• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia awataka Watanzania kuchangia Miundombinu ya Elim

Imewekwa: November 9th, 2022


Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda ameishukuru na kuipongeza Taasisi ya FLAVIANA MATATA ( Flaviana Matata Foundation) kwa kuboresha na miundombinu ya Elimu na kujenga nyumba za walimu zipatazo nne(4) katika shule ya msingi Msinune iliyopo kata ya Kiwangwa Katika Halmashauri ya Chalinze Mkoani Pwani.


Pongezi hizo amezitoa jana katika hafla ya ufunguzi wa nyumba hizo shuleni hapo,Profesa Mkenda katika hotuba yake alifurahishwa na moyo wa upendo wa Taasisi hiyo kwa kuamua kutatua changamoto ya upungufu wa nyumba za walimu nchini.


Profesa Mkenda aliwataka watanzania kuwa na utamaduni wa kuchangia miradi ya Elimu kama tunavyoweza kuchangia na kufanikisha shughuli za kijamii kama misiba , arusi na ugonjwa. Hali kadhalika aliwasihi watanzania kushiriki kikamilifu katika kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia kwani kwa kufanya hivyo ni sehemu ya ibaada mbele za Mungu.

“Watanzania tuchangie maendeleo ya elimu kwa kuboresha miundombinu ya elimu katika shule zetu tulizosoma popote zilipo hapa nchini Tanzania na mfano mzuri nitaonyesha mimi kama kiranja wa elimu, nitachangia katika shule zote nilizopita kuanzia shule ya Msingi na sekondari.” Profesa Mkenda alisema.


Pamoja na nasaha alizozitoa kwa kwa watanzania aliahidi kuendelea kuboresha mzingira ya kufundishia na kujifunzia kwa kuendelea kujenga vyumba vya madarasa,nyumba za walimu,maabara,ajira kwa walimu wa masomo ya sayansi na ujenzi wa vyoo,kupitia Mamlaka ya Elimu Tanzania(TEA).


Aidha Mheshimiwa Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia aliwahakikishia wanachalinze kuwa uanzishwaji wa chuo cha Elimu ya Ufundi VETA Kwa halmashauri ya Chalinze upo katika hatua nzuri na muda si mrefu mchakato wa uanzishaji utaanza.


Kwa upande wake Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete alitoa shukrani za dhati kwa Taasisi ya Flaviana Matata kwa kazi nzuri na ya kizalendo kwa kuwajali walimu wa shule ya Msingi Msinune na wanachalinze kwa ujumla.

“Naishukuru serikali ya awamu ya sita chini Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuboresha miundombinu ya elimu kwani hivi juzi halmashauri ya wilaya ya Chalinze tumepokea jumla ya fedha za kitanzania bilioni 1.2 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa 60 kwa ajili ya wanafunzi watakaoanza kidato cha kwanza 2023, shukrani kwa serikali.” Ridhiwani alisema.


Naye Mkurugenzi  Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania Bi Bahati Geuzye alieleza majukumu ya Mamlaka ya Elimu Tanzania kuwa ni kusaidia kuboresha miundombinu ya elimu kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa Elimu nchini.

“Mamlaka ya Elimu tumeboresha miundombinu ya Elimu sehemu mbalimbali hapa nchini mfano mzuri ni hapa Msinune tumeweza kushirikiana na Taasisi ya Flaviana Matata katika ujenzi wa nyumba hizi zinazofunguliwa leo.” Mkurugenzi alisema.


Kwa upande Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Flaviana Matata,Bi Flaviana Matata aliwaomba watanzania kuunga mkono juhudi zake katika kuwasaidia watanzania wenye uhitaji katika nyanja mbalimbali kwa chochote walichonacho ili kusukuma gurudumu la Maendeleo nchini Tanzania.


Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Chalinze Mheshimiwa Hassani Mwinyikondo alipata fursa ya kutoa neno la shukrani kwa niaba ya Halmashauri ya Chalinze , aliishukuru serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri inazofanya kuboresha maisha ya wanachalinze katika sekta mbalimbali kama Elimu,Afya, Kilimo na Maji. Mwinyikondo alitoa shukrani za dhati kwa Bi Flaviana Matata kwa uzalendo uliotukuka katika kwa kuiona changamoto ya ukosefu wa Nyumba na kuifanyia kazi mara moja 


Aidha Mwinyikondo alimshukuru Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia,Profesa Mkenda kwa ahadi yake ya kuanzisha chuo cha VETA  na akaahidi kutoa ushirikiano wa hali ya juu Katika uanzishaji wa chuo hicho.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • PPRA yatoa Mafunzo ya NeST kwa Watendaji wa Kata na Wakuu wa Shule Chalinze

    May 08, 2025
  • Watendaji wa Kata na Vijiji wapewa Mafunzo ya namna ya kukusanya Kodi ya Majengo Chalinze

    May 07, 2025
  • PPRA yatoa mafunzo ya Ununuzi kwa watumishi wa Afya Chalinze

    May 07, 2025
  • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango yafanya ziara kukagua miradi ya maendeleo

    May 06, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.