WAZIRI wa Maji Juma Aweso ametoa maelekezo kwa Mamlaka za maji nchini kuhakikisha wanawaunganishia maji wananchi wanaoomba ndani ya siku saba.
Awesome alitoa maelekezo hayo leo wakati kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji ilipofanya ziara ya kukagua miradi katika Halmashauri ya Chalinze wilaya ya Bagamoyo.
"Hatutaki kusikia mwananchi ameomba kuunganishiwa maji anakaa miezi sita bila kupata huduma hiyo kuanzia sasa anayeomba huduma hiyo isizidi siku saba awe ameunganishiwa" alisema.
Aidha alisema hatapenda kusikia mtendaji wa chini anawagombanisha na wananchi wanaohitaji kuunganishiwa maji kwa muda na badala yake kuchukua muda mrefu kufanya kazi hiyo.
Awesome pia alielekeza watu wenye madeni sugu ya bili za maji kufika kwenye mamlaka za maji wakubaliane walipe kidogokidogo wakati huo wakiwa wameunganishiwa maji.
Aliiahidi kamati hiyo kufanyia kazi ushauri wanaoutoa huku akisema kuwa Mamlaka ya maji Vijijini na Mijini (RUWASA) haitakuwa kikwazo katika utekelezaji wa miradi.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji Dkt Christine Ishengoma aliipongeza Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Dar es Salam (DAWASA) kwa namna wanavyopambana kufikisha huduma ya maji kwa wananchi.
Dkt Ishengoma alisema ipo mikoa ambayo ina mgawo wa maji tofauti na mkoa huo wa Pwani ambao kikwazo hicho hakipo na Mamlaja zinafanya kazi nzuri katika miradi inayotekelezwa..
Katibu Mkuu wa wizara ya Maji Anton Sanga aliipongeza Dawasa kwa kuonyesha kwa vitendo thamani ya fedha kwenye miradi ambapo aliendelea kusisitiza wananchi kuunganishiwa mani.
Mtendaji mkuu wa DAWASA Cyprian Luhemeja alisema watatatekeleza maagizo yaliyotolewa na Waziri wa maji ya kuwarejeshea maji wenye madeni sugu ili wakati wanalipa madeni yao pamoja na kuwaunganishia maji
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge alisema kuwa kwasasa maji yanapatikana kwa asilimia 80 na kwamba lengo ni kufikia asilimia 95 kwa mjini na Vijiji 84.
114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu
Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze
Simu: +255232935403
Simu ya mkononi:
Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz
Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.