• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Wanafunzi wa Shule ya Msingi Gongo wapatiwa Baiskeli

Imewekwa: February 29th, 2020


Shirika linalojishughulisha na uhifadhi na utunzaji wa mazingira(Savings Africa’s Nature)la kijiji cha Gongo Kata ya Mkange,Halmashauri ya Chalinze lenye makao yake makuu Jijini Dar es salaam,limetoa msaada wa baiskeli 35 kwa wanafunzi wa shule ya msingi Gongo iliyopo kata ya Mkange,msaada huo umetolewa kwa wanafunzi wanaotoka umbali wa kilometa zaidi ya kumi kuja kusoma shuleni hapo..


Wanafunzi hao wamekuwa wakifika shuleni kwa shida kutokana na wazazi wao kuishi kitongoji cha Tumbili kitongoji ambacho kiko umbali wa kilomita zaidi ya kumi ili kufika Gongo shule ya msingi.


Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Mwalimu Jeremiah Anthony Tito katika kupambana na changamoto iliyokuwa ikiwakabili wanafunzi wake alizungumza na uongozi wa shirika la uhifadhi na utunzaji mazingira ili wanafunzi hao waweze kupatiwa baiskeli ili kuwawezesha kuwahi masomo kwa wakati.


Mwalimu Tito akitoa ufafanuzi wa namna shirika lilivyoweza kujitoa ana sema,niliandika barua ya kuomba msaada kwa wafadhiri hao nikieleza changamoto za umbali wa mahali wanapoishi wanafunzi na shuleni. Uongozi wa shirika ulipokea maombi yangu nakuahidi kuyafanyia kazi.


Anaemdelea kusema shirika la Saving Afirica’s Nature hatimaye liliweza kupata jumla ya baiskeli 35 ambazo zimegawiwa kwa wanafunzi wapatao 25 baiskeli 10 bado zinafanyiwa marekebisho pindi zikikamilika nazo watagawiwa walengwa,pamoja na mgawanyo wa baiskeli hizo Kamati ya shule na Halmashauri ya kijiji cha Gongo zimeweka kanuni za namna ya matumizi ya baiskeli hizo.


Halmashauri ya kijiji inatakiwa kuhakikisha kwamba baiskeli hizo zinatumika kwa matumizi ya mwanafunzi kwenda shule na si vinginevyo,baiskeli hizo zitafanyiwa matengezo na shirika kila baada ya Miezi mitatu kwa matengenezo madogadogo mzazi atahusika moja kwa moja.


Aidha baiskeli hizo wanafunzi watazitumi hadi watakapo kamilisha masomo yao baada ya hapo watazirejesha shuleni na kupatiwa wanafunzi wengine, isipokuwa kwa mwanafunzi atakayemaliza masomo yake ya darasa la Saba na kupata ufaulu wa wastani wa alama “B” atabaki nayo kama zawadi yake na utaratibu huu utatumika kama motisha kwa wanafunzi kuongeza bidii katika masomo.


Katika hafla ya makabidhiano mmoja wa wanafunzi walinufaika na usafiri  aitwaye Rajabu Shabani alilishukuru shirika kwa niaba ya wanafunzi wenzake na kuahidi kusoma kwa bidii na kufika shuleni kwa wakati ili kuendelea na masomo pasipo kuchelewa.


Naye Afisa Elimu Msingi wa Halmashauri ya Chalinze Bi. Zainabu Juma Makwinya alilishukuru shirika la Saving Africa’s Nature kwa juhudi za makusudi za kuunga mkono serikali katika utoaji wa Elimu katika halmashauri ya Chalinze na kuwaomba wadau wengine kushiriki katika kuboresha miundombinu ya Elimu kwani uhitaji bado ni mkubwa katika sekta ya Elimu


Kwa upande wake mwakilishi wa shirika la Saving Africa’s Nature alisisitiza na kuwataka wazazi ,walimu na halmashauri ya kijiji wanasimamia matumizi sahihi ya baiskeli hizo ili kufikiwa malengo ya msaada huo kwa wanafunzi.


Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • PPRA yatoa Mafunzo ya NeST kwa Watendaji wa Kata na Wakuu wa Shule Chalinze

    May 08, 2025
  • Watendaji wa Kata na Vijiji wapewa Mafunzo ya namna ya kukusanya Kodi ya Majengo Chalinze

    May 07, 2025
  • PPRA yatoa mafunzo ya Ununuzi kwa watumishi wa Afya Chalinze

    May 07, 2025
  • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango yafanya ziara kukagua miradi ya maendeleo

    May 06, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.