• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Madiwani wa Chalinze wafurahia uchakataji wa maziwa kiwanda cha ASAS

Imewekwa: May 27th, 2025


Na John Mlyambate, Iringa


Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze mkoani Pwani leo wametembelea kiwanda cha kuchakata maziwa cha ASAS kilichopo katika Manispaa ya Iringa, mkoani Iringa, na kufurahishwa na namna shughuli za uzalishaji wa maziwa zinavyotekelezwa kwa weledi na ubora wa hali ya juu.


Ziara hiyo ni sehemu ya mafunzo kwa viongozi hao wa kisiasa ili kujifunza mbinu bora za uchakataji wa mazao ya mifugo, hasa maziwa, kwa lengo la kuchochea maendeleo ya sekta hiyo katika Halmashauri ya Chalinze. Wakiwa kiwandani hapo, madiwani walipata fursa ya kuona hatua zote za uzalishaji wa maziwa kuanzia mapokezi ya maziwa ghafi, uhifadhi, vipimo vya ubora, uchakataji hadi kufungashwa kwa ajili ya kuingia sokoni.


Madiwani walionesha hamu ya kufahamu kwa kina namna kiwanda hicho kinavyopata maziwa kutoka kwa wafugaji wadogo, na mfumo wa ukusanyaji wa maziwa hayo kutoka vijijini hadi kufikishwa kiwandani. Wakizungumza na menejimenti ya kiwanda, walielezwa kuwa kuna mtandao wa mawakala wanaoshirikiana na wafugaji katika kukusanya maziwa kutoka maeneo mbalimbali ndani na nje ya mkoa wa Iringa.


Kwa mujibu wa Meneja Uendeshaji wa Kiwanda hicho, Bwana Lipita Mtimila, kiwanda hicho hupokea maziwa kutoka kwa wafugaji zaidi ya 2,000 kila siku, ambapo ushirikiano wa karibu kati ya kiwanda na wakulima umechangia katika kuboresha ubora wa maziwa na kuongeza kipato kwa jamii zinazozalisha bidhaa hiyo.


Mbali na kutembelea kiwanda, madiwani pamoja na wataalamu wa Halmashauri ya Chalinze walifika katika shamba la mifugo la ASAS lililopo Matembo, nje kidogo ya Manispaa ya Iringa, ambapo walijionea shughuli za ufugaji wa kisasa wa ng’ombe wa maziwa na jinsi wanavyohudumiwa kwa njia bora za kisayansi ili kuongeza uzalishaji.


Ziara hiyo imewawezesha madiwani kupata uelewa mpana wa mnyororo wa thamani wa maziwa na fursa zilizopo katika sekta hiyo, ambapo waliahidi kuyatumia mafunzo hayo kuhamasisha uwekezaji katika viwanda vidogo na vya kati vya kuchakata mazao ya mifugo katika Halmashauri ya Chalinze.


Kwa upande wao, baadhi ya madiwani walisema ziara hiyo imewafungua macho kuhusu namna sekta binafsi inavyoweza kushirikiana na serikali katika kuongeza ajira, kipato na usalama wa chakula, wakiahidi kuhamasisha mifumo bora ya ufugaji na ukusanyaji wa maziwa katika maeneo yao.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • TANGAZO LA KAZI June 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Maandalizi ya Maonyesho ya Nanenane kanda ya Mashariki yapamba moto

    July 29, 2025
  • Halmashauri ya wilaya ya Chalinze kujenga kituo cha mafuta kwa mapato ya ndani

    July 16, 2025
  • Mkurugenzi Mtendaji Chalinze Atembelea maonyesho ya 49 ya Saba saba

    July 14, 2025
  • Walimu wapewa maelekezo ya kazi Chalinze

    July 10, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.