• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Walimu wapewa maelekezo ya kazi Chalinze

Imewekwa: July 10th, 2025



Na John Mlyambate, Chalinze


Tume ya Utumishi wa Walimu katika Wilaya ya Bagamoyo imetoa mafunzo maalum kwa walimu wapya walioajiriwa hivi karibuni katika Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze. Mafunzo hayo yamelenga kuwajengea uwezo waajiriwa hao kuhusu taratibu za kiutumishi pamoja na maadili yanayopaswa kuzingatiwa katika taaluma ya ualimu.


Mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete, yakihusisha wadau mbalimbali wakiwemo maafisa kutoka Ofisi ya Utumishi ya Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze na viongozi wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT). Walimu waliopatiwa mafunzo wanatoka katika shule za msingi na sekondari ndani ya halmashauri hiyo.


Akizungumza katika mafunzo hayo, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze, Bwana Archanus Kilaja, aliwataka walimu hao wapya kuwa na nidhamu ya kazi, kufanya kazi kwa weledi na kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zinazosimamia utumishi wa umma.


Bwana Kilaja alisisitiza kuwa ualimu ni wito unaohitaji moyo wa kujitolea na uwajibikaji wa hali ya juu. Alisema walimu wana nafasi muhimu katika kuandaa kizazi cha baadaye cha taifa, hivyo wanapaswa kufahamu kuwa wao ni kioo cha jamii na wanapaswa kuwa mfano bora kwa wanafunzi wao.


Aidha, aliwataka walimu hao kufuata mipango kazi ya shule na kushirikiana na walimu wakuu pamoja na viongozi wa elimu katika maeneo yao ya kazi. Alisema ushirikiano ni msingi wa mafanikio ya kitaaluma kwa walimu na ufaulu wa wanafunzi mashuleni.


Wawakilishi wa Ofisi ya Utumishi na CWT walisisitiza umuhimu wa walimu kufahamu haki na wajibu wao kazini. Pia walieleza kuwa serikali ipo tayari kuwasaidia walimu wanaotekeleza wajibu wao kwa bidii na uadilifu, lakini haitavumilia walimu watakaokiuka maadili ya kazi.


Mafunzo hayo yametoa fursa kwa walimu kujifunza kuhusu matumizi ya miongozo ya utumishi wa umma, namna ya kuandaa na kutekeleza mipango kazi ya kila siku, pamoja na kujenga mahusiano mazuri na wanafunzi, wazazi na jamii kwa ujumla.


Walimu wapya waliopatiwa mafunzo wametoa shukrani kwa tume na halmashauri kwa kuwaandalia mafunzo hayo, wakisema kuwa yamewaandaa vyema kwa safari ya kazi waliyoianza rasmi. Waliahidi kuwa watatumia mafunzo hayo kama mwongozo wa utendaji kazi wao wa kila siku.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • TANGAZO LA KAZI June 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Walimu wapewa maelekezo ya kazi Chalinze

    July 10, 2025
  • Kampeni ya Ugawaji vyandarua bila malipo yazinduliwa Chalinze

    July 10, 2025
  • Waziri Dkt Kijaji Azindua Kampeni ya Chanjo ya Mifugo Kitaifa Mkoani Pwani

    July 09, 2025
  • Waziri Kikwete Apokea Hundi ya Tsh Milioni 52 kutoka kiwanda cha Keda

    June 21, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.