• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Viongozi Jimbo la Chalinze wafanya ziara kujionea uharibifu uliofanywa na Mvua ilioambatana na Upepo Kata ya Pera

Imewekwa: March 6th, 2021

Mh Ridhiwani Kikwete (Mbunge jimbo la Chalinze) akiongozana na Mwenyekiti wa Halmashauri Mh. Geofrey Kamugisha na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Chalinze Ndugu: Ramadhani Possi, wamefanya ziara  na kuwatembelea  wakazi wa Kitongoji cha Pingo ambao nyumba zao zimebomolewa kwa upepo ulioambatana na mvua.

Wakiwa katika ziara hiyo Katani Pera, Viongozi hawa ambao ni nguzo ya Halmashauri ya Chalinze wameshuhudia uharibifu wa zaidi ya nyumba 30 ambazo zimeezuliwa paa kutokana na mvua iliyoambatana na upepo mkali, iliyonyesha katika maeneo hayo ya Pingo na maeneo mengine ya Halmashauri

Akizungumza baada ya kujionea athari hiyo iliosababishwa na mvua iliyoambatana na upepo mkali , Ridhiwani alisema kuwa wamepewa taarifa na uongozi wa Serikali ya kijiji kuhusiana na kadhia hiyo iliowapata.

"Tulijulishwa na uongozi wenu wa kijiji kuhusu kutokea kwa tukio hili, tumekuja tumejione hali halisi poleni sana kwa kadhia hii, tumeona yapo mambo yaliyo ndani ya uwezo wetu kama  Halmashauri tutayafanyiakazi, yaliyo juu yetu tutayawasilisha Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ili kuona ni namna gani tunasaidiana" alisema Ridhiwani.

Nae Mwenyekiti wa Halmashauri Mh. Geofrey Kamugisha alisema kuwa wamefika kwa lengo la kuwapa pole kwa tukio hilo, huku akieleza kwamba wamejionea nyumba zaidi ya 30 zilizokumbwa na maafa hayo, ambapo ametoa  pole kwa waadhirika wote na kueleza kuwa wanakwenda kukaa kama uongozi ili kuona ni namna gani wanaweza kuungana nao katika kutafuta suluhu ya haraka.

"Kama viongozi wa Halmashauri na wataalamu wetu tutakwenda kukaa kuona ni namna gani tunavyoweza kushirikiana katika kusaidiana kwenye janga hili, tunawapa pole endeleeni kuwa watulivu Serikali yenu sikivu ikiongozya na Rais Dkt John Joseph Pombe Magufuli ipo pamoja nanyi wakati wote wa shida na raha," alisema Mh. Kamugisha.

Akizungumza katika  eneo lililopata madhara Mkurugenzi Mtendaji Ndugu: Ramadhani Possi alisema “licha ya kuona hali halisi, yupo tayari kupokea maelekezo ya viongozi  kisha kufanyia kazi mambo yaliondani ya uwezo wa Halmashauri ili kuona ni naamna gani watakavyochukua hatua za haraka katika kutafuta suluhu ya janga hilo.

Akizungumza mbele ya Viongozi waliotembelea  eneo lililoathirika na Mvua ya upepo kwa niaba ya Waathirika wote Bi. Mariam Salehe na Bw. Muhidini Rashid walimpongeza Mbunge na msafara wake kwa kufika eneo lililoadhirika na kuwafariji, huku wakiwaombea baraka katika uongozi wao ili waendelee kuwatumikia wana-Chalinze wote.

"Tunawaombea dua muendelea kuwatumikia wananchi usiku na mchana, kitendo chako Mbunge Ridhiwani kuambatana na viongozi wenzako kuja kutufariji kimetuongezea imani kwenu, tunawashukuru sana," alisema Mariamu.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • PPRA yatoa Mafunzo ya NeST kwa Watendaji wa Kata na Wakuu wa Shule Chalinze

    May 08, 2025
  • Watendaji wa Kata na Vijiji wapewa Mafunzo ya namna ya kukusanya Kodi ya Majengo Chalinze

    May 07, 2025
  • PPRA yatoa mafunzo ya Ununuzi kwa watumishi wa Afya Chalinze

    May 07, 2025
  • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango yafanya ziara kukagua miradi ya maendeleo

    May 06, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.