• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Wanawake wajawazito waaswa kufika vituo vya afya pindi wanapohisi maumivu na uchungu

Imewekwa: July 9th, 2024

Wanawake wajawazito  wameaswa kuwahi kufika kwenye vituo vya Afya na Hospitali pindi wanapoanza kuhisi maumivu na uchungu ili waweze kufanyiwa vipimo kabla ya kujifungua kwa lengo la kuokoa maisha ya mama na Mtoto.

Hayo yamesemwa na Mganga mfawidhi wa kituo cha Afya  cha Chalinze Dkt Isdori Mfugale  leo Julai 8,2024 alipokuwa akifanya mahojiano na  kituo cha Chalinze fm kwenye kipindi cha Gumzo leo kinachoruka kila jumatatu hadi ijumaa kuanzia saa 04:00 hadi saa 07:00 mchana.

Pia Dkt Mfugale amesema mfumo huo unao muwezesha  mama kujifungua akiwa kwenye  beseni maalumu (Jacuzzi/water birth) lenye maji ya uvugu uvugu ni teknolojia  inayomwezesha  mama  mjamzito kujifungua mtoto wake akiwa ndani ya beseni hilo kwa kumpunguzia  maumivu chini ya  usimamizi na uangalizi maalumu kutoka kwa  wataalamu wa teknolojia hiyo na huduma  hiyo  imeanza kutolewa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili .

Akizitaja faida atakazo zipata mama mjamzito anapojifungulia kwenye beseni hilo amesema itamsaidia mama huyo kupunguza maumivu ,kupunguza uwezekano wa kuchanika wakati wa kujifungua, inamsaidia  kumuandaa kisaikolojia akiwa katika hali ya uchungu na kutumia muda mfupi  wakati wa kujifungua .Pia amesema  ni njia isiyo zuia maendeleo ya uchungu kwa mama mjamzito.

Aidha Dr Mfugale amesema  huduma hiyo ni salama kwa mama na mtoto kama itafanywa na wataalamu wanaotoa huduma hiyo.Pia ni huduma inayohitaji maandalizi mbalimbali ikiwemo na upimaji wa afya kwa kumfanyia mama huyo vipimo ili afahamu kama ana vigezo vinavyo ruhusu kujifungua katika beseni hilo maalumu.

Sanjari na hayo ametaja sababu zinazosababisha mama kutoweza kujifungua katika beseni hilo maalumu ni pamoja kuwa na maambukizi ya UKIMWI,homa ya ini,asiwe na changamoto kwenye via vya uzazi pia  awe na uwezo wa kujifungua pasipo kufanyiwa upasuaji.Kadhalika kwa upande wa mtoto anapaswa awe katika mlalo ulio sahihi pindi anapokuwa tumboni.

Vile vile Mganga mfawidhi wa kituo cha Afya cha Chalinze ametoa wito kwa watoa huduma kuwa na lugha rafiki wakati wa kuwahudumia kina mama hao wanapo jifungua  ili kuwasaidia kuwaandaa kisaikolojia itakayo pelekea mama huyo kujifungua salama.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • PPRA yatoa Mafunzo ya NeST kwa Watendaji wa Kata na Wakuu wa Shule Chalinze

    May 08, 2025
  • Watendaji wa Kata na Vijiji wapewa Mafunzo ya namna ya kukusanya Kodi ya Majengo Chalinze

    May 07, 2025
  • PPRA yatoa mafunzo ya Ununuzi kwa watumishi wa Afya Chalinze

    May 07, 2025
  • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango yafanya ziara kukagua miradi ya maendeleo

    May 06, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.