• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Kamati ya Siasa Mkoa yakagua Viwanda

Imewekwa: August 17th, 2018

Kamati ya Siasa ya Halmashauri kuu ya Mkoa wa Pwani leo imekagua na kuona uzalishaji katika viwanda vya Sayona Fruits Ltd na Twyford vilivyo katika Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze.Ziara hiyo imeongozwa na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Pwani Mheshimiwa Ramadhani Maneno na Viongozi mbalimbali wa serikali wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo.

Ziara hiyo imekagua Kiwanda cha Sayona Fruits Ltd kinachotengeneza vinywaji mbalimbali vinavyotokana na matunda,kiwanda hicho kipo katika kijiji cha Mboga kata ya Msoga,hali kadhalika kamati ya siasa Mkoa ilifika katika kijiji cha Pingo kata ya Pera na kukagua uzalishaji wa vigae katika kiwanda cha Twyford.

Kwa mujibu wa Afisa Uhusiano wa kiwanda cha Sayona Bwana Abubakar Mlawa akitoa taarifa fupi ya kiwanda hicho,alieleza kuwa kiwanda hicho mpaka sasa kina thamani ya Dola za Kimarekani zaidi ya milioni 55,na kimetoa ajira kwa watanzania zaidi ya 800 ambao wameajiriwa kiwandani hapo.Aidha kiwanda hicho kinashiriki katika kutoa huduma za jamii kwa wakazi wa Chalinze kama ujenzi wa nyumba ya Mganga na uchangiaji wa ujenzi wa miundombinu ya Elimu katika shule ya sekondari Lugoba.”Kiwanda hiki pia kinawawezesha wananchi wa Chalinze na maeneo jirani kuwapatia soko la matunda wanayolima kwani kiwanda hiki kwa siku kinahitaji tani 300 za matunda .”Mlawa alisema.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo alitoa wito kwa serikali za vijiji na mamlaka za serikali za mitaa kufungua fursa kwa wawekezaji wa viwanda na kuondokana na urasimu wa kutoa ardhi kwani kauli mbiu yetu ni kuwa na viwanda vya kutosha,viwanda ambavyo vitatoa ajira kwa wananchi hususan wakulima wa matunda.”Sayona wanahitaji matunda tani 300 kwa siku hivyo wakulima wa matunda kwa sasa soko la matunda siyo changamoto tena bali ni wananchi kulima kitaalamu ili kuzalisha matunda yenye ubora kwa matumizi ya viwandani.”Ndikilo alisema.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Pwani ,Ramadhani Maneno ameushukuru uongozi wa kampuni ya Sayona kuiruhusu kamati ya siasa Mkoa kukagua na kuona hali ya uzalishaji wa bidhaa zitokanazo na matunda na kumshukuru mwekezaji kwa juhudi anazozifanya katika kuisadia jamii inayozunguka kiwanda kwa kuwapatia ajira,kununua matunda yanayolimwa na wananchi na kulipa kodi ambayo  ni chanzo cha mapato kwa serikali.

 Aidha Mheshimiwa Maneno aliongezea kwa kusema kuwa; Uungwana wetu wa kuitunza ardhi ni matokeo ya mafanikio kwa Mkoa wa Pwani  kuwa ni Mkoa wa viwanda,kwani uungwana wetu wa kuithamini ardhi kwa kutoiuza, pamoja na umasikini wetu tuliokuwa nao hatukuweza kushawishika na kuiuza.”Mwenyekiti wa Mkoa alisema

Wajumbe wa kamati ya siasa mkoa katika picha ya pamoja baada ya kumaliza kukagua shughuli za uzalishaji katika kiwanda cha vigae cha Twyford

kilichopo katika kijiji cha Pingo(wa saba kutoka kulia) ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Pwani,Mhe,Ramadhani Maneno.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • TANGAZO LA KAZI June 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Waziri Kikwete Apokea Hundi ya Tsh Milioni 52 kutoka kiwanda cha Keda

    June 21, 2025
  • Chalinze yapongezwa kwa Hati Safi Mfululizo miaka mitano

    June 18, 2025
  • Mwenyekiti wa UWT akagua miradi ya maendeleo Chalinze

    June 13, 2025
  • Madiwani wa Pangani waipongeza Chalinze kwa Miradi ya mapato ya ndani

    June 11, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.