• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Pongezi zatolewa Halmashauri ya Chalinze kwa kutekeleza miradi ya maendeleo kwa viwango

Imewekwa: April 25th, 2021

Hayo yamejiri leo tarehe 25.04.2021 katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze katika kikao cha majumuisho ya ziara ya kutembelea miradi ya maendeleo kati ya Katibu wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) taifa Ndugu Elirehema Kaaya na viongonzi wa Halmashauri, madiwa na wataalamu.

Awali akizungumza katika kikao hicho, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya chalinze Ndugu Ramadhani Possi alisema, “Ndugu Katibu wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) taifa Halmashauri ya Chalinze ilianza Mwaka 2016 baada ya Halmashauri ya kugawanywa toka Halmashauri ya Bagamoyo. Leo hii umekuja kujionea miradi inayotekelezwa kwa kupitia fedha za ndani na ruzuku kutoka serikali kuu. Miradi hiyo ikiwa ni Ujenzi wa Jengo la Halmashauri, Standi ya Mabasi, Soko la kisasa Choo cha kulipia na Uboreshaji wa Miundombinu ya Majengo katika Hospitali ya wilaya Msoga.

Aidha Ndugu Possi aliongeza kusema “kama Halmashauri tumetekeleza ujenzi wa Miradi hii kwa kutumia utaratibu wa Force Account kwa lengo la kupunguza gharama ili kuokoa baadhi ya fedha na kuzielekeza katika shughuli zingine. Katika hili Halmashauri ilipatiwa fedha kiasi cha Tsh. Bilioni moja kwaajili ya uboreshaji wa miundombinu Hospitali ya Wilaya Chalinze ili itekeleze ujenzi wa Majengo manne(4) kwa kutumia utaratibu wa force account imefanikiwa kujenga majengo sita kwa kiwango kilekile cha fedha”.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri Wilaya ya Chalinze, Mh: Geofrey Kamugisha alimshukuru Katibu wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) kufika Halmashauri ya Chalinze na kusema, “Ujio wako ni faraja kwetu kwani kwa niaba ya madiwani wenzangu zipo changamoto nyingi ambazo tunatamani utusaidie kuzifikisha mahali husika, ikiwemo Upungufu wa wafanyakazi kama walimu wa sanyansi kwa ajili ya shule za sekondari, watumishi wa afya na watumishi wengine kwenye kada mbalimbali hivyo ujio wako nimatarajio yetu kuwa tutapata ufumbuzi na kuondoa changamoto hiyo”.

Aidha Mh. Kamugisha aliongeza kuwa “Madiwa watafurahi kama stahiki zao zitaangaliwa kwa upya kwani muongozo unaotumika katika kutoa stahiki zao umetengenezwa Zaidi ya miaka 15 iliyopita hivyo kutoendana na uhalisia wa maisha ya waheshimiwa hawa kwa sasa, ni matumaini yetu kuwa jambo hili pia litashughulikiwa ili kuleta motisha kwa madiwani katika utendaji wao wa kazi katika maeneo yao.

Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete akizungumza mbele ya Katibu wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) taifa Ndugu Elirehema Kaaya alitoa masikitiko yake kutokana na mifumo ya ulipaji kodi iliopo hasa Service Levy, ambayo imekuwa ikiwakandamiza watu wa Chalinze kwani makampuni mengi yanayochimba madini Chalinze kodi hii hulipia Dar es Salaam kwa kuwa ofisi zao zipo huko na kutowanufaisha wanachalinze.

Ninaomba ukiwa kama katibu mkuu wa ALAT taifa katika vikao vyenu vya ALAT kupitia sekletarieti utufikishie malalamiko yetu ya kupunjwa mapato ya Halmashauri yetu, kwani katika swala la uchimbaji madini Halmashauri hulipwa Kodi ya madini ya Halmashauri tu na Service Levy kutokulipwa. Jambo hili katika Mkoa wa Pwani linazikumba Halmashauri nyingi. Hivyo ujio wako ni furaha kwetu kwani tunategemea kuwa jambo hili litafanyiwa kazi kwa haraka ili Halmashauri yetu iweze kuongeza kipato kupitia chanzo hicho kwani zaidi ya 15% hadi 20% ya mapato ambayo yalitakiwa kuwa Chalinze yanakwenda kwenye Halimashauri za Mkoa wa Dar es Salaam Alisema Mh. Kikwete

Nae Katibu wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) taifa Ndugu Elirehema Kaaya, Aliwapongeza viongozi wa Halmashauri ya Chalinze kwa utekelezaji mzuri wa miradi ya maendeleo kwani katika miradi yote alioitembelea amekuta miradi imejengwa kwa viwango vya hali ya juu na dhamani ya fedha ukulinganisha na utekelezaji ipo katika Uhalisia.

