Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Chalinze limeketi leo katika Ukumbi wa Halmashaurikujadili kujadili uanzishwaji wa Wilaya Mpya ya Chalinze.Baraza hilo limeitishwa maalumu kwa ajenda moja mahsusi ya kuanzishwa kwa wilaya ya Chalinze.
Baraza hilo limehudhuriwa na viongozi mbalimbali katika Wilaya ya Bagamoyo ambao ni Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo,Katibu Tawala wa Wilaya na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama
Kuanzishwa kwa Wilaya ya Chalinze ni kutokana na ahadi ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kuipandisha Halmashauri ya Chalinze kuwa Wilaya kutokana na kukuwa kwake na kuwa na uwezo wa kujiendesha hususan uwezo wake wa kukusanya mapato ya ndani.
Kwa upande wake Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete alipopata fursa ya kutoa salamu katika Baraza hilo alimshukuru Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwa uamuzi wa busara kuipandisha hadhi Halmashauri ya Chalinze na kuifanya kuwa wilaya,pia aliwashukuru Madiwani na wataalamu wa Halmashauri kwa kufanya kazi kwa ushirikiano na kuwataka wasonge mbele kwa maslahi ya wana Chalinze.
Naye Mkuu wa Wilaya Mheshimiwa Zainabu Rashid Kawawa aliwapongeza wanachalinze, Madiwani na wataalamu kwa kufanya kazi kama timu na kuwatakia mafanikio zaidi Katika utekelezaji wa miradi na kuwapongeza Menejimenti ya Halmashauri kwa kutekeleza miradi mizuri na kwa kiwango kizuri.
Katika kikao cha Baraza hilo lililoongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri Mheshimiwa Geofrey Kamugisha, Madiwani kwa kauli moja walikubaliana Wilaya ya Chalinze ianzishwe kwa kuzingatia mipaka ya Halmashauri ya Chalinze pasipo manadiliko yoyote.
Lugoba Chalinze
Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze
Simu: +255232935403
Simu ya mkononi:
Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz
Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.