• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Mhe. Ridhiwani Kikwete awataka wataalamu kusimamia miradi kama ilivyopangwa

Imewekwa: February 21st, 2023



Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mhe.Ridhiwani Kikwete amesema ili wananchi wanufaike na miradi inayotengewa fedha za Serikali ni vema wataalamu kuisimamia miradi hiyo itekelezwe kama ilivyopangwa na kupunguza kero kwa wananchi.


Mhe.Ridhiwani ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ameyasema hayo alipokuwa katika ziara yake kwenye kata kuzungumza na wananchi na kusikiliza kero zao.


"Wataalamu katika maeneo ambao mmetoa ahadi kufanya kazi kukamilisha miradi na kutatua kero za wananchi naombeni mkatekeleze hayo yapo maeneo ambayo ni maalumu yanatakiwa utekelezaji waharaka kuondoa vikwazo vya shughuli nyongine kwa wananchi" amesema .


Amesema Serikali imekuwa ikitenga fedha kwa ajili ya kutatua vikwazo kwa wananchi ili waweze kufanya shughuli zao za kuwakwamua kimaendeleo hivyo wanaopewa jukumu la kusimamia wanatakiwa kufanya hivyo kwa kutokuwa kikwazo.


Akizungumzia kero ya maji amesema upo mradi wa maji Wami unaotekelezwa ambao unatarajia kugharimu biln 44 ambao utakwenda kuondoa kero ya ukosekanaji wa maji kwenye baadhi ya maeneo ambao unachangiwa na baadhi ya mabomba kuchakaa na mengine kupasuka.


Mhe Ridhiwani amesema fedha mradi huo ambao unatarijiwa kukamilika mwishoni mwa Machi mwaka huu tayari  zimetolewa na mkandarasi anaendelea na kazi katika maeneo mbalimbali ya Halmashauri ya Chalinze.


"DAWASA waelewe Rais Samia Suluhu Hassan anarudisha fedha kwa wananchi kwa njia ya kutekeleza miradi ya maendeleo hivyo hakikisheni mradi unatekelezwa kwa wakati wananchi wanufaike nao" amesema


Mhe.Ridhiwani anafanya ziara katika maeneo mbalimbali ya jimbo la  chalinze kusikiliza ba kutia majibu kwa baadhi ya kero za wananchi ambapo kero nyingi zilizoainishwa ni pamoja na maji, migogoro ya ardhi  na barabara.


Awali akizungumza katika mkutano uliofanyika Kijiji cha Hondogo Diwani wa Mandera Leon amemshukuru Mbunge huyo kwa namna anavyotoa fedha kutoka kwenye mfuko wa jimbo na kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo wa barabara, shule  na maji.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • PPRA yatoa Mafunzo ya NeST kwa Watendaji wa Kata na Wakuu wa Shule Chalinze

    May 08, 2025
  • Watendaji wa Kata na Vijiji wapewa Mafunzo ya namna ya kukusanya Kodi ya Majengo Chalinze

    May 07, 2025
  • PPRA yatoa mafunzo ya Ununuzi kwa watumishi wa Afya Chalinze

    May 07, 2025
  • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango yafanya ziara kukagua miradi ya maendeleo

    May 06, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.