• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Biteko: Fanyeni siasa za kubadilisha maisha ya watu si maneno

Imewekwa: October 11th, 2023



Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Dotto Biteko amesema ili kuwa na maendeleo ni vema kufanya siasa za kubadili maisha ya watu badala ya siasa za maneno.


Vilevile amesema Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wanatakiwa kuacha kujiingiza kwenye matusi na kejeli badala yake wa waelezee yale waliyofanyika kwenye maeneo.


Biteko ameyasema hayo leo mjini Lugoba alipokuwa akihutubia Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) pamoja na Wakazi wa Jimbo la Chalinze kwenye mkutano wa kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani uliondaliwa na Mbunge wa jimbo hilo Ridhiwani Kikwete.


Naibu Waziri Mkuu huyo alisema muda huu ni wakuelezea Maendeleo yaliyofanyika na si kuishia kuongea na kuacha watu wengine kuzungujza maneno ya kejeli kwa Serikali iliyopo madarakani.


Kadhalika alisisitiza wanachama hao kuachana na siasa za utambulisho na kuwa na siasa za Maendeleo sambamba na kushirikiana kwa kila jambo kushikamana.


"Shikamaneni, thaminianeni na kuvumiliana angalieni yanayowaweka pamoja badala ya yale yanayowatenganisha tusiingie kwenye matusi na kejeli kazi yetu iwe ya kuyasemea yale yaliyofanywa na serikali" alisema.


Pia aliwataka Watumishi kushirikiana na wananchi kuwafuata walipo na kutagua kero zao badala ya kukaa kwenye madawati ofisini wakiwasubiri.


" Wananchi wanachohitaji ni huduma tuwapelekee maendeleo huko waliko rasilimali fedha zilizopo zitumike kwa kiwango kinachotakiwa" 


Katika hatua nyingine Naibu Waziri Mkuu huyo na Waziri wa Nishati ameagiza uongozi wa Tanesco Mkoa wa Pwani kuhakikisha wanaunganisha umeme kwenye shule ya Sekondari Moreto ambapo aliahidi kupeleka kompyuta kumi ili wanafunzi hao waweze kusoma maomo ya sayansi.


Akizungumza katika mkutano huo Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt.Jakaya Kikwete ambae pia alikuwa mbunge wa kwanza jimbo la Chalinze alisema, uteuuzi wa Naibu Waziri Mkuu Biteko sio jambo la kushangaza kwani ni Naibu Waziri wa tatu sasa.


Alisema ,Rais Samia Suluhu Hassan amefanya chaguo sahihi  kwa katumia Mamlaka yake ya kikatiba kuteua.


"Biteko fanyakazi zako,kwa mujibu wa katiba ya nchi,mwenye Mamlaka ya kufanya maamuzi ni Rais, na katumia Mamlaka yake ya kikatiba,midomo imeumbiwa kusema,waache waseme.”


Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete amesema jimbo hilo katika utekelezaji wa ilani umefikia asilimia 96.


Kikwete alisema tayari sh. Bilioni sita zimepokelewa katika Halmashauri ya Chalinze kutekeleza mambo mbalimbali ya maendeleo na kuondoa vikwazo vilivyokuwepo awali.


Akizungumzia upande wa Elimu Mbunge huyo ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora aliishukuru Serikali wakati anaingia katika nafasi ya Ubunge wa jimbo hilo kulikuwa na shule za Sekondari 17 na sasa zinefikia 25 ikiwa ni ongezeko la shule nane.


Aidha alibainisha kwamba ujenzi wa shule za msingi umeongezeka na kuondoa kikwazo cha mlundikano wa wanafunzi darasani na sasa kufikia 113, huku zahanati zikiongezeka kutoka 36 hadi 61 na vituo vya afya ambavyo sita viko katika hatua ya ukamilishaji kutoka vinne vilivyokuwepo awali.


Kadhalika alisema huduma ya maji imeongezeka kutoka lita 7,500 hadi kufikia milion 21 vioski 114 hadi 1224 na wakazi wanaopata huduma sasa wamefikia asilimia 96 kutoka 62 za awali.


Kwa mujibu wa Kikwete upande wa nishati ya umeme shule za msingi 108 zimeunganishwa umeme Sam amba na Vijiji vyote 75 katika kata 15 za Halmashauri ya Chalinze huku akiwahamasisha wananchi kuwa na mwamko wa kuunganisha nishati hiyo.


Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • PPRA yatoa Mafunzo ya NeST kwa Watendaji wa Kata na Wakuu wa Shule Chalinze

    May 08, 2025
  • Watendaji wa Kata na Vijiji wapewa Mafunzo ya namna ya kukusanya Kodi ya Majengo Chalinze

    May 07, 2025
  • PPRA yatoa mafunzo ya Ununuzi kwa watumishi wa Afya Chalinze

    May 07, 2025
  • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango yafanya ziara kukagua miradi ya maendeleo

    May 06, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.