• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Wakuu wa wilaya za Mafia na Kibiti Waapishwa Rasmi

Imewekwa: January 30th, 2023


Wakuu wa wilaya za Mafia na Kibiti leo wameapishwa rasmi na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mheshimiwa Abubakari Kunenge. Hafla fupi ya uapisho imefanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani wakuu wa wilaya waliokula kiapo ni Kanali Samwel Kolombo, ambaye ameapishwa kuwa Mkuu wa wilaya ya Kibiti na Ndugu Zephania Stephen Sumaye ambaye ameapishwa kuwa Mkuu wa wilaya ya Mafia.Hafla hiyo ya uapisho imeshuhudiwa na viongozi,ndugu,jamaa na marafiki.


Baada ya zoezi la kiapo wakuu wa wilaya hao walikula kiapo cha uadilifu kwa viongozi wa umma,kiapo hicho waliongozwa na Kaimu Kamishina wa maadili mkoa wa Pwani kinachowataka kutunza maadili kama viongozi wa umma kwa mujibu wa sheria.


Kwa Upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani Bi Zuwena Omary alitoa nasaha zake kwa wakuu wa wilaya waliokula kiapo na wakuu wa wilaya waliohamia katika mkoa wa Pwani na kuwatakia utumishi uliotukuka na kuwataka kusimamia ukusanyaji mapato katika halmashauri na kuwataka kuongoza kwa misingi utawala wa sheria na kuahidi kuwapa ushirikiano wa hali ya juu katika kazi.


Naye Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Pwani Msheshiwa Mwinshehe Mlao aliwakaribisha wakuu wa wilaya waliohamia na walioteuliwa na kuwataka wakatekeleze Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi kwa vitendo na kuwatakia utendaji mwema ndani ya mkoa wa Pwani.


Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mheshimiwa  Abubakar Kunenge katika hotuba yake baada ya kuwaapisha wakuu wa wilaya aliwakabidhi vitendea kazi kama wakuu wa wilaya na kuwataka wakawe watumishi waendako katika maeneo yao ya kazi,akawataka wakasimamie utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi, kusimamia vipaumbele vya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan na kuwataka kuzingatia utawala wa sheria (Rule of Law) katika kutekeleza majukumu ya serikali.


Mheshimiwa Kunenge amewataka wakuu wa wilaya mkoani Pwani kuyajua maeneo yao ya utawala sanjari na kujua mahitaji ya wananchi hususan Elimu,Afya na maji ili kuweza kuyasemea kwa mamlaka za juu kwa hatua zaidi.


Mkuu wa Mkoa alimalizia kwa kuwapongeza viongozi wa wilaya zote na halmashauri kwa kazi nzuri wanazozifanya za ukusanyaji wa mapato na kuwataka viongozi walioapishwa na waliohamia kuendeleza mazuri waliyoyakuta ili mkoa wa Pwani uendelee kusonga mbele.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • PPRA yatoa Mafunzo ya NeST kwa Watendaji wa Kata na Wakuu wa Shule Chalinze

    May 08, 2025
  • Watendaji wa Kata na Vijiji wapewa Mafunzo ya namna ya kukusanya Kodi ya Majengo Chalinze

    May 07, 2025
  • PPRA yatoa mafunzo ya Ununuzi kwa watumishi wa Afya Chalinze

    May 07, 2025
  • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango yafanya ziara kukagua miradi ya maendeleo

    May 06, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.