• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Wananchi wa Chalinze watakiwa kuchangamkia fursa ya urasimishaji makazi

Imewekwa: August 22nd, 2023


Wananchi wa kitongoji cha Pera ,kata ya Pera katika Mamlaka ya Mji Mdogo wa Chalinze wametakiwa kuchangamkia fursa ya urasimishaji wa makazi kupitia Mradi wa Urasimishaji unaotekelezwa na serikali ya Tanzania kupitia Benki kuu ya Dunia . Kauli hiyo imetolewa leo katika Mkutano wa Uhakiki wa Milki za Ardhi(Public Display) uliofanyika leo katika Ofisi ya Mtendaji wa Kata ya Pera.


Akizungumza katika Mkutano wa uzinduzi wa zoezi la uhakiki wa milki za Ardhi, Meneja wa Urasimishaji Mijini wa Mradi kutoka Wizara ya Ardhi, Bwana Leons Peter Mwenda ametoa Elimu kwa umma juu ya faida za urasimishaji na umilki wa ardhi kwa wananchi wa Pera,amewataka wananchi kuwa makini katika zoezi hili la uhakiki milki za ardhi kabla ya kuanza kupandwa mawe katika viwanja vyao kwa kujiridhisha kuhusu taarifa zao walizojisajili kama ziko sahihi.


Mwenda katika Mkutano huo alieleza vitu vya msingi katika uhakiki wa milki za ardhi,ikiwa ni pamoja na usahihi wa majina ya mmilki yanayofanana na majina yaliyo katika vitambulisho vya utaifa,usahihi wa namba ya NIDA,namba ya simu iwe sahihi kwani ndiyo itakayotumika katika mawasiliano yote katika mchakato wa urasimishaji makazi,hivyo namba ya simu inatakiwa iendane na majina yaliyo kwenye kitambulisho cha NIDA.


Aidha Mwenda aliweza kufafanua aina mbalimbali za umilki kwa mujibu wa sheria ambazo wananchi wanaweza wakaamua kumilki kutokana na utashi wao. Umilki huo ni pamoja na Umilki wa pekee ni umilki ambao mtu anamilki pekee, Umilki wa pamoja usiogawanyika wa mke na mme,umilki huu ni maalum kwa mke na mme walioowana na mmoja wapo akifariki anayebaki anaendelea kuwa mmilki halali pasipo mchakato wowote wa mirathi.


Umilki mwingine aliotolewa ufafanuzi katika mkutano huo ni umilki chini ya msimamizi mlezi,umilki huu unafanywa na mzazi kama msimamizi wa mtoto ambaye hajafikisha miaka 18,hivyo kwa kuwa sheria za Tanzania haziruhusu umilki wa mali kwa mtu aliye na umri chini ya miaka 18 mzazi sharti awe mdhamini. Umilki mwingine ni umilki wa usimamizi wa mirathi na umilki wa ardhi kwa hisa.


Mgeni Rasmi katika uzinduzi wa zoezi la uhakiki wa Milki za ardhi, Mheshimiwa Mussa Gama,Mwenyekiti wa kamati ya Uchumi ,Ujenzi na Mazingira na Diwani wa kata ya Vigwaza aliishukuru serikali kwa mradi wa urasimishaji ardhi kwani ni suluhisho la migogoro katika halmashauri yetu ya Chalinze na kuwataka wananchi kushiriki kikamilifu katika zoezi hili muhimu la uhakiki wa milki za ardhi kwa faida yao.

 

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • PPRA yatoa Mafunzo ya NeST kwa Watendaji wa Kata na Wakuu wa Shule Chalinze

    May 08, 2025
  • Watendaji wa Kata na Vijiji wapewa Mafunzo ya namna ya kukusanya Kodi ya Majengo Chalinze

    May 07, 2025
  • PPRA yatoa mafunzo ya Ununuzi kwa watumishi wa Afya Chalinze

    May 07, 2025
  • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango yafanya ziara kukagua miradi ya maendeleo

    May 06, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.