Ni hakika kuwa Halmashuri ya Chalinze Mmepata viongozi mahiri Ukianzia Mbunge wenu Mh. Ridhiwani Kikwete, Mwenyekiti Mh. Geofrey Kamugisha, Mkurugenzi Mtendaji Ndugu Ramadhani Possi na Madiwani wote, Kitu kikubwa nilichojifunza kutoka kwenu ni kuwa  mihimiri yote hii ya uongozi mnanafanya kazi kwa kushirikiana ndio maana mmeweza kufika hapa mlipo fika. Wito wangu kwenu ni kuwa muendeleze ushirikiano huo ili Halmashauri iweze kufika mbali zaidi katika maswala ya maendeleo.

Katika ziara yangu yapo mambo mengi mazuri nimejionea lakini upo ushauri wa msingi nataka kuwapatia, Mnapoendelea na uboreshaji wa Miundombimu ya majengo Hospitari ya Msoga ni vema mfikirie swala la uwekaji wa uzio katika mipaka, hata kama uwekaji wa ukuta utakuwa gharama ni vyema mpande hata miti za uzio kuzunguka eneo lote la Hospitali kwani itasaidia kuhifadhi mazingira, kupendezesha eneo na kuzui wavamizi, jambo la pili katika maeneo ambayo kunahitajika maji ya kutosha ni pamoja na Hospitari, sijaona miundombinu ya kuvuna maji ya mvua hivyo kama Halmashauri fanyeni utaratibu wa kufanya tathimini na kuweka miundombinu hiyo ili maji yatakayopatikana yasaidie katika swala zima la kufanya usafi na kuboresha mazingira kwa kuzuia maji kutiririka hovyo kitukinachopelekea mmomonyoko wa udongo.

Aidha aliwasihi madiwani na wataalamu kuwa watulivu wakati changamoto ambazo wamezieleza zikishughurikiwa.  “Kuhusu changamoto za upungufu wa watumishi ikiwemo walimu, watumishi wa afya na utawala naomba nilibebe kama lilivyo na kulifikisha katika ofisi husika. Pia katika sehemu nyingi nilizokuwa nikipita kumekuwa na malalamiko mengi kuhusu stahiki za madiwani hivyo naomba kwa kupitia viongozi wao wa alat mkoa naomba mlilete ili tulifikishe katika mkutano mkuu wa taifa kwani jambo hili hata Bungeni limezungumziwa hivyo Waziri wa TAMISEMI Mh: Ummy Mwalimu alilijibia na kusema wamelipokea na wanalifanyia kazi hivyo tuwe na subira wakati swala hili likishughurikiwa

Mwenyekiti wa Halmashauri Wilaya ya Chalinze, Mh: Geofrey Kamugisha akisalimiana na 

Katibu wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) taifa Ndugu Elirehema Kaaya Mara

baada ya kutembelea ofisini kwake

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Chalinze Ndugu Ramadhani Possi(Aliesimama) akitoa

neo la utangulizi Mbele ya Katibu wa Jumuiya ya Tawala  za  Mitaa     Tanzania (ALAT) taifa 

Ndugu Elirehema Kaaya kabla ya kutembele miradi ya maendeleo inayotekelezya Chalinze

Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete(Wakatikati aliyevaa Miwani) akifafanua jambo

 katika Mradi wa soko  linalojengwa kwa fedha za mapato ya ndani mbele ya Katibu wa Jumuiya ya 

Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) taifa Ndugu Elirehema Kaaya

.


Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • TANGAZO LA KAZI June 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Waziri Kikwete Apokea Hundi ya Tsh Milioni 52 kutoka kiwanda cha Keda

    June 21, 2025
  • Chalinze yapongezwa kwa Hati Safi Mfululizo miaka mitano

    June 18, 2025
  • Mwenyekiti wa UWT akagua miradi ya maendeleo Chalinze

    June 13, 2025
  • Madiwani wa Pangani waipongeza Chalinze kwa Miradi ya mapato ya ndani

    June 11, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.