• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Vikundi vyenye sifa Chalinze vyatakiwa kufanya maombi ya mikopo kupitia wezesha Portal

Imewekwa: October 2nd, 2024



Na John Mlyambate


Vikundi mbalimbali vilivyopo ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze ambavyo vinakidhi vigezo, vimetakiwa kuwasilisha maombi yao ili kunufaika na mikopo kupitia mfumo wa kielektroniki wa Wezesha Portal. Hii ni fursa kwa vikundi vya wanawake, vijana, na watu wenye ulemavu ili kuimarisha shughuli zao za kujipatia kipato.


Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Chalinze, Bwana Ramadhan Possi, alitoa wito huu mnamo Septemba 30, 2024, wakati wa mahojiano maalum na kituo cha Redio Chalinze FM katika kipindi cha *Maskani ya Chalinze*. Kipindi hiki huruka kila Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa 10:00 jioni hadi saa 12:00 jioni, ambapo alieleza utekelezaji wa tangazo la kufunguliwa kwa dirisha la utoaji wa mikopo hiyo.


Bwana Possi alibainisha kuwa hadi kufikia Agosti 31, 2024, Halmashauri ya Chalinze tayari imetenga jumla ya Shilingi Bilioni 1.864 kwa ajili ya mikopo kwa vikundi vya wanawake, vijana, na watu wenye ulemavu. Fedha hizi zimetengwa kwa lengo la kuwawezesha wananchi kujikwamua kiuchumi na kuimarisha kipato cha kaya zao.


Katika mahojiano hayo, Bwana Possi alieleza kuwa Serikali imefanya maboresho katika utoaji wa mikopo kwa kuongeza umri wa wanufaika wa kundi la vijana kutoka miaka 18 hadi 45, tofauti na awali ambapo umri ulikuwa kati ya miaka 18 na 35. Alisema kuwa mikopo hii haina riba yoyote, hivyo kuwa fursa bora kwa wananchi kuacha kukopa mikopo yenye masharti kandamizi.


Aidha, Mkurugenzi alifafanua kuwa kiwango cha mikopo kinachotolewa kinaanzia shilingi laki tano hadi shilingi milioni 150 kwa wajasiriamali wadogo na wa kati. Alitoa shukrani kwa wananchi kwa kuwa wavumilivu tangu kusitishwa kwa mikopo hiyo Aprili 14, 2023, kwa lengo la kuboresha mfumo wa utoaji wa mikopo.


Kwa upande wake, Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii, Nyamayao Said Ally, alisisitiza kuwa vikundi vinavyotaka kukopeshwa vinapaswa kupitia mafunzo na kupata cheti cha utambuzi. Alisema vikundi vinaweza kupata msaada kutoka kwa watendaji wa kata na maafisa maendeleo ya jamii katika ofisi za kata ili kufanikisha maombi ya mikopo kwa njia bora na sahihi.


Serikali kupitia Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Mhe. Mohamed Mchengerwa, ilitoa tangazo la kufunguliwa kwa dirisha la utoaji wa mikopo kwa vikundi vya wanawake, vijana, na watu wenye ulemavu kuanzia Julai 2024, ikiwa ni sehemu ya jitihada za kukuza uchumi wa wananchi.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • PPRA yatoa Mafunzo ya NeST kwa Watendaji wa Kata na Wakuu wa Shule Chalinze

    May 08, 2025
  • Watendaji wa Kata na Vijiji wapewa Mafunzo ya namna ya kukusanya Kodi ya Majengo Chalinze

    May 07, 2025
  • PPRA yatoa mafunzo ya Ununuzi kwa watumishi wa Afya Chalinze

    May 07, 2025
  • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango yafanya ziara kukagua miradi ya maendeleo

    May 06, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.