• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI apongeza Utekelezaji wa Sekta ya Afya Chalinze

Imewekwa: June 3rd, 2025


Na John Mlyambate


Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia masuala ya Afya, Profesa Tumaini Joseph Nagu, leo amefanya ziara ya kikazi katika Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze akiwa ameambatana na timu ya wataalamu kutoka TAMISEMI kwa lengo la kukagua na kujionea maendeleo ya sekta ya afya katika halmashauri hiyo.


Profesa Nagu alianza ziara yake kwa kutembelea Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Chalinze kisha kuelekea katika Kituo cha Afya Chalinze ambapo alikagua miundombinu mbalimbali ikiwemo majengo ya huduma za afya na vifaa tiba vinavyotumika katika utoaji wa huduma kwa wananchi.


Katika ukaguzi wake, Naibu Katibu Mkuu alionesha kuridhishwa na hali ya miundombinu ilivyoboreshwa kwa ushirikiano kati ya serikali kuu na mapato ya ndani ya halmashauri. Alisema hatua hiyo inaakisi dhamira ya serikali ya awamu ya sita katika kuboresha huduma za afya nchini kwa lengo la kumrahisishia mwananchi kupata huduma bora karibu na makazi yake.


Profesa Nagu alipata fursa ya kuzungumza na baadhi ya wagonjwa waliokuwa wakipata huduma kituoni hapo, ambapo walieleza kufurahishwa na ubora wa huduma na kuwepo kwa vifaa tiba vya kisasa vinavyowezesha huduma kutolewa kwa haraka na kwa ufanisi.


Katika ziara hiyo, Profesa Nagu pia alitembelea na kukagua Duka la Dawa la Jamii lililopo katika Kituo cha Afya Chalinze. Alilipongeza duka hilo kwa kuwa la kisasa na lenye uwezo mkubwa wa kuhifadhi dawa, jambo linalosaidia wananchi kupata dawa kwa wakati bila usumbufu.


Msafara huo ulielekea pia katika Hospitali ya Wilaya ya Chalinze iliyopo Msoga, ambapo Profesa Nagu alikagua Kituo cha Dharura cha Matibabu (EMD) pamoja na majengo mbalimbali ya hospitali hiyo. Alifurahishwa na kiwango cha ujenzi wa miundombinu ya kisasa yenye viwango vinavyokidhi mahitaji ya utoaji wa huduma bora.


Akizungumza na watumishi wa sekta ya afya katika halmashauri hiyo, Profesa Nagu aliwapongeza kwa juhudi kubwa wanazozifanya katika kuwahudumia wananchi licha ya changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo kazini. Alisema serikali inatambua mchango wao na itaendelea kuboresha mazingira ya kazi.


Aliwahimiza watumishi hao kuendeleza moyo wa uzalendo kwa kutoa huduma kwa upendo na uadilifu kwa wananchi, pamoja na kuitunza miundombinu na vifaa tiba ili viweze kudumu kwa matumizi ya muda mrefu.


Profesa Nagu alisisitiza kuwa serikali ya awamu ya sita imejipanga kikamilifu kuhakikisha kila mtanzania anapata huduma bora za afya, na kwamba Chalinze ni mfano wa mafanikio ya utekelezaji wa mpango huo kutokana na usimamizi mzuri wa viongozi wa halmashauri hiyo.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • TANGAZO LA KAZI June 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • DC Ndemanga Aongoza Kikao cha Tathmini ya Utekelezaji wa Mkataba wa Lishe

    June 10, 2025
  • Mkutano Mkuu wa Kijiji cha Tukamisasa waazimia Mwenyekiti Kupisha Uchunguzi

    June 10, 2025
  • Waziri Kikwete atua Geneva kushiriki Mkutano wa 113 wa Shirika la kazi Duniani

    June 04, 2025
  • Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI apongeza Utekelezaji wa Sekta ya Afya Chalinze

    June 03, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.