• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete akabidhi vifaa vya kujifunzia Mazizi

Imewekwa: January 6th, 2023

Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete akabidhi vifaa vya kujifunzia Mazizi 

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Ridhiwani Kikwete(Mb) akabidhi vifaa vya Elimu kwa ajili ya kujifunzia wanafunzi wa Shule ya Msingi Mazizi. Vifaa alivyokabidhi ni Madaftari makubwa (Counter book Quire 2) yapatayo 720,kalamu 1000,daftari ndogo 1440,mabegi ya kubebea madaftari,vifaa vya kuchorea,vifutio na vichongeo.


Vifaa hivyo vimetolewa na Bwana Kant ambaye ni mmiliki wa Kampuni ya Shiram Construction Limited inayojishughulisha na shughuli za Ujenzi katika Kijiji cha Mazizi. Kwa mujibu wa taarifa iliyosomwa na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mazizi,kampuni hii ni mdau mkubwa katika masuala ya Elimu katika kijiji cha Mazizi kwa kutoa misaada mbalimbali ya vifaa vya Elimu ili kuboresha mazingira ya kujifunzia.


Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete ambaye alikuwa Mgeni rasmi katika hafla fupi ya kukabidhi vifaa hivyo katika Ukumbi wa kijiji hicho aliipongeza Kampuni hiyo kwa moyo wa utoaji huduma kwa jamii kama mwekezaji na kuzitaka Kampuni zingine zilizowekeza katika halmashauri ya Chalinze kuiga mazuri yanayofanywa na Kampuni ya Shiram Construction Limited ili kutekeleza wito wa Serikali wa kuitaka sekta binafsi kuchangia shughuli za Maendeleo katika maeneo zinakowekeza.


Naye Diwani wa kata ya Msata na Mwenyekiti wa kamati ya Elimu Afya na Maji,Mheshimiwa Selestine Semiono alimpongeza Mheshimiwa Mbunge kwa kukubali wito wa kuja kukabidhi vifaa hivyo na kutoa shukrani zake kwa Serikali ya awamu ya sita jinsi ilivyoweza kuleta fedha za miradi ya Maendeleo katika kata yake ya Msata.


Aidha aliishukuru Serikali kwa kufungua barabara katika maeneo korofi ambayo yalikuwa hayafikiki kipindi cha nyuma lakini sasa panafikika na akamwomba Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete kuendelea kuiboresha barabara hiyo.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • PPRA yatoa Mafunzo ya NeST kwa Watendaji wa Kata na Wakuu wa Shule Chalinze

    May 08, 2025
  • Watendaji wa Kata na Vijiji wapewa Mafunzo ya namna ya kukusanya Kodi ya Majengo Chalinze

    May 07, 2025
  • PPRA yatoa mafunzo ya Ununuzi kwa watumishi wa Afya Chalinze

    May 07, 2025
  • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango yafanya ziara kukagua miradi ya maendeleo

    May 06, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.