• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Vibanda 136 vya kufanyia Biashara vyaanza kujengwa Chalinze

Imewekwa: November 5th, 2022


Halmashauri ya wilaya ya Chalinze imeanza ujenzi wa vibanda 136 kuzunguka soko kuu la halmashauri la Bwilingu,ili kuwawezesha wajasiriamali na wafanyabiashara katika halmashauri ya Chalinze kufanya biashara katika vibanda hivyo na ndani ya soko. Ujenzi huo umeanza leo katika soko la Bwilingu na unategemea kukamilika ndani ya mwezi mmoja hadi mitatu ili wananchi waweze kuendelea na biashara kwa wakati.


Akitoa taarifa hiyo kwa vyombo vya habari Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chalinze,Hassani Mwinyikondo aliahidi kuwa ujenzi huo utakamilika kwa wakati na utatumia muda mfupi kwani halmashauri imejipanga kuhakikisha kuwa vibanda hivyo vinakamilika kwa wakati na kuanza kutumika.

“Halmashauri tumejipanga kuhakikisha tunaweka mazingira rafiki kwa wajasiriamali kufanya biashara kwa kutumia miundombinu rafiki inayoandaliwa na halmashauri kwa misingi ya kuwakwamua wanachalinze kiuchumi.” Mwinyikondo alisema.


Naye Diwani wa kata ya Bwilingu, Mheshimiwa Nassa Karama kwa niaba ya wananchi wa Bwilingu alipongeza juhudi za halmashauri ya wilaya ya Chalinze kwa uamuzi wa kujenga vibanda zaidi ya 136 vitakavyotumika kwa biashara kuzunguka soko la Bwilingu.

“Vibanda hivi vinajengwa kwa kutumia mapato ya ndani ya halmashauri na utakuwa mradi utakaoiletea halmashauri mapato na hatimaye kuweza kutoa huduma za jamii zenye tija kwa wananchi kama afya ,elimu na maji.” Mheshimiwa Nassa alisema.


Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Chalinze,Bwana Ramadhani Possi  alisema ujenzi wa vibanda 136 kuzunguka soko la Bwilingu ni mwendelezo wa ujenzi wa soko kwa maana ya ujenzi awamu ya pili,ujenzi awamu ya kwanza ilikuwa ni soko lenyewe na kwa sasa tunaanza awamu ya pili ya ujenzi wa vibanda ambavyo vitatumika na wafanyabiashara ujenzi huu utatumia fedha za kitanzania milioni 748.

“ Tulichelewa kuanza awamu ya pili ili tukamilishe zoezi la kulipa fidia kwa wananchi waliokuwa wanaidai halmashauri,kwa kuwa hili la fidia liko mbioni kukamilika ndiyo maana tumeanza rasmi na tunatarajia kazi hii ikamilike ndani ya muda mfupi na vibanda kuanza kufanya kazi.” Possi alisema.


Aidha Kamanda wa polisi wilaya ya kipolisi Chalinze SSP Hussein Mdoe aliahidi kutoa ushirikiano wa hali na mali kuhakikisha kuwa amani inakuwa ya kutosha katika maeneo yote ya kufanyia biashara na wananchi watafanya biashara kwa amani na utulivu.

“Jeshi la polisi tupo tayari kuilinda amani na kuwahakikishia wananchi usalama katika maeneo yote ya kufanyia biashara muda wote.” SSP Mdoe alisema.


Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • PPRA yatoa Mafunzo ya NeST kwa Watendaji wa Kata na Wakuu wa Shule Chalinze

    May 08, 2025
  • Watendaji wa Kata na Vijiji wapewa Mafunzo ya namna ya kukusanya Kodi ya Majengo Chalinze

    May 07, 2025
  • PPRA yatoa mafunzo ya Ununuzi kwa watumishi wa Afya Chalinze

    May 07, 2025
  • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango yafanya ziara kukagua miradi ya maendeleo

    May 06, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.