Ofisi ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,imetoa mafunzo ya kilimo kwa Vijana kwa kutumia Teknolojia ya Kitalu Nyumba(Green House) kwa vijana wapatao 100 katika Halmashauri ya Chalinze hivi karibuni.
Mafunzo hayo yametolewa katika Kijiji cha Lugoba kwa kujumuisha vijana wa kata za Bwilingu,Pera,Msoga,Lugoba,Kiwangwa,Msata na Mandela. Mafunzo haya yametolewa ili kuwajengea uwezo vijana ili kuwavutia kutafuta maarifa na kujianiri katika sekta ya kilimo na Kilimo biashara. Matumizi ya Teknolojia mbalimbali katika kilimo duniani kote yameonyesha kuwavutia vijana katika kilimo na kuwapa tija na ufanisi kibiashara.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chalinze,Hassan Mwinyikondo akifunga Mafunzo hayo aliishukuru serikali ya awamu ya sita kwa jitihada zake za kuwakwamua vijana kiuchumi kwa kuwapa maarifa wezeshi yanayowawezesha kupambana na umaskini kipitia kilimo cha kutumia Vitalu Nyumba kwa kilimo chenye tija.
Mwinyikondo aliwataka Vijana kuyatumia maarifa waliyoyapata kwa weledi na kwa faida yao na jamii kwa ujumla ili kujikwamua kiuchumi ili kufikia azima ya serikali na ilani ya Chama cha Mapinduzi kwa Ujumla.
Katika hotuba yake ya kuhitimisha mafunzo Mwenyekiti aliwataka vijana wahitimu kujiunga katika vikundi ili halmashauri iweze kuwapatia mikopo ya kujenga vitalu nyumba kutokana na asilimia 10 ya mapato ya ndani ya Halmashauri.
“Mafunzo haya yakawe chachu ya mafanikio na maarifa mliyoyapata mkayatumie kwa vitendo na kuwawezesha pia vijana wenzenu ambao hawajayapata mafunzo haya na hatimaye mkapate mikopo ambayo itatumika katika kilimo cha vitalu nyumba.”Mwinyikondo alisema.
Naye Mkuu wa Idara ya Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika,Bwana Jovin Bararata aliishukuru Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kutoa mafunzo kwa vijana kuhusu Kilimo cha Kisasa na utumizi wa Vitalu nyumba kwa kilimo chenye tija ,hali ambayo itawafanya vijana kukipenda kilimo kinachotumia teknolojia ya kitalu nyumba kwa uzalishaji wenye tija.
Aidha Bararata aliahidi kuwa mafunzo haya yatakuwa endelevu kwa vijana ili waweze kupambana na umasikini kupitia teknolojia ya kilimo inayotumia vitalu nyumba.
“ Idara ya kilimo tunaahidi kuendelea kuwajengea uwezo vijana juu ya utumizi wa vitalu nyumba katika Halmashauri ya Chalinze kwa kuhakikisha kila kata Teknolojia hii inatumika kwa ufasaha ili kuwavutia vijana kukipenda kilimo kama mkombozi katika jamii.” Bararata alisema.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chalinze akifunga Mafunzo kwa Vijana
114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu
Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze
Simu: +255232935403
Simu ya mkononi:
Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz
Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.