• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Usafi wafanyika kwa kina Chalinze

Imewekwa: April 29th, 2018

Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya  Chalinze,wafanyakazi na wananchi wa mamlaka ya mji mdogo wa Chalinze wameweza kutekeleza kwa vitendo agizo la Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samiah Suluhu Hassan la kufanya usafi wa mazingira kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi,Wananchi hawa wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji ,Bwana Edes Lukoa wamefanya usafi katika kituo cha afya Chalinze,stendi ya mabasi na soko kuu la Chalinze kwa kuzibua mitaro na kuzoa taka kwa kutumia lori la kuzolea taka,zoezi hili limefanyika jana Jumamosi kwa mwitikio wa hali ya juu.

                                                                                                      Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya Bwana Edes Lukoa akifanya usafi na wananchi wa Chalinze siku ya usafi

Baada ya shughuli ya usafi wananchi wa chalinze na wafanyabiashara wa soko la chalinze linalojulika kwa jina la Soko la kwa Mama Kaguo waliwasilisha maombi yao kwa Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya  Chalinze kutaka wajengewe soko ambalo litakuwa na mgawanyo mzuri kwa wafanyabiashara  kulingana na bidhaa wanazouza katika soko hilo,kupitia kwa Mjumbe wa kamati ya usafi ya soko Bwana Abdulratif Gama alisema”Kwa sasa hakueleweki lipi ni soko kuu na yapi ni masoko madogomadogo kwani hivi sasa tuna masoko matatu,hapa tulipo kwa Mama Kiguo,kuna soko jingine lijulikanalo kama kwa Kassim na soko la Shaabani Nguruka ,hivyo tunaomba tuwe na eneo maalum kwa ajili ya soko”.

Naye Diwani wa kata hiyo Mheshimiwa Lucas Lufunga aliungana na mawazo ya wakazi wa kata yake ya Bwilingu na kuomba halmashauri iweke mikakati ya kujenga soko jipya la wilaya kwani hivi sasa Chalinze ni halmashauri lakini pia ni mamlaka ya mji mdogo ina hitaji kuwekewa mipango mizuri na endelevu kwa maendeleo endelevu kwa vizazi vijavyo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa halmashauri Bwana Lukoa aliwataka wafanyabiashara kuwa na utamaduni wa kufanya usafi kila siku na hususan siku hii ya usafi kitaifa ambayo imepangwa na serikali kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi iwe ni siku ya usafi,kila mwananchi katika siku hii atekeleze wajibu wake kuanzia asubuhi saa moja hadi saa nne asubuhi hili ni agizo kila mwananchi anatakiwa kutii.”Nawakumbusha tena kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi wananchi mjitokeze kufanya usafi na hili lizingatiwe bila kupuuzwa”

Hata hivyo Bwana Lukoa alitoa ufafanuzi kuhusu uanzishwaji wa soko la kisasa na kituo cha mabasi kwa hapa Chalinze”Halmashauri inaendelea na mchakato wa kupata eneo kwa ajili ya ujenzi wa soko na kituo cha mabasi hivyo tuvute subira katika hili na tuzingatie usafi kwa hali tuliyo nayo kwa sasa”.Lukoa alisema.



Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • TANGAZO LA KAZI June 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Waziri Kikwete Apokea Hundi ya Tsh Milioni 52 kutoka kiwanda cha Keda

    June 21, 2025
  • Chalinze yapongezwa kwa Hati Safi Mfululizo miaka mitano

    June 18, 2025
  • Mwenyekiti wa UWT akagua miradi ya maendeleo Chalinze

    June 13, 2025
  • Madiwani wa Pangani waipongeza Chalinze kwa Miradi ya mapato ya ndani

    June 11, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.