• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Watendaji wa Kata na Vijiji wapewa Mafunzo ya namna ya kukusanya Kodi ya Majengo Chalinze

Imewekwa: May 7th, 2025

Na John Mlyambate


Watendaji wa Kata na Vijiji katika Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze wamepatiwa mafunzo maalum kuhusu ukusanyaji wa kodi ya majengo (Property Tax) ili kuongeza ufanisi wa ukusanyaji wa mapato katika maeneo yao ya utawala. Mafunzo hayo ni sehemu ya jitihada za serikali katika kuhakikisha kuwa kila mwananchi anayemiliki jengo analipa kodi stahiki kwa maendeleo ya taifa.


Mafunzo hayo yametolewa na wataalam kutoka Sekretarieti ya Mkoa wa Pwani kwa kushirikiana na wataalam wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze. Watendaji kutoka kata zote 15 pamoja na vijiji 74 vya halmashauri hiyo walishiriki katika mafunzo hayo ambayo yalilenga kuwawezesha kiufundi na kisheria juu ya zoezi hilo muhimu la ukusanyaji wa mapato.


Katika mafunzo hayo, washiriki walipewa elimu juu ya njia mbalimbali za ukusanyaji wa kodi ya majengo, matumizi ya mifumo ya kielektroniki katika ukusanyaji huo, pamoja na viwango vya tozo vinavyopaswa kutozwa kwa mujibu wa sheria. Pia walielezwa taratibu sahihi za kukusanya kodi hiyo, uthamini wa majengo, na wigo mpana wa ukusanyaji kodi katika maeneo yao.


Mafunzo hayo yalilenga kuhakikisha kuwa watendaji wanakuwa na uelewa wa pamoja kuhusu mchakato mzima wa ukusanyaji wa kodi ya majengo, kuondoa mkanganyiko uliokuwepo awali, na kuhakikisha kuwa hakuna mapato yanayopotea kutokana na kutokuwepo kwa taarifa sahihi au ufuatiliaji hafifu.


Aidha, watendaji wa kata na vijiji walipewa majukumu mahsusi ya kufanikisha ukusanyaji wa kodi katika maeneo yao. Walielekezwa kuhakikisha wanatambua majengo yote, wanashirikiana kwa karibu na wananchi, na wanatumia vizuri mifumo ya kielektroniki iliyowekwa kwa ajili ya ukusanyaji wa kodi hiyo.


Serikali ya Wilaya ya Chalinze inaamini kuwa kupitia mafunzo hayo, ukusanyaji wa kodi ya majengo utaongezeka kwa kiasi kikubwa, hali itakayoiwezesha halmashauri kutoa huduma bora zaidi kwa wananchi kupitia mapato ya ndani yatakayopatikana.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • PPRA yatoa Mafunzo ya NeST kwa Watendaji wa Kata na Wakuu wa Shule Chalinze

    May 08, 2025
  • Watendaji wa Kata na Vijiji wapewa Mafunzo ya namna ya kukusanya Kodi ya Majengo Chalinze

    May 07, 2025
  • PPRA yatoa mafunzo ya Ununuzi kwa watumishi wa Afya Chalinze

    May 07, 2025
  • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango yafanya ziara kukagua miradi ya maendeleo

    May 06, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.