmashauri ya Chalinze kwa jinsi walivyojipanga kutengeneza madawati hayo na kukamilisha kwa wakati."Nakupongeza Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri,wakuu wa Idara wa Chalinze kwa jinsi mlivyojipanga vizuri kutekeleza maagizo ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kutengeneza madawati kwa ajili ya Wanafunzi wote wa sekondari na shule za msingi Hongereni sana kwa kazi nzuri."Ndikilo alisema.

Pamoja na pongezi hizo Mhandisi Ndikilo aliwataka Wanafunzi kusoma kwa bidii na kupata ushindi mzuri kwani mazingira ya kujifunzia ni rafiki kwao na kuwataka wazazi kuwasimamia watoto wao ili Elimu bora itakayowasaidia Katika maisha yao kwani urithi pekee na wenye tija ni Elimu na si vinginevyo.



Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo,Bi Zainabu Kawawa akitoa taarifa ya utekelezaji wa maagizo ya Waziri Mkuu kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo. Kawawa alisema Katika Halmashauri ya Chalinze suala la madawati litabaki kuwa historia,kwani shule zote za msingi 106 na shule za sekondari 21 zina madawati na hakuna mwanafunzi anayekaa chini. Utekelezaji wa zoezi hili ulianza mwezi Julai mwaka huu na leo tunahitimisha zoezi hili kwa kumkabidhi Mkuu wa Mkoa madawati ili aweze kugawa katika shule za msingi na sekondari zilizokuwa bado zinauhitaji.


Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo alimpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Chalinze Bwana Ramadhani Possi kwa jitihada anazozifanya kutekeleza maelekezo ya serikali kutokana na mapato ya ndani, sanjari na kufanya kazi kwa kushirikiana na wakuu wa Idara na Vitengo katika Halmashauri yake."Hongera Sana Mkurugenzi na Menejimenti yako kwa kujipanga vizuri na kutatua kero mbalimbali za wananchi." Kawawa alipongeza.


Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete alimshukuru Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo kwa jitihada zake katika kuhamasisha utekelezaji wa maelekezo ya serikali kwa wakati hususan Ujenzi wa miundombinu ya Elimu,kutokana na usimamizi bora leo Chalinze hatuna upungufu wa madawati kwa shule zetu zote za msingi na sekondari."Tunamshukuru sana Mkuu wetu wa Mkoa." Ridhiwani alisema.


Aidha Mheshimiwa Kikwete katika kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Halmashauri katika kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia alitoa jumla ya fedha za kitanzania Milioni 3.6 ili ziweze kutengeneza madawati kwa ajili ya wanafunzi,na kutokana na mchango huo inapelekea Halmashauri ya Chalinze kumaliza kabisa tatizo la upungufu wa madawati katika shule zote.


Kwa upande wa Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Kikaro waliotoa shukrani zao kwa Halmashauri ya Chalinze kupitia nyimbo walizoandaa zilizokuwa na maudhui ya kuipongeza serikali kwa kuboresha miundombinu ya Elimu.Waliimba nyimbo hizo mbele ya Mgeni Rasmi,ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo na kuipongeza serikali kwa mipango yenye tija.



Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • PPRA yatoa Mafunzo ya NeST kwa Watendaji wa Kata na Wakuu wa Shule Chalinze

    May 08, 2025
  • Watendaji wa Kata na Vijiji wapewa Mafunzo ya namna ya kukusanya Kodi ya Majengo Chalinze

    May 07, 2025
  • PPRA yatoa mafunzo ya Ununuzi kwa watumishi wa Afya Chalinze

    May 07, 2025
  • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango yafanya ziara kukagua miradi ya maendeleo

    May 06, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.