• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Zingatieni Kanuni za Kilimo cha Pamba-Ndikilo

Imewekwa: May 24th, 2018

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo amewapongeza wakulima wa zao la pamba katika halmashauri ya wilaya ya Chalinze,pongezi hizo amezitoa leo katika ziara yake ya kikazi aliyoifanya katika vijiji vya kata za Mbwewe,Mandera na Miono.Mheshimiwa Ndikilo amekagua  na kuona kilimo cha zao la pamba katika kijiji cha Kwamkonje na kuona jinsi zao hili linavyostawi katika halmashauri ya wilaya ya Chalinze.

Katika ukaguzi huo Mheshimiwa amewataka wananchi wa Chalinze na Mkoa wa Pwani kwa ujumla kupambana na umaskini kwa kulima mazao ya pamba na korosho kwani mazao haya yanastawi vizuri katika mkoa wa Pwani”Nimefarijika na taarifa ya Mkurugenzi wa Halmashauri lakini pia kauli ya mwenyekiti wa halmashauri kwamba zao la pamba linakubali na pia nimejionea mwenyewe”Mhandisi Ndikilo alisema.

Aidha Mkuu wa mkoa aliwataka wakulima wa zao la pamba kuzingatia masharti na kanuni za kilimo bora katika uzalishaji ili kulijengea thamani na kutoliharibu kwa kuchanganya maji na mchanga kwani kufanya hivyo hupelekea kufa kwa soko la pamba katika soko la kimataifa na kupelekea umaskini kwa wanchi au wakulima wa pamba.Ndikilo amewataka wananchi kulima kwa wingi zao la pamba kwani serikali inatoa mbegu,viuatilifu na soko la uhakika kwa wakulima wa zao hili.

Katika ziara hiyo Mkuu wa Mkoa aliweza pia kuona na kukagua kiwanda cha kuchambua pamba katika kijiji cha Mandera,kiwanda ambacho hakifanyi kazi na aliagiza wataalam wa masuala ya umeme kukifanyia uchunguzi zaidi ili kiweze kufanyakazi ya kuchambua pamba kwani malighafi kwa ajili ya kiwanda hicho inapatikana katika mkoa wa Pwani kwa sasa.

Mhandisi Ndikilo alitembelea msitu wa Uzigua ujulikanao kama “Uzigua Forest”ili kuona ustawi wa msitu huo ambao bado unakaliwa na wafugaji kitu ambacho ni kinyume na sheria za misitu.Katika hili Mhandisi Ndikilo aliagiza kuwa zoezi la kuwaondoa wafugaji katika msitu wa Uzigua liwe endelezu ili kuulinda msitu huu kwani ni chanzo cha mvua katika maeneo yetu na pia ni kivutio cha utalii kwani hata wanyama waliotoweka hapo awali wameanza kurejea.”Mkuu wa Wilaya zoezi hili liwe endelevu ili kunusuru msitu huu.”Ndikilo aliagiza.



Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango chafanya kikao kujadili mapato na matumizi kwa mwezi Aprili 2025.

    May 31, 2025
  • Maafisa Habari watakiwa kuitangaza miradi ya serikali

    May 30, 2025
  • Halmashauri ya Chalinze yatembelewa na wawekezaji wa nyumba

    May 29, 2025
  • Kampeni ya "Ni rahisi sana"yatoa Elimu kuhushu usalama Mtandaoni Chalinze

    May 28, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.