• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Soko la kisasa Halmashauri ya Chalinze kuamilika Juni 2021

Imewekwa: April 9th, 2021

Kamati ya siasa ya Mkoa wa Pwani imefanya ziara kutembelea miradi mbalimbali inayotekwelezwa Halmashauri ya Chalinze. Kamati hiyo ikiongonzwa na Mwenyekiti wake Mh. Ramadhani Maneno imetembelea Ujenzi wa soko la kisasa lililopo kata ya Bwilingu linalojengwa kupitia mapato ya ndani.

Akisoma Taarifa mbele ya kamati hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Chalinze Ndugu: Ramadhani Possi alisema “Mradi wa soko kwa awamu ya kwanza unagharimu Kiasi Cha Tsh Milioni 472 na kutokana na Maelekezo ya Kamati ya fedha Mipango na Uongozi Halmashauri imefanya upanuzi wa Soko hilo na Kuongeza Sehemu nyingine ambayo inagharimu kiasi cha Tsh Milioni 200. Mradi huu wa soko tulitegemea ukamilike Mwisho wa mwezi wa nne lakini mkandarasi ameomba tumpe muda hadi mwisho wa Mwezi wa tano mwaka huu, Mapema mwezi juni huduma zitaanza kutolewa katika soko hili la kisasa”

“Mradi wa soko una jumla ya vizimba 160 na kutokana na maelekezo ya kamati ya Fedha, Mipango na Uongozi tutajengwa fremu za maduka ya Kupangisha visivyopungua 180 na tayari tumekwisha jenga choo cha kulipia ambavyo hivi vyote vitakuwa ni vyanzo vipya vya mapato vitakavyo saidia kukuza pato la Chalinze” Aliongeza Ndugu: Possi.

Aidha Ndugu Possi, aliwashukuru wananchi wa chalinze hususani wamiliki vibanda sehemu ambayo limejengwa soko jipya kwa ushirikiano wao, mara baada ya kuelezwa adhima ya serikali kujenga soko hilo na kuwataka kuhama walianza kubomoa vibanda vyao vya zamani wenyewe hivyo kuleta urahisi kwa mkandarasi kuendelea na kazi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Mkoa Mh. Ramadhani Maneno kwa niaaba ya kamati ya siasa Mkoa, aliupongeza Uongozi wa Chalinze Chini ya Mwenyekiti wa Halmashauri Mh. Geofrey Kamugisha, Madiwani wote, Mkurugenzi Mtendaji Ndugu: Ramadhani Possi na wataaramu, kwa kazi nzuri wanazoendelea kufanya Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze hususani usimamizi wa miradi ya maendele kwa viwango.

“Nimefurahishwa sana na hiki ninachokiona Chalinze kwenye Mradi huu wa soko, nimeridhika mno mno mno, nichelee kusema kuwa kwa kweli Mkurugenzi mmepata mnahitaji kumpa ushirikiano wa kutosha katika utekelezaji wa miradi na majukumu mengine ndani ya Halmashauri. Wito wangu kwenu Madiwani ni kwamba muendelee kuonesha ushirikiano na wataalamu na kama kunasehemu ambapo mnaweza kuwasemea wapandishwe vyeo au madaraja fanyeni hivyo na msiwaonee kwa lolote kwani kwa kufanya hivyo mtakuwa mmewapa motisha na wanaweza fanya kazi nzuri zaidi” Alisema Mh. Maneno

Akihitimisha mazungumzo na Madiwani na Watendaji wa Halmashauri ya Chalinze Mh. Maneno alisema "Napenda kuwashukuru pia kwa namna ambavyo mmeendelea kutekeleza ilani ya chama cha mapinduzi  kwa usimamiaji wa miradi ya maendeleo kwa viwango na kwa ubunifu wa hali ya juu hasa katika swala la upunguzaji wa gharama kwa kutumia force Account, Ni wito wangu kwenu Madiwani na Wataalamu wote kujitahidi kutenda kazi zenu kwa kufuata miongozo na kwa haki ili kutokuigombanisha serikali na wananchi wake"

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • TANGAZO LA KAZI June 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Waziri Kikwete Apokea Hundi ya Tsh Milioni 52 kutoka kiwanda cha Keda

    June 21, 2025
  • Chalinze yapongezwa kwa Hati Safi Mfululizo miaka mitano

    June 18, 2025
  • Mwenyekiti wa UWT akagua miradi ya maendeleo Chalinze

    June 13, 2025
  • Madiwani wa Pangani waipongeza Chalinze kwa Miradi ya mapato ya ndani

    June 11, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.