• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Maadhimisho ya wiki ya elimu ya watu wazima yafanyika Chalinze

Imewekwa: September 3rd, 2025



Maadhimisho ya Wiki ya Elimu ya Watu Wazima na Elimu Nje ya Mfumo Rasmi yamefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Shule ya Sekondari Lugoba, iliyopo ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze. Tukio hilo limewakutanisha wadau mbalimbali wa elimu wakiwemo walimu wakuu wa shule za msingi na sekondari, maafisa elimu kata pamoja na wajasiriamali wanaotengeneza bidhaa mbalimbali kwa matumizi ya binadamu.


Akizungumza katika maadhimisho hayo, Afisa Elimu ya Watu Wazima wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze, Mwalimu Selemani Nkunguu, aliwasilisha taarifa ya utekelezaji wa shughuli za elimu ya watu wazima kwa mgeni rasmi. Alieleza kuwa, halmashauri imepata mafanikio makubwa katika kuwafikia watu wazima pamoja na wanafunzi wa kike waliokwama kuendelea na elimu kutokana na sababu mbalimbali kama vile kupata ujauzito wakiwa bado shuleni.


Mwalimu Nkunguu alibainisha kuwa elimu ya watu wazima na elimu nje ya mfumo rasmi imekuwa na mafanikio makubwa kupitia mifumo kama MEMKWA (Mpango wa Elimu ya Msingi kwa Waliokosa) na MUKEJA (Mpango wa Kuendeleza Elimu ya Juu kwa Waliokatishwa). Pia, alieleza kuwa walimu wengi wa shule za msingi na sekondari wamejiendeleza kitaaluma kupitia elimu ya masafa, hatua ambayo imewawezesha kutoa mchango mkubwa katika jamii.


Aidha, Nkunguu alisisitiza kuwa mafanikio haya yametokana na juhudi za serikali ya awamu ya sita kupitia sera zake nzuri zinazolenga kutoa fursa sawa za elimu kwa makundi yote ya wananchi, hususan waliokosa fursa ya kupata elimu katika mfumo rasmi. Hii imechangia kuongeza idadi ya wananchi wanaoweza kusoma na kuandika, pamoja na kuwawezesha kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo.


Kwa upande wake, Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo ambaye pia ni Afisa Tarafa ya Msata, Bi. Jesca Samson, aliipongeza Halmashauri ya Chalinze kwa juhudi zake madhubuti katika kuhakikisha elimu inawafikia wananchi wote. Alisema kuwa jitihada hizo zimekuwa msaada mkubwa kwa wananchi waliokatishwa masomo, kwani sasa wanaweza kutimiza ndoto zao kwa kupata maarifa yanayowawezesha kubadilisha maisha yao.


Bi. Jesca alieleza kuwa elimu ya watu wazima inasaidia kupunguza ujinga na kuongeza maarifa kwa wananchi, hivyo kusaidia kuinua kipato cha familia na taifa kwa ujumla. Alisisitiza kuwa elimu si kwa ajili ya watoto pekee, bali ni haki ya kila Mtanzania na kwamba kila mmoja anapaswa kutumia fursa hii kujifunza na kujiendeleza.


Katika hotuba yake, mgeni rasmi wa maadhimisho hayo aliwataka wananchi wa Chalinze na maeneo mengine nchini kuendana na kaulimbiu ya mwaka huu isemayo: “Kukuza Kisomo katika Zama za Kidijitali kwa Maendeleo Endelevu ya Taifa Letu.” Alieleza kuwa teknolojia ya kidijitali imefungua fursa nyingi na ni muhimu kwa wananchi kujiendeleza kielimu ili waweze kuzitumia kikamilifu.


Mgeni rasmi alihitimisha kwa kutoa wito kwa wadau wa elimu, viongozi wa serikali za mitaa na jamii kwa ujumla kuendelea kushirikiana katika kuhamasisha elimu ya watu wazima. Alisisitiza kuwa hakuna maendeleo ya kweli bila wananchi kuwa na uelewa wa masuala mbalimbali ya kijamii, kiuchumi na kisiasa kupitia elimu.


Maadhimisho hayo yalihitimishwa kwa maonesho ya bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na wajasiriamali waliopata mafunzo kupitia elimu nje ya mfumo rasmi. Maonesho hayo yalionyesha jinsi elimu inavyoweza kubadilisha maisha ya wananchi kwa kuwapa maarifa ya kuzalisha, kuendesha biashara na kujitegemea kiuchumi.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • TANGAZO LA KAZI June 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Maadhimisho ya wiki ya elimu ya watu wazima yafanyika Chalinze

    September 03, 2025
  • Tume ya Utumishi wa Umma Kufanya Ukaguzi Chalinze

    September 01, 2025
  • Mafunzo kwa wasimamizi wasaidizi ngazi ya kata yafunguliwa Rasmi

    August 04, 2025
  • Maandalizi ya Maonyesho ya Nanenane kanda ya Mashariki yapamba moto

    July 29, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.