• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Uzinduzi wa Chanjo ya Surua, Lubela na Polio - Chalinze

Imewekwa: October 22nd, 2019

Katibu Tawala wa Wilaya ya Bagamoyo Bi. Kasilida Mgeni amezindua rasmi zoezi la Chanjo ya Surua na Lubela pamoja na  sindano za polio kiwilaya katika kata ya Msata jana ikiwa na kaulimbiu Chanjo ni kinga kwa pamoja tuwakinge. Uzinduzi huo ulifanyika  zahanati ya Msata iliyopo kijiji cha Msata ikiwa ni kampeni ya nchi nzima ya kutoa Chanjo kwa jamii hasa watoto kuanzia umri wa miezi 9 mpaka miaka 5

Mara baada ya Mganga mkuu wa Wilaya Dkt.Ernest Kyungu kutoa taarifa fupi juu ya jitihada zinazofanyika ili kufanikisha zoezi zima la utoaji wa Chanjo ndipo mgeni rasmi Bi.Kasilida Mgeni akatoa neno kwa  wananchi pamoja na viongozi waliohudhuria hafla hiyo ya Uzinduzi wa chanjo.

‘’Nawaomba ndugu wananchi wa Kata ya Msata na Halmashauri ya Chalinze kwa ujumla  mjitokeze kwa wingi ili kushiriki kikamilifu zoezi hili kwa kuwapeleka watoto wenu kwenye zahanati inayotoa chanjo ili kuwakinga watoto na magonjwa ya polio, Lubela na Surua.’’Alisema Bi.Kasilida.

Hata hivyo aliongeza kwa kusema..

‘’Nahimiza kuwepo na ushirikiano  baina ya wazazi yaani baba na mama katika kushiriki shughuli hizi za chanjo kwani suala hili si la mama peke yake bali hata kina baba wanatakiwa kuwa mstari wa mbele katika kuhimiza na kutekeleza jambo hili hivyo  wazazi mshirikiane katika shuguli zote za kiafya zinazowahusu watoto wenu zitakazojitokeza hapo mbeleni’’

Naye Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Chalinze Bi. Amina Kiwanuka ametoa pongezi kwa wananchi na kusema..

‘’Nawapongeza wale wote mliojitokeza na kushiriki vyema katika kuleta watoto wenu ili kupata chanjo kwani chanjo ni kinga kwa watoto ambao ndio taifa la kesho hivyo basi bado nasisistiza  muwape taarifa na walioko majumbani kujitokeza kwa wingi ili kufanikisha jambo hili na kuzikinga afya za watoto wetu.’’

Aidha Diwani wa Kata ya Msata Mh.Selestine Semiono aliwataka wananchi kushirikiana vyema na watoa chanzo kwa kuwapa ushirikiano na kujitokeza kwa wingi ili kuwapeleka watoto wao kupata Chanjo nakufanya Chalinze iwe mstari wa mbele katika masuala ya afya.

Kwa niaba ya wananchi wa Kata ya Msata Bi.Mwajuma Mbwana  alitoa shukrani za dhati kwa kusema ‘Tunaishukuru Serikali yetu na Halmashauri yetu kwa ujumla kwa kuwezesha upatikanaji wa Chanjo hizi kwani zitasaidia kuondoa magonjwa haya katika jamii zetu hasa kwa watoto wetu.’

Ikumbukwe kuwa kampeni za utoaji Chanjo ilianza mnamo tarehe 17/10/2019 na kufikia tamati siku ya Jumatatu ya tarehe 21/10/2019(jana) lakini zoezi hili litakua ni endelevu kwa siku zote katika vituo vya Afya zahanati na Hospitali

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • TANGAZO LA KAZI June 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Waziri Kikwete Apokea Hundi ya Tsh Milioni 52 kutoka kiwanda cha Keda

    June 21, 2025
  • Chalinze yapongezwa kwa Hati Safi Mfululizo miaka mitano

    June 18, 2025
  • Mwenyekiti wa UWT akagua miradi ya maendeleo Chalinze

    June 13, 2025
  • Madiwani wa Pangani waipongeza Chalinze kwa Miradi ya mapato ya ndani

    June 11, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.