• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Watendaji simamieni majukumu yenu na kufanya maamuzi kwa mujibu wa kanuni, sheria na taratibu

Imewekwa: March 16th, 2021

Hayo yamesemwa leo na  Mwenyekiti wa Halmashauri Mh. Geofrey Kamugisha alipofanya kikao chake cha kwanza na watendaji wote wa Vijiji na Kata katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze.

Mwenyekiti wa Halmashauri Mh. Geofrey Kamugisha amefanya kikao cha pomoja na watendaji wa Kata na Vijiji wote ili kuwasikiliza changamoto zao na kuona namna ambavyo anaweza kuzitatua ili kuwawekea mazingira mazuri ya ufanyajikazi kwa ajili ya ustawi wa Chalinze.

Awali akizungumza kabla ya kuruhusu kupokea changamoto kwa watendaji  Mh. Kamugisha aliwaambia watendaji hao madhumuni ya kuwa na kikao cha pamoja ni kusikiliza changamoto zinazowakabiri katika maeneo yao ya kazi. Aidha Aliwataka watendaji kusimamia kwa weredi ukusanyaji wa mapato katika maeneo yao ili kuiwezesha Chalinze kupata fedha za kutosha zitakazosaidia katika utekelezaji wa mambo mbalimbali ya maendeleo katika maeneo yao.

Akitoa dira ya Halmashauri, aliwaambia Halmashauri ya Chalinze imepanga kufanya mambo mengi na kutekeleza miradi mkakati ili kuongeza vyanzo vya mapato. Miongoni mwa miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa stendi ya mabasi Chalinze, Maegesho ya Magari makubwa, Soko, ununuzi greda, ununuzi Matrekta angalau moja kwa kila kata na upimaji wa ardhi ili miradi hii yote iweze kusaidia kuongeza mapato katika Halmashauri.

hivyo Watendaji wakiwa kama wasimamizi wanahitaji kusimamia upatikanaji wa mapato kwa kuziba mianya yote ambayo inaweza pelekea upotevu wa mapato.

“Lengo la kila Halmashauri katika nchi yetu ni kuona inatekeleza mambo yake iliyo jiwekea  katika bajeti  kwa asilimia (100%) ili kuleta ustawi wa wananchi wakazi na wapitao katika maeneo yao. kufikia adhima hiyo, niwajibu wa kila mtu ikiwa ni pamoja na watendaji na  wanasiasa kuhakikisha wanasimamia upatikanaji wa fedha (mapato) katika maeneo yao, hili linaenda sambamba na uibuaji wavyanzo vipya ili Halmashauri isitegemee chanzo kimoja tu kikuu yaani machimbo ya kokoto”. Alisema  Mh. Kamugisha

Aidha Mh. Kamugisha aliongezea kusema, “Nimekuwa nikikutana na changamoto mbalimbali niwapo katika ziara zangu vijijini na changamoto nyingi husababishwa na watendaji kushindwa kufanya maamuzi kwa wakati, hivyo nawaagiza leo watendaji wote kufanya kazi zenu pasipo kuyumbishwa wala kuogopa chochote lakini zingatieni sheria , kanuni, taratibu na miongozo iliyowekwa.”

Akihitimisha, Mh. Kamugisha alisema, “Zipo changamoto nyingi ambazo kama Watendaji mmezizungumza ikiwemo ugumu wa uendeshaji wa ofisi kwa kutokuwapo na fungu la kutosha, kama kiongozi napenda kuwaahidi kuwa nimezichukua changamoto zenu na ninakwenda kuzifanyia kazi moja baada ya nyingine. Yapo mambo ambayo mmeyasema na tayari yapo kwenye mpango wa bajeti wa mwaka wa fedha ujao na mengine yapo kwenye utekelezaji wa bajeti ya mwaka wa fedha unaoendelea hivyo tuendelee kuwasiliana pale ambapo mtaona mambo hayaendi sawa”.

Aidha Mh. Kamugisha aliwakumbusha watendaji wa vijiji pamoja na kata kuwa mpaka sasa Serikali imefanikiwa kununua pikipiki kwa maafisa Ugani na Mifugo wa Kata, Waratibu wa Elimu kata wote na watendaji wa kata wote ni adhima ya serikali kununua pikipiki kwa watendaji wa vijiji wote. Pia aliwasihi, kwa kuwa vijiji ni vingi, hutekelezaji huo utafanyika kwa awamu kwa kuzingatia vijiji vyenye changamoto zaidi ndivyo vitakavyopewa kipaombele.

Aliwataka watendaji kutokua chanzo cha migogoro na kuhakikisha wanasimamia matumizi bora ya ardhi kwa kuwaongoza wafugaji na wakulima katika maeneo yao na kusimamia namna bora ya uendeshaji wa shughuli za kiuchumi ili pasiwepo migongano ya aina yoyote ambayo inaweza sababisha kutokea kwa uvunjifu wa amani.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • PPRA yatoa Mafunzo ya NeST kwa Watendaji wa Kata na Wakuu wa Shule Chalinze

    May 08, 2025
  • Watendaji wa Kata na Vijiji wapewa Mafunzo ya namna ya kukusanya Kodi ya Majengo Chalinze

    May 07, 2025
  • PPRA yatoa mafunzo ya Ununuzi kwa watumishi wa Afya Chalinze

    May 07, 2025
  • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango yafanya ziara kukagua miradi ya maendeleo

    May 06, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